K - Lyn ni mtu wa ku -spend ama kutafuta maisha?

Kama Huyo manzi alikuwa hajamchota mzee hela kpind cha uhai wake bas huyo demu atakuwa bonge la fala, alitakuwa mpak sa hv awe na reserve ya 50billion, badae mambo yakiwa kama hv unajikausha kama huoni, hata wakikupa shiling mia fresh tuu....
Una akili wewe
 
Huyo Jack nilimdharau toka nimfollow insta sabab anapost mapicha yaleyale tu ya maslay queen yaan nilitgemea kwa level yake angekua mhamasishaji flani au anapost baadhi ya projects kuhamasisha vijana.... ni mtu wa bata tu nadhani hajabadilika mtazamo
We nae we umefanyia nini vijana
Msitake kila mtu awe mpigania uhuru
 
Okey mkuu ila kila binadamu aliumbwa kwa upekee wake na kila mtu alipo anafit kwa namna yake.simaanishi kwamba hakuna wanaoishi maisha ambayo hawayastahili kutokana na vipawa Mungu alivyowapa ila kuna wengine wameumbwa jinsi walivyo ili kuleta ukamilifu flani. By the way kila nachofanya kinaleta impact, hata ninaponunua kitu chochote jua kuna mkulima au kiwanda kimepata pesa lakini humo humo kuna wafanyakazi wamepata mshahara na serikali ikapata kodi . Hiyo kodi ndio inatusababishia tujengewe huduma za kijamii unazoziona.

Sikatai kwenda extra miles lakini si kila mtu anaweza kwenda so jaribu tu kuheshimu life la wengine na kama unatoa ushauri bhasi toa katika position ya kutojiona wewe upo right zaidi kuliko mwenye life lake

Sent from my SM-G900F using JamiiForums mobile app
 
Unajua kuna kitu kinaitwa "Boldness "na kingine kinaitwa "Pride ".Usipokuwa makini unaweza dhani Boldness ni Pride na Pride ni Boldness. Mengi katika kitabu chake alipoandika
I can, I must, I will, Hakuwa na Pride bali alikuwa Bold kwamba haya mambo yanawezekana. Hali kadhalika mimi. Samahani kwa kushindwa kunielewa mkuu!
 
Unachokiongelea nimekielewa vizuri ila najaribu kukuonesha upande ambao wewe unahisi kama hautakiwi kuwepo.

Issue ni moja, kila kitu duniani kilianzishwa kwa diversity na binadamu tupo dynamic and diverse.Kufikiria kwamba kuna njia moja ambayo ni perfect kuiishi unakuwa unaenda kinyume ya nature yetu kama binadamu. Kila mtu ana kipawa, nafsi na matamanio yake katika kupata fullfillment, Binadamu tumetofautiana, wakati wengine wakitaka pesa kuna wengine wanataka fame and attention. Wakati wengine wakiamini katika biashara, wapo wanaomini katika taaluma au uongozi aidha wa kidini ama wa kawaida ili wawatumikie watu katika namna ambayo haitawapa pesa. So kuna wengine wanafanya kazi kiasi na wakipata muda hupumzika na kuinjoi life lao.

Life is really boring without diversity.. by the way lets agree to disagree. Uwe na siku njema
 
Kwa staili hiyo ya Maisha ni lazima udange hakuna namna. Kuna wasichana wanavaa nguo za mamilioni ya shilingi lakini vichwani hawana hata mpango mmoja wa kutafuta hela zaidi ya kutegemea miili yao kama kitega uchumi.
ila kazi ya kutafuta pesa (kula kwa jasho) ni yetu sisi wanaume mkuu. basi tu huwa tunataka kuwepa majukumu.
 
Kma ana furaha na maisha yake ya nini afanye yote hayo? Tatizo litakuja kama atakua haridhiki na hali hiyo alafu hachukui hatua...!
 
Boss inaonekana umestaarabika sana. Heko kwako
 
Kma ana furaha na maisha yake ya nini afanye yote hayo? Tatizo litakuja kama atakua haridhiki na hali hiyo alafu hachukui hatua...!
Kuridhika wewe tu huo ndio waitwa ubinafsi unajitenga na shida za wengine. Hata kwenye maombi utakuta unaomba, Mungu nibariki mimi, mke wangu na watoto wangu. Hukumbuki km kuna jirani, ndugu, jamaa, marafiki na wa Tanzania wote kwa ujumla. Mungu alikuleta duniani ili uweze kuwa na impact kwa watu wengine pia. Mfano mwalimu au daktari anaweza kuwa hatoi ajira kwa wengine lakini kwa kufundisha au kutibu kwa uaminifu na kwa bidii anakuwa amegusa maisha ya watu wengi kupitia taalum yake hiyo!
 
Sijaongelea kutoa pesa tu nimeongelea kuathiri jamii inayotuzunguka kwa njia chanya. Hata ukijitolea kufundisha watoto tuition kwa masaa 2 kila siku utakuwa umeiathiri jamii kwa njia moja au nyingine. Ninachomaanisha hapa ni kuacha kujifikiria sisi na maisha yetu tu, na kuachana na wengine!
 
Hakuna mtu ambaye anaishi asiguse maisha ya wengine mkuu, hata muokota makopo anagusa maisha ya jamii maana anasafisha mazingira. Mfanyakazi wa taasisi yeyote anagusa maisha ya jamii maana anazalisha jamii inatumia. Mtu yeyote anayeishi Duniani hawezi kuishi yeye kama yeye lazima ategemeane na jamii yake. Ila mwisho wa siku lazima kila mtu aishi maisha yake. Wewe ukitaka nifanye kama unavyofanya wewe ntakua naishi maisha yasiyo ya kwangu...! Haina maana ya wewe likizo yako iutumie kwenye mashamba yako na mimi nifanye kama wewe...

Mimi naweza kuamua kuingia pale kunduchi beach kwenda kurefresh mind na bado nikawa nimesaidia wengine...! Maana mimi kwenda pale inawawezesha wao kulipa Kodi na kuwezesha familia zao kuishi!
 
Imeandikwa ulapo au unywaji fanya kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 1Corithians 10:31.Kama wewe unaamini kulewa pombe kupitiliza ni fresh tu. Kumbuka kuna leo na kesho, utajibuje mbele za Mungu.
 
Imeandikwa ulapo au unywaji fanya kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 1Corithians 10:31.Kama wewe unaamini kulewa pombe kupitiliza ni fresh tu. Kumbuka kuna leo na kesho, utajibuje mbele za Mungu.
Ohoooo tumefika huko tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…