Kaa mbali na tapeli huyu Uttu Kingwande.

emkey

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
728
Reaction score
137
Wanajf, heshima kwenu.
Naomba niwajuze kuwa, kuna jamaa anamiliki computer kadhaa alizoweka shule ya msingi annex, lengo lake ni kuwafundisha walimu wa shule za msingi, cha ajabu walimu wake hawalipi mishahara na wahitimu hawapewi vyeti.
 
Tutampataje huyu jamaa kama madai haya ni ya kweli na kama ni ubaya unamwandikia tutathibitishaje kwa ushahidi ili sheria ifuate mkondo wake?
 
Wanajf, heshima kwenu.
Naomba niwajuze kuwa, kuna jamaa anamiliki computer kadhaa alizoweka shule ya msingi annex, lengo lake ni kuwafundisha walimu wa shule za msingi, cha ajabu walimu wake hawalipi mishahara na wahitimu hawapewi vyeti.
ametapeli shilingi milioni hamsini wananchi mbeya mjini alifungua kituo mbeya day secondary akahidi kuwapatia watu computer kwa bei nafuu yaani sh 70000 elfu sabini hakuleta computer wala redio kakimbia mpaka naandika haya mke wake amekamatwa jijini mbeya anashiliwa na jeshi la polisi kituo cha central
 
Mbeya ametapeli kwa kutumia au kwa kupitia ofisi za jiji yaani akishilikisha mkurugenzi na meya.Aliwambia ana wqfadhili wa kusaidia somo la computer mashuleni na akapewa hall laMbeya day.alikusanya wahitimu wa kidato cha nne 1000@sh.40,000/ .Pia akawambia mfadhili wake ametuma laptop kwa wanafunz atawauzia kwa Tsh.70,000/ wanafnunzi 150 wakatoa.Pia kwa kuhusisha jiji karibu shule zote alipitia na kuagiza kila mwanafunzi atoe1000/-kwa ajir ya kuandaa picha na fomu za komputer,kwa wastan kila shule sekondari na msingi ailamba 1,000,000/-mwishoni mbeya alionekana na gari mpya ya Noah yenye maneno"Papaa Noma".baada ya hapo waliobaki walisombwa na polisi.
 
Mliotapeliwa mbeya na huyu jamaa uttu kingwande njooni dsm nitawasaidia kuwapeleka anapoishi, ninapajua hadi nyumbani kwake. Ni-pm tuwasiliane.
 
wajinga ndio waliwao kekundu kekundu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…