Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kuna watu ambao hakika ni sumu katika maisha yetu na wanatuua kidogo kidogo bila wenyewe kujua,wanaweza kuwa ni wazazi,ndugu zetu,waume na wake zetu,wafanyakazi wenzetu na watu ambao tunakutana nao kila siku katika maisha yetu
Watu hawa watanyonya nguvu yako,na kukuacha hoi bini taabani,watapandikiza nguvu hasi katika maisha yako kwa matusi,kejeli,dharau,na kukukandamiza kwa kila namna,utajikuta unakufa pole pole bila kujijua.
Watakufanya upoteze thamani yako,raha yao kukuona unakuwa mtu na mwenye kukosa hadhi mbele za watu na jamii kwa ujumla,hawakawii kukutungia habar za uwongo ili mradi hadhi yako na heshima yako ipotee,kuwa makini sana
Wapo tayar kuhakikisha haufanikiwi katika maisha yako ya utafutaji,wakiwa nawe wanajifanya ni watu wema kwako lkn kiuhalisia wanakutakia mabaya katika maisha yako.
Kumbuka upweke ni wa mpito tu ni bora uwe mpweke kwa mda fulani kuliko kuwa karibu na watu hawa,kwani hathari ya kuwa na watu hawa maishani mwako ina madhara ya mda mrefu sana
Ni hayo tu!