]Juzi nimejiunga nikakuta kumbe zile dk 300 si kwa mitandao yote kama wanavyotangaza. Ukishajiunga unaambiwa dk150 ni tigo/tigo tu, na zilizobaki 150 ndo za mitandao mingine.
Hii ni kupotosha wateja mnapotangaza kuwa ni dk300 kwenda mitandao yote.
TCRA Mnasemaje hii ni sawa
Makampuni mengi ya biashara nchini, hasa ya simu hayako wazi (wanadanganya au kuhadaa wateja wao); mara nyingi kama sio zote hawaweki wazi au kueleza "Masharti na Vigezo kuzingatiwa".
Nashauri, kabla ya kuingia kwenye huduma zao waombe wakueleze haya "Masharti na Vigezo kuzingatiwa" kimaandishi ndio uingie. Ikiwa vinginevyo, nenda mbele mamlaka ya mawasiliano