Kabendera na wenzake lazima wabweke

Kabendera na wenzake lazima wabweke

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Uwepo wa Makonda ndani ya mfumo hakika si jambo rafiki kwa mafisadi na wezi wa mali za Umma.

Majambazi yale hutengeneza wigo mpana wa kutetewa na kusifiwa ili kwalo yaendelee kuiba, kuficha na kujinufaisha wao na watetezi wao.

Wazi inafahamika, Makonda pamoja na mapungufu yake kama binadamu angalau kwa kiasi fulani huwa upande wa wasumbukao na utapeli wa mafisadi na wezi wa mali za Umma.

Kwa sababu hiyo, watu aina ya Kabendera ambao kwa kivuli cha uhuru wa mawazo na kukosoa, hutumiwa sana ili kuwasema wale wote waonekanao ni kikwazo kwa maslahi ya laghai wale!

Lililo jema ni; nia ya watu kama kina Kabendera inafahamika. Na njia pekee ya kujishughilisha nao ni kuhangaisha na kuwafilisi wanao watuma huku waking'olewa ndani ya mfumo kuepusha yale yaliyompata kipenzi cha Watanzania wengi.

Shime bwana mdogo Makonda, usihangaike na mbwa mbwekaji bali hangaika na mwenye mbwa mbwekaji.
 
mwambie abadilshe sheria ya TAKUKURU ya mwaka 2007 ili wala rushwa wapelekwe moja kwa moja mahakamani tuone kama yeye atabaki uraiyani
wezi nwa wala rushwa wote wa nchi hii wanatoka chama cha MAKONDA na yeye ni miongoni mwa hao wezi na wala rushwa.
MSITUCHOSHE KWA NGONJERA ZENU ZA KITOTO HAPA
 
Back
Top Bottom