Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
- Thread starter
- #221
Hakuna niliposema imeondoa maana, wewe ndiye hujanielewa.yes kuandika hivyo haiondoi maana kwa kabendera ni mwandishi nadhani bwana kiranga atakua ameelewa
Jamani, kwani hatuwezi kuyakubali mazuri mengi yaliyomo katika kitabu cha Kabendera na pia bado tukakosoa kwa kuonesha mapungufu yanayoweza kuboreshwa?
Hivi wabongo wengine mnajua hata book review inakuwaje?
Kwa nini mnafanya mtu yeyote anayeonesha kitu cha kuboresha ana dismiss kitabu kizima?
Hamuoni kuwa kazi hii ya kuonesha mapungufu ni kazi ambayo Kabendera anahitaji kusaidiwa ili kutoa second edition bora zaidi ya kitabu hiki?
Kabendera kaandika kitabu kizuri, kitabu kinachohitajika, kitabu kinachohitaji uhakiki pia, lakini ni kitabu ambacho kina makosa bado.
Kaandika Bibi Titi Muhammed alikuwa muanzilishi wa TAA. This is not the case.
Kasema Dodoma ilikuwa designated kuwa capital mwaka 1915, this is misleading, Dodoma may have been identified to have the potential to be a capital in 1915.
Kakosea tarehe ya ajali na kufariki Edward Moringe Sokoine, kaziweka mwaka 1983 wakati zipo mwaka 1984.
Kakosea jina la Waziri wa Afya wa zamani, kamuandika Dr. Aaron Chidua, anaitwa Dr. Aaron Chiduo.
Kakosea jina la Jaji Nassoro Mnzavas. Kaandika Mzavas.
Wengine wanasema kakosea tarehe ya kukamatwa yeye mwenyewe, amekamatwa tarehe 29.
Haya ni makosa ya wazi tu ambayo tunayaona kwa sababu ni spelling za majina na tarehe. Lakini ni wazi kuna makosa zaidi.
Zitto Kabwe kajitokeza na kusema narrative ya alivyovyamia ofisi ya mkurugenzi wa usalama wa taifa ina makosa. Irekebishwe.
Absalom Kibanda kaomba radhi na kusema kuwa alipewa kazi ya ku proofred kitabu hakuifanya vizuri, kwq sababu hakukaa na kitabu kwa muda mrefu, sasa anaona kuna makosa ambayo yanatakiwa kurekebishwa. Huyu ni mtu aliyehusika sana kufanya mahojiano ya muhimu yaliyokuwa source za kitabu wakati Erick Kabendera yuko nje. Obviously kuna makosa mengine mengi ambayo si spelling na tarehe tu. Yarekebishwe tupate kitabu kizuri zaidi kwenye second edition au edition ya Kiswahili.
Haya ni makosa ambayo hata watu tunaofurahia kuandikwa hiki kitabu tuna wajibu wa kuyasema ili yasahihishwe tupate kitabu bora zaidi.
Kwa nini tunaweka false dichotomy fallacy kwamba mtu akionesha makosa ya kitabu, basi anakataa kwamba kitabu bado kina maana katika ile larger narrative yake?
That is a false dichotomy, the two things are not mutually exclusive options, this is not an issue of "ama ukikubali kitabu chote kama kilivyo, ama ukikatae kitabu chote kama kilivyo".
Naweza kukikubali kitabu kwa sehemu kubwa lakini pia nikaona makosa bado.
Kabendera hakuandika msahafu, na hata hiyo misahafu yenyewe hatuiamini hivyo.
Tukubali kukosolewa na kukosoana, kujisahihisha na kusahihishana, hii ni hoja muhimu ya kitabu cha Kabendera kwamba Magufuli hakukubali kujikosoa, kukosolewa, kujisahihisha wala kusahihishwa.