Kabila gani lina lafudhi nzuri ya Kiswahili Tanzania?

Nafkri Wasukuma mkuu
 
Ukienda Kenya, hata uwe Mbena, Mruguru, mmakonde n.k. ukiongea utasifiwa kuwa unaongea Kiswahili sanifu na lafudhi yenye mvuto.
 
Msikilize mama samia anaongea vizuri hadi raha...
 
Nadhani wakenya, ndiyo wanalafudhi nzuri zaidi
 
Wasukuma wana lafudhi nzuri sana na tone nzuri. Tone ya matumaini!
Wasukuma Wana Rafidhi nzuri sana.
Wasukuma ni kabila lenye lafudhi mbaya ya kuzungumza Kiswahili.
Hahaha, wasukuma tena!
Hawa wasukuma ni wale tu ambao walizaliwa na kukulia mjini na walianza kuongea Kiswahili kama lugha mama, yaani kama lugha ya kwanza. Hawa unakuta ni wale ambao hawajui kabisa kuongea Kisukuma, au kama wanajua kuongea basi walijifunza ukubwani wakiwa tayari wanajua Kiswahili kama lugha yao ya kwanza. Hata hivyo, hongera zao
 
Mtoa kama kitu hukifahamu ni busara kuuliza maana kwa namna ulivyolitumia hilo neno "lafudhi" ni dhahiri hukua na uhakika juu ya utamkaji au uandishi wake mara "r" mara "l".
Tukirudi katika mada ukanda wa Pwani kwa kiasi kikubwa ndio wenye lafudhi bora zaidi kwa maana asilimia kubwa zaidi ndio lugha mama yao. Note; nimesema kwa kiasi kikubwa sio wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…