sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Baada ya kumpa 5 Ndg. Masua Bwire jana, Usiku mzima nilikua nawaza, dirisha dogo la usajili la TPL linafungiliwa wiki kadhaa zijazo.. Je ni mchezaji gani Simba SC tumsajiri toka hizi timu za hapa Bongo??
1. Golikipa:
Kwa sasa Simba SC ina magolikipa bora kabisa nchini, Manula na Dida. Kwa kifupi tuna Tanzania 1 na Tanzania 2. Hapo sijamtaja golikipa bora wa michuano migumu barani Africa, ukiacha AFCON ambayo ni CECAFA.
2. Beki:
Beki ya Simba SC imesheheni vilivyo.. kuna vijana kuna wakongwe. Mfano akiumia kwasi kuna tshabalala, akiumia nyoni kuna juuko, akiumia wawa kuna mlipili, kuna kapombe n.k. Wachambuzi wa soka pamoja na Alex Kitenge wanakiri kua Simba SC ina beki imara zaidi nchini.
3. Viungo:
Hapa ndipo Mnyama alipotakata. Kuna kila aina ya kiungo unayemjua wewe dunia hii, na wote ni mafundi haswaaa. Mpaka sasa kuna viungo hawajatumika ipasavyo, ambapo naona kama wakienda mtaa wa 2 wanaingia moja kwa moja katika kikosi chao cha kwanza.
4. Ushambuliaji:
Package iliyopo huku ni balaa tupu. Kuna Okwi, MK14, Kichuya, Salamba, Bocco n.k Kwa kifupu Bongo hii hakuna mshambuliaji toka timu pinzani atakayethubutu kukaa hata benchi.
Sasa nadiriki kusema kabla dirisha dogo la usajili halijafunguliwa.. Si tushalifunga.
Tunasubiri kuwafahamu mabingwa wa CAF Confederation Cup na CAF Champions League, ili tuweze kusajili wachezaji toka hizo timu.. Hela si tunazo.. Hahaha.