Kabla dirisha dogo halijafunguliwa, Simba SC kashalifunga

Kabla dirisha dogo halijafunguliwa, Simba SC kashalifunga

Hapo,
Haruna Niyonzima,
Nicolas Gyan
James Ketoi
inabidi walipwe chao na waondolewe Msimbazi.
Halafu yatafutwe majembe mengine matatu ya kigeni katika nafasi ya Ushambuliaji.
Yaana yatafutwe majembe ya uhakika.
Hata likipatikana kwanza Jembe moja au mawili sio mbaya.
Hapo wanaostahili kuondoka ni Niyonzima tu Kotei ni back up ya Mkude hope umeona mechi ambazo hawakucheza kulikuwa na kupwaya Fulani kwenye kiungo labda Mzamiru apone haraka
 
Kwa hiyo Amunike hana akili timamu?
Chizi tu..Kama uliona interview ya Banda wakati wanaenda Cape Verde..aliwaonyesha viongozi wa Baroka videos za Ajibu wakavutiwa nae..wakamwambia amshawishi aende kukipiga bondeni....Coach angekuwa Sunday Oliseh au Okocha unafikiri wangemuacha???
 
Chizi tu..Kama uliona interview ya Banda wakati wanaenda Cape Verde..aliwaonyesha viongozi wa Baroka videos za Ajibu wakavutiwa nae..wakamwambia amshawishi aende kukipiga bondeni....Coach angekuwa Sunday Oliseh au Okocha unafikiri wangemuacha???
Hahaha.. Ikawaje sasa mpaka sasa bado yupo bongo?
 
Nimecheka hiyo namba 3 ulivyo malizia hoja yako
 
Mwenye pesa ni Mo Dewji na wala siyo Simba, mlivyo washamba mpaka mnajipachika eti nyinyi ndio wasemaji wa familia ya Dewji, hivi tangu lini mzaramo fukara awe msemaji wa muhindi Billionare?
Daaah sawa mkuu lakini si ndio tajiri wetu anaetufanya tusitembeze bakuli kama wale jiran zetu
 
Nimecheka hiyo namba 3 ulivyo malizia hoja yako
Hahaha.. Lakini ndo ukweli wenyewe huo Mkuu.. Imagine, Mzamiru, Mzee wa Makombora ya masafa marefu Ndemla, Niyonzima tukiwatupa kwenye kikosi chao lazima wageuke kua lulu.
 
Wale waliokua wanapiga kelele kuhusu msimamo wa ligi.. Baada ya mechi ya jana ya Stand vs Mwadui.. Mambo yako hivi..
binzubeirysportsonline_Bphek4rjc3V.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Jana nilikuwa nacheki mpira wa man u vs everton na ruvu shootng hakika mpira wa simba ulivutia zaidi ya wa man u
Yaani mpira mmecheza na wale watoto afu mnajisifia mna mpira mzuri kuliko man?
 
Baada ya kumpa 5 Ndg. Masua Bwire jana, Usiku mzima nilikua nawaza, dirisha dogo la usajili la TPL linafungiliwa wiki kadhaa zijazo.. Je ni mchezaji gani Simba SC tumsajiri toka hizi timu za hapa Bongo??

1. Golikipa:
Kwa sasa Simba SC ina magolikipa bora kabisa nchini, Manula na Dida. Kwa kifupi tuna Tanzania 1 na Tanzania 2. Hapo sijamtaja golikipa bora wa michuano migumu barani Africa, ukiacha AFCON ambayo ni CECAFA.

2. Beki:
Beki ya Simba SC imesheheni vilivyo.. kuna vijana kuna wakongwe. Mfano akiumia kwasi kuna tshabalala, akiumia nyoni kuna juuko, akiumia wawa kuna mlipili, kuna kapombe n.k. Wachambuzi wa soka pamoja na Alex Kitenge wanakiri kua Simba SC ina beki imara zaidi nchini.

3. Viungo:
Hapa ndipo Mnyama alipotakata. Kuna kila aina ya kiungo unayemjua wewe dunia hii, na wote ni mafundi haswaaa. Mpaka sasa kuna viungo hawajatumika ipasavyo, ambapo naona kama wakienda mtaa wa 2 wanaingia moja kwa moja katika kikosi chao cha kwanza.

4. Ushambuliaji:
Package iliyopo huku ni balaa tupu. Kuna Okwi, MK14, Kichuya, Salamba, Bocco n.k Kwa kifupu Bongo hii hakuna mshambuliaji toka timu pinzani atakayethubutu kukaa hata benchi.

Sasa nadiriki kusema kabla dirisha dogo la usajili halijafunguliwa.. Si tushalifunga.
Tunasubiri kuwafahamu mabingwa wa CAF Confederation Cup na CAF Champions League, ili tuweze kusajili wachezaji toka hizo timu.. Hela si tunazo.. Hahaha.
Mlipeni chake Niyonzima kufuatana na mkataba.
Kama Mwambeleko, anajuta kuingia Msimbazi.
 
Wale waliokua wanapiga kelele kuhusu msimamo wa ligi.. Baada ya mechi ya jana ya Stand vs Mwadui.. Mambo yako hivi..View attachment 915695
Hii ligi inauonevu mkubwa sana team nyingine bado ina mechi nane zingine kumi na mbili hauwezi kuwa mwanya wa kupanga matokeo huu.
Hii bodi ya ligi inaongozwa na vichwa maji hii tena maji ya tope
 
Hii ligi inauonevu mkubwa sana team nyingine bado ina mechi nane zingine kumi na mbili hauwezi kuwa mwanya wa kupanga matokeo huu.
Hii bodi ya ligi inaongozwa na vichwa maji hii tena maji ya tope
Yanga bhana..
1. Mlipangiwa mechi 3 za mwanzo ugenini.. Mkalalamika
2. Mkapangiwa mechi 11 nyumbani.. Mkafurahi
3. Sasa mpo nyuma mechi 2.. Mnapiga kelele, utafikiri hamtacheza hivyo viporo vyenu
 
Back
Top Bottom