adakiss23
JF-Expert Member
- Jan 23, 2011
- 4,732
- 4,901
Kwenye hii issue ninachokiona ni hivi.. hata jana mzee kinesi amelizungumzia pia ingawa kwa juu juu. Kipindi kile cha utawala wa Rage Makamu Mzee Kinesi baada ya Kaburu kujiuzulu. Wachezaji wengi wa Simba walipigwa chini baada ya kuona wanahujumu timu kama mnakumbuka kina Maftah Nyoso Boban na wengineo. Timu ikabaki nyeupe mno. Wakapandishwa watoto kibao wa Simba B kina Messi Hassan Isihaka Ndemla Rashid Mkoko Kiparamoto Gallas Hassan Hatibu walikuwa wengi karibu 13. Kuna baadhi walipewa mkataba wa miaka 3 wengine 2. Baadhi ya waliopewa miaka miwili ni Ndemla ambaye juzi juzi ameongeza mkataba mwingine n mmojawapo ambaye alipewa miaka mitatu ni nahodha wa sasa Hassan Isihaka ambaye simba juzi juzi nae kwakuwa alibakiza mwaka mmoja viongozi wamemwongezea miaka mingine miwili inakuwa mitatu pamoja na kumboreshea baadhi ya vipengele vya mkataba. Inawezekana hata messi alisaini mkataba wa miaka mitatu sababu kwa muda ule ni wachezaji wawili au watatu wa simba B walikuwa wanakuja vizuri ambao ni Messi n Mkude. Ingawa Mkude alipewa mkataba mapema sana msimu m1 kabla.