JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,744
Ili gari yenye gearbox ya automatic(automatic transmission) iweze kubadilisha gear kuna taarifa kuu mbili ni lazima zipokelewe na mfumo wa kompyuta(control unit) ndio gear zitaweza kubadilika. Taarifa hizo ni:-
1. Speed ambayo driving shaft/tairi zinazunguka.
2. Speed ambayo engine inazunguka(Engine RPM).
Au kwa lugha rahisi ili gari iweze kubadili gear ni lazima speed ya engine na speed ya gari zifahamike. Iwapo kimojawapo kati ya hivyo kitakosekana basi ni lazima kuwe na matatizo katika ubadilishaji wa gear au hata kukosa gear kabisa.
Sasa kama umeangalia kwa umakini, kimojawapo kati ya hivyo viwili kinahusiana na engine. Hivyo endapo speed ya engine haipandi vile inavyoyakiwa, gari haitobadilisha gear. Na shida haitakuwa gearbox ila ni engine.
Njia rahisi ya kuweza kujua kama shida ni gearbox au engine ni.
1. Endapo unaendesha gari na unaona ukikanyaga accelerator muungurumo wa engine/mshale wa RPM unaenda juu sana na gari inaenda kwa speed ndogo kuliko kawaida basi shida ipo kwenye gearbox.
2. Endapo unaendesha gari na unaona ukikanyaga accelerator muungurumo wa engine unabaki kawaida/mshale wa RPM haufiki hata 3 au kama inataka kuzima basi shida ni engine.
Mwisho
**********#############*************
Tunajihusisha na
1. Full Systems Diagnosis (Gharama ni Tsh. 50,000/= tu kwa gari zote ndogo)
2. Engine Diagnosis kwa brand yoyote ya gari. Gharama ni Tsh. 30,000/= tu
3. Repair Matatizo ya engine.
4. Repair matatizo ya Automatic Gearbox.
5. Kupima na kukagua gari kwa wanaotaka kununua gari zilizotumika.
6. Pia kama unahitaji gari used ambayo inafanya kazi vizuri tuwasiliane. Tutatatuta kuipima na kuhakikisha kuwa ni nzima kabla ya kukuita.