Kabla hujakubali kuolewa wakati humpendi mwanaume muwazie yule mwanaume anaekuoa kwa sababu anakupenda.

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,342
Reaction score
88,625
Naomba kudeclare interest kabla sijaenda mbali: Mimi ni muumini wa mapenzi. Naamini katika ndoa yenye mapenzi na sio sababu nyingine.

Nina rafiki yangu aliolewa siku kadhaa nyuma. Siku ya kuvalishwa pete nilienda nae ukweni kwao. Lakini hakuwa na furaha kabisa. Mpaka mawifi wanatuambia muambieni mwenzenu asmile basi hata kwenye picha tu.

Baada tukio wakati tunarudi nikamwambia huna furaha umelazimishwa kuolewa? Kama unaona humtaki huyu kaka una nafasi bado hii ni pete tu muache kuliko uje kumuumiza baadae. Akaniambia nitakujibu kesho. Kesho yake nikamuuliza tena umeamua kuolewa au kukatisha ndoa. Akaniambia naolewa ile jana nilikua excited. Lakini picha zake kila mtu alikua anasema hana furaha.

Akaja akaolewa. Lakini hana furaha kabisa. Jana akaanza kuniambia habari za talaka. Ndoa hata miezi mitatu haina. Nikamuuliza unakumbuka niilivyokuambia ukatishe kuolewa wakati umevalishwa pete? Kwanini unataka umuumize mumeo na anakupenda sana. Akanijibu tu aliolewa kwa sababu alikua na stress na alitaka kumridhisha mama yake ila hajioni kabisa kumpenda mumewe. Nikamwambia sasa utafanyaje. Akasema hajui ila anaona hayuko sehemu sahihi na haenjoy ndoa yake. Nilichomshauri nikamwambia fuata moyo wako ila kuachika ni aibu zaidi tena kwa tamaa zako wakati ulikuwa na nafasi ya kukataa ndoa toka mwanzo.

Namuonea sana huruma mume wake maana anampenda sana mkewe ila mke hampendi kiasi cha kutotaka kuzaa na mumewe. Ameolewa lakini bado ana mapenzi mazito kwa ex bf wake. Na anavyoongea ni kama anataka amzalie kabisa huyu ex wake wakati yeye mke wa mtu. Siku mumewe akija kujua kilicho ndani ya mke wake kama sio kumuua bas atamuua yeye maana wajeda mapenzi yanajuaga kuwaumiza kweli kweli.

Kwa wenzangu, sio lazima uolewe ndo uonekane umekamilika. Kabla hujajifikiria wewe na ubinafsi wako mfikirie yule mwanaume aliekuona wewe ni mwanamke sahihi kwake na ni mwanamke anayetaka atumie maisha yake yaliyobaki duniani na wewe.

Usiolewe kumridhisha mtu au kukomesha wale waliosena hutaolewa. Maisha ni matamu ukiwa kwenye ndoa sahihi (sijaolewa ila najua utamu wa mapenzi).

Ewe mwanamke usitoke kwenye ndoa kwa upumbavu wako. Achika kwa kushindwa kumvumilia mume ila sio kwa kushindwa kuigiza upendo ambao haukuwepo toka siku unasema I DO.
 
Hivi unaoa/olewa kisa shinikizo la ndugu kweli?

Hiyo ndoa utaitumikia wewe ua hao ndugu!? Waafrica sisi bwana tuna mambo ya kupangiana maisha kiduanzi sana.
 
Asante kwa kutukumbusha,i will work on it
 
Hakushinikwa hata eti. Mama ake alimwambia nataka nione ndoa yako kabla hujafikisha miaka 30. Alivyotokea muoaji akakubali afulfill ndoto ya mama ake.

Kingine alikua anataka harusi flani hivi ya heshima na nini.
Hivi unaoa/olewa kisa shinikizo la ndugu kweli?

Hiyo ndoa utaitumikia wewe ua hao ndugu!? Waafrica sisi bwana tuna mambo ya kupangiana maisha kiduanzi sana.
 
Nenda kamwambie bhana MI napendaga kwa bahati pia Kama ngamia nimezoea jangwani.....am sad
 
Huyu mwanajeshi sijui kama hatajiua wallah. Maana anamuona huyu mwanamke kama mboni yake. Angejuaaaaa
Kawaida yenuu Mnaolewa sababu mko desparate na ndoa..! Mwisho wa siku mnabeba mimba za wanaume wengne mnaowapenda mumeo akijua anauaa wote kama ana moyo mdogoo..
 
Hakushinikwa hata eti. Mama ake alimwambia nataka nione ndoa yako kabla hujafikisha miaka 30. Alivyotokea muoaji akakubali afulfill ndoto ya mama ake.

Kingine alikua anataka harusi flani hivi ya heshima na nini.
Kuna watu wengine wana asili ya ubinafsi sana. Mzazi huwezi kumpangia mwanao masuala kama ndoa ambayo ni mambo mazito. Mimi mzazi akitaka anilazimishe nioe labda anipe billion ile Mo Dewji hapo anipe na mke anaetaka yeye nimuoe.

La sivyo ndio hapo kutaka ku fulfill dream ya mtu ambaye yeye hiyo ndoa wala hajui inaenda kuwa vipi. Mwisho wa siku ni lawama mateso na chuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…