Kete Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 6,656
- 6,886
Sababu sio mama ni ukicheche tu wa mtu basi.Wakati mama ake ataumia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sababu sio mama ni ukicheche tu wa mtu basi.Wakati mama ake ataumia
Sijaanza mwaya ila kuna watu wenye tabia hizo wanaona kila mtu yupo hivyoUmeanza lini umalaya?!!?
You wrote kile nilichokuwa nawazaAkiua x atakuja mwingine bibie atakaempenda. Nimemshauri ahamie mkoa anakofanyia kazi mumeww wakaishi nae la sivyo itachukua muda huyu mwanamke kumpenda mjeda
Naomba kudeclare interest kabla sijaenda mbali: Mimi ni muumini wa mapenzi. Naamini katika ndoa yenye mapenzi na sio sababu nyingine.
Nina rafiki yangu aliolewa siku kadhaa nyuma. Siku ya kuvalishwa pete nilienda nae ukweni kwao. Lakini hakuwa na furaha kabisa. Mpaka mawifi wanatuambia muambieni mwenzenu asmile basi hata kwenye picha tu.
Baada tukio wakati tunarudi nikamwambia huna furaha umelazimishwa kuolewa? Kama unaona humtaki huyu kaka una nafasi bado hii ni pete tu muache kuliko uje kumuumiza baadae. Akaniambia nitakujibu kesho. Kesho yake nikamuuliza tena umeamua kuolewa au kukatisha ndoa. Akaniambia naolewa ile jana nilikua excited. Lakini picha zake kila mtu alikua anasema hana furaha.
Akaja akaolewa. Lakini hana furaha kabisa. Jana akaanza kuniambia habari za talaka. Ndoa hata miezi mitatu haina. Nikamuuliza unakumbuka niilivyokuambia ukatishe kuolewa wakati umevalishwa pete? Kwanini unataka umuumize mumeo na anakupenda sana. Akanijibu tu aliolewa kwa sababu alikua na stress na alitaka kumridhisha mama yake ila hajioni kabisa kumpenda mumewe. Nikamwambia sasa utafanyaje. Akasema hajui ila anaona hayuko sehemu sahihi na haenjoy ndoa yake. Nilichomshauri nikamwambia fuata moyo wako ila kuachika ni aibu zaidi tena kwa tamaa zako wakati ulikuwa na nafasi ya kukataa ndoa toka mwanzo.
Namuonea sana huruma mume wake maana anampenda sana mkewe ila mke hampendi kiasi cha kutotaka kuzaa na mumewe. Ameolewa lakini bado ana mapenzi mazito kwa ex bf wake. Na anavyoongea ni kama anataka amzalie kabisa huyu ex wake wakati yeye mke wa mtu. Siku mumewe akija kujua kilicho ndani ya mke wake kama sio kumuua bas atamuua yeye maana wajeda mapenzi yanajuaga kuwaumiza kweli kweli.
Kwa wenzangu, sio lazima uolewe ndo uonekane umekamilika. Kabla hujajifikiria wewe na ubinafsi wako mfikirie yule mwanaume aliekuona wewe ni mwanamke sahihi kwake na ni mwanamke anayetaka atumie maisha yake yaliyobaki duniani na wewe.
Usiolewe kumridhisha mtu au kukomesha wale waliosena hutaolewa. Maisha ni matamu ukiwa kwenye ndoa sahihi (sijaolewa ila najua utamu wa mapenzi).
Ewe mwanamke usitoke kwenye ndoa kwa upumbavu wako. Achika kwa kushindwa kumvumilia mume ila sio kwa kushindwa kuigiza upendo ambao haukuwepo toka siku unasema I DO.