Kabla hujakubali kuolewa wakati humpendi mwanaume muwazie yule mwanaume anaekuoa kwa sababu anakupenda.

Kabla hujakubali kuolewa wakati humpendi mwanaume muwazie yule mwanaume anaekuoa kwa sababu anakupenda.

Write your reply...hivi bado watu wanaoa na kuolewa siku hizi .anyway npo hapa kuwakilisha chama cha mabachelor
 
makosa mawili makubwa mnayofanya wanawake wa siku hizi kuingia ktk ndoa:-
1. kuridhisha wazazi hasa wakina mama ndio wanaongoza ktk hili kuwapelekea watoto zao kutofaidi maisha ya ndoa....unakuta mdada wa watu anaolewa hata na mtu asiyependa ndo hapo habari za michepuko huanza hii mbaya sana.

2. kuwatambia wenzake mtaani kwamba fulani kaolewa....yes kuolewa ni heshima ila kwa ndoa za namna hizi hakuna maana halisi ya ndoa hapo.

muhimu kusikiliza moyo wako unataka nini, hakuna kitu kizuri katika maisha haya kama amani.
 
Sijafikia huko mkuu kuliwa na shemeji yangu. Siwezi kuwaachanisha kwanza wataachana wenyewe tu yakiwafika hapa.
Kumsaidia shogaako,jitongozeshe kwa mumewe akubabue afu awafumanie apate sababu!



Vere simpo!
 
Sasa taahira kama huyo unamshauri wa nini si umuache tu akachukue namba yake ya masingle mother fala wahed huyo......

Siku hizi mabinti akili zao wanazielewa wenyewe,
 
Naomba kudeclare interest kabla sijaenda mbali: Mimi ni muumini wa mapenzi. Naamini katika ndoa yenye mapenzi na sio sababu nyingine.

Nina rafiki yangu aliolewa siku kadhaa nyuma. Siku ya kuvalishwa pete nilienda nae ukweni kwao. Lakini hakuwa na furaha kabisa. Mpaka mawifi wanatuambia muambieni mwenzenu asmile basi hata kwenye picha tu.

Baada tukio wakati tunarudi nikamwambia huna furaha umelazimishwa kuolewa? Kama unaona humtaki huyu kaka una nafasi bado hii ni pete tu muache kuliko uje kumuumiza baadae. Akaniambia nitakujibu kesho. Kesho yake nikamuuliza tena umeamua kuolewa au kukatisha ndoa. Akaniambia naolewa ile jana nilikua excited. Lakini picha zake kila mtu alikua anasema hana furaha.

Akaja akaolewa. Lakini hana furaha kabisa. Jana akaanza kuniambia habari za talaka. Ndoa hata miezi mitatu haina. Nikamuuliza unakumbuka niilivyokuambia ukatishe kuolewa wakati umevalishwa pete? Kwanini unataka umuumize mumeo na anakupenda sana. Akanijibu tu aliolewa kwa sababu alikua na stress na alitaka kumridhisha mama yake ila hajioni kabisa kumpenda mumewe. Nikamwambia sasa utafanyaje. Akasema hajui ila anaona hayuko sehemu sahihi na haenjoy ndoa yake. Nilichomshauri nikamwambia fuata moyo wako ila kuachika ni aibu zaidi tena kwa tamaa zako wakati ulikuwa na nafasi ya kukataa ndoa toka mwanzo.

Namuonea sana huruma mume wake maana anampenda sana mkewe ila mke hampendi kiasi cha kutotaka kuzaa na mumewe. Ameolewa lakini bado ana mapenzi mazito kwa ex bf wake. Na anavyoongea ni kama anataka amzalie kabisa huyu ex wake wakati yeye mke wa mtu. Siku mumewe akija kujua kilicho ndani ya mke wake kama sio kumuua bas atamuua yeye maana wajeda mapenzi yanajuaga kuwaumiza kweli kweli.

Kwa wenzangu, sio lazima uolewe ndo uonekane umekamilika. Kabla hujajifikiria wewe na ubinafsi wako mfikirie yule mwanaume aliekuona wewe ni mwanamke sahihi kwake na ni mwanamke anayetaka atumie maisha yake yaliyobaki duniani na wewe.

Usiolewe kumridhisha mtu au kukomesha wale waliosena hutaolewa. Maisha ni matamu ukiwa kwenye ndoa sahihi (sijaolewa ila najua utamu wa mapenzi).

Ewe mwanamke usitoke kwenye ndoa kwa upumbavu wako. Achika kwa kushindwa kumvumilia mume ila sio kwa kushindwa kuigiza upendo ambao haukuwepo toka siku unasema I DO.

Love is overrate honey!

Dont be fooled!

It is unfortunate women always fail on LOVE....It is unfortunate!
 
Duh yan mambo ya wanawake[emoji58][emoji58]
 
Back
Top Bottom