Kabla hujamdhamini mtu, hakuna tofauti kati ya mdhamini na mkopaji deni linaposhindwa kulipwa

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
96
Reaction score
1,745
BENKI KUUZA MALI YA MDHAMINI.

Bashir Yakub, WAKILI
+255714047241

Tarehe 1/4/2023 Mahakama ya rufaa imesisitiza kuwa unapomdhamini mtu kwa kuweka mali yako rehani ili uliyemdhamini achukue mkopo basi unatakiwa kujua kuwa hatia yako na huyo uliyemdhamini ni sawa pale anaposhindwa kulipa mkopo.

Mahakama imesema hivyo wakati ikitafsiri kifungu cha 78 cha Sheria ya Mikataba katika Rufaa Na.376/2019 kati ya Partrick Edward Mushi vs Commercial Bank of Africa.

Kwa hiyo wanaodhamini wanatakiwa kujua kuwa kudhamini ni sawa na kukopa. Wewe uliyedhamini na huyo uliyemdhamini akachukua hela nyote ni sawa likitokea la kutokea.

Usije kutegemea kuwa utasema mimi ni mdhamini tu, laa hasha, nyote ni sawa.

Na mahakama inasisitiza kuwa endapo uliyemdhamini atashindwa kulipa mkopo basi yafaa mali yako iuzwe mara moja, huu ndio msimamo.

Kwa msimamo huu ni muhimu sana kabla hujamdhamini mtu kujiridhisha na kila kitu ikiwemo uwezo wake wa kulipa, biashara zake, uaminifu wake,utu na mahusiano yenu nk.

Katika mambo ambayo hutakiwi kukurupuka ni hili. Tunajua wadhamini nao hupewa fungu mkopo ukitoka, lakini yawezekana hilo fungu ndiyo pesa ya mauzo ya mali yako.

Nirudie tena kuwa hakuna tofauti kati ya mdhamini na mkopaji deni linaposhindwa kulipwa.
 
Ukikopa bank,ukashindwa kulipa ni shida.Japo kuna wachagga waliosoma CUBA wanajua jinsi ya kusolve hii issue.Ila hii ya kausha damu na chupi mkononi natoka na rungu tu hambebi hata vumbi!Maana hawa wake zetu wanakopa bila kutuambia wakianza kudaiwa wanahamishia zengwe nyumbani
 
BENKI KUUZA MALI YA MDHAMINI.

Bashir Yakub, WAKILI
+255714047241

Tarehe 1/4/2023 Mahakama ya rufaa imesisitiza kuwa unapomdhamini mtu kwa kuweka mali yako rehani ili uliyemdhamini achukue mkopo basi unatakiwa kujua kuwa hatia yako na huyo uliyemdhamini ni sawa pale anaposhindwa kulipa mkopo.

Mahakama imesema hivyo wakati ikitafsiri kifungu cha 78 cha Sheria ya Mikataba katika Rufaa Na.376/2019 kati ya Partrick Edward Mushi vs Commercial Bank of Africa.

Kwa hiyo wanaodhamini wanatakiwa kujua kuwa kudhamini ni sawa na kukopa. Wewe uliyedhamini na huyo uliyemdhamini akachukua hela nyote ni sawa likitokea la kutokea.

Usije kutegemea kuwa utasema mimi ni mdhamini tu, laa hasha, nyote ni sawa.

Na mahakama inasisitiza kuwa endapo uliyemdhamini atashindwa kulipa mkopo basi yafaa mali yako iuzwe mara moja, huu ndio msimamo.

Kwa msimamo huu ni muhimu sana kabla hujamdhamini mtu kujiridhisha na kila kitu ikiwemo uwezo wake wa kulipa, biashara zake, uaminifu wake,utu na mahusiano yenu nk.

Katika mambo ambayo hutakiwi kukurupuka ni hili. Tunajua wadhamini nao hupewa fungu mkopo ukitoka, lakini yawezekana hilo fungu ndiyo pesa ya mauzo ya mali yako.

Nirudie tena kuwa hakuna tofauti kati ya mdhamini na mkopaji deni linaposhindwa kulipwa.
Je kama umedhaminiwa na office,alafu ukapunguzwa kazini na ukawa huna tena uwezo wa kufanya marejesho, Je Bank wataidai office yako ya zamani!!?
 
Kwa hiyo wanaodhamini wanatakiwa kujua kuwa kudhamini ni sawa na kukopa. Wewe uliyedhamini na huyo uliyemdhamini akachukua hela nyote ni sawa likitokea la kutokea.
Inategemea na sharti la udhamini mfano namdhamini mtu anachukuwa mkopo akishindwa kulipa zitauzwa mali zake pindipo hazijafidia ndio huja kuuzwa mali zangu ili kufikia kiwango cha mkopo. Lakini pia naweza kuendeleza malipo pindipo kama atashindwa basi ipo nafasi kwa makubaliano ya mkataba mpya baina ya mdai na mdhamini.
 
Back
Top Bottom