Swali lako ni fair. Kama unamaanisha “taja idea ambayo hakuna binadamu yeyote kabla ya Yesu aliyewahi kusema hata kwa namna inayofanana”, basi sitadai kwamba ninaweza kuthibitisha hilo.
Lakini hilo halimaanishi Yesu hakuleta idea au framework yenye distinctive impact.
Mfano mmoja mkubwa ni kuweka upendo wa Mungu na upendo wa jirani—hata adui—katika kiini cha maisha ya kiroho na maadili. Yesu anasema:
“Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.”
Hiyo si sawa na kusema hakuna mtu kabla yake aliyewahi kusema “usiwe na chuki.” Hoja ni kwamba Yesu aliichukua na kuiweka ndani ya mfumo wake wa mafundisho kwa namna yenye nguvu sana: si kumpenda tu anayekupenda, bali kumpenda adui na kumtendea mema anayekudhuru.
Na kuna tofauti kati ya “Yesu alikuwa wa kwanza kabisa kusema sentence hii duniani” na “Yesu alitoa/aliendeleza mfumo wa mawazo ambao ukawa na impact kubwa sana.”
Kama challenge yako ni kwamba “show me one idea ambayo ni 100% non-derivative”, basi hilo ni standard ambayo ni ngumu sana kuitumia kwa mtu yeyote wa historia. Karibu kila mwanafalsafa, mwanasayansi au mwalimu mkubwa alijenga juu ya mawazo yaliyokuwepo kabla yake.
Kwa hiyo mimi sikusema Yesu alitengeneza kila idea kutoka zero. Nilichosema ni kwamba aliweza kuwasilisha mafundisho yaliyokuwa na nguvu kiasi cha kubadili historia ya dunia.
Na hapo ndipo swali langu la mwanzo lilipo: unaweza kuamini Yesu alikuwa wrong, unaweza kumcriticize, lakini bado ukatambua ukubwa wa impact yake.
Impact ≠ proof kwamba alikuwa sahihi. Lakini pia disagreement ≠ sababu ya kumdhihaki.
Kama ulivyosema, there is nothing original there.
Na usimkataze mtu kukataa ukubwa wa impact ya Yesu mpaka umsikilize kwanza.
Kina Waingereza walikuwa wanamuona Sir Winston Churchill kuwa ni shujaa wao mkubwa sana, kwa sababu alitetea Ufalme wao. Lakini waliotawaliwa na waingereza wengi, hususan Wahindi, walimuona Churchill kama mkandamizaji mkubwa aliyewatesa.
Sasa, mtu anayesema usimdhihaki Churchill kwa sababu alifanya mambo makubwa duniani, katetea ufalme mkubwa sana, kuna watu wameumizwa na ufalme huo, hao wanahaki ya kuudhihaki ufalme huo kwa kusema ufalme mkubwa gani mbona umekosa haki nanumetuonea tu?
Na Yeu naye ni hivuo hivyo. Kuna watu wameumizwa na messages zake, ukiwaambia Yesu kafanya makubwa watakwambia makubwa gani mbona yametuumiza tu, bira hata asingekuwapo tusingeumizwa.
Kwa hivyo hawa wakiamua kumdhihaki Yesu, ni haki yao. Usiwakataze.
Kuwakataza hivyo ni censorship. Ni kumnyima mtu uhuru wake wa kujieleza.
Msikilize kwanza, halafu kama unaweza kumpinga kwa hoja, ndiyo umpinge.
Dunia inaenda ikiongeza elimu na the zeitgeist inaenda na kuongeza moral standard.
Watu walionekana superheroes miaka ya nyuma kwanza wanaonekana mapungufu yao, na pengine watu wanaweza hata kuhoji kama walifanya net positive at all.
Huyo Yesu mwenyewe mnamuongelea kwa stories za kuungaunga zenye natobo kibao, mpaka hapo habari nzima inakuwa na matobo yanayoifanya ihojike na kudhihakika sana kama mtu anatafuta kuijua kihistoria.
Acha huu uwe mjadala wa wazi, watu wawe huru kusema, wawe huru hata kumdhihaki Yesu, uwasikilize kwa muktadha mpana, kisha uamue kuwa huyu alidhihaki kama comedy tu hapa sitamchukulia serious, huyu hapa alidhihaki kwa falsafa lakini hoja yake ina mapungifu haya na haya, huyu hapa alimdhihaki lakini kuna ukweli mkubwa ambao hatukuufikiria.
Yani watu wangekuwa na msimamo kama wako hata huyo Yesu asingeweza kusema ukamjua.
Kwa sababu na yeye kuna wakati alionekana kama anamdhihaki Musa na mambo ya Uyahudi yaliyo rigid kwenye sheria.
Kwa hivyo, kwa kukataa Yesu asidhihakiwe, unaweza kukataa a new paradigm shift of moral consciousness of this time that is equal to what Jesus did to Judaism.
Wewe unachoona dhihaka, mwingine anaona funzo la kifalsafa. Sasa utakataaje dhihaka na kutenganisha kukataa dhihaka na mafunzo ya kifalsafa kwwnye mambo subjective hivi?
Dhihaka ni sehemu ya uhuru wa kujieleza. Jamii zote zinazothamini uhuru zinatakiwa kuthamini uhuru wa watu kufanya dhihaka, bila kujali wana uwezo gani na wamechangia nini.
Yesu mwenyewe alipofanyiwa dhihaka kubwa ya kusulubuwa huju askari wa Kiruni wakifanya kamari kugawana mavazi yaje, aliikabiki dhihaka ike kwa kusema wasamehe baba, kwa maana hawajui watendalo.
Sasa wewe kama unamthamini sana Yesu, kwa nini na wewe usiwasamehe tu hao wafanya dhihaka kama watu wasiojua watendalo?
Kama dhihaka imekaa vibaya, na wewe una uhuru wa kuikosoa hiyo dhihaka, lakini, kwenye jamii huru, huna uhuru wa kuikataza dhihaka.