Unalazinisha impact iwe kubwa.Nimekusoma vizuri, na hapa nakubaliana na wewe kwenye jambo moja muhimu: mtu ana uhuru wa kumdhihaki Yesu, kama ambavyo ana uhuru wa kumkosoa. Sikupaswa kutumia lugha inayoweza kueleweka kama ninataka kumzuia mtu kufanya hivyo.
Lakini bado kuna sehemu moja ya hoja yangu ambayo sidhani kama umeibatilisha.
Niliposema βkabla hujamdhihaki mtu ambaye ameacha impact kubwa, tambua kwanza ukubwa wa impact yakeβ, sikumaanisha βusimdhihaki kwa sababu hujafanya makubwa.β Hiyo ingekuwa fallacy kama ulivyosema.
Nilimaanisha: usichanganye ukubwa wa impact na ukweli wa mafundisho.
Churchill anaweza kuwa shujaa kwa Waingereza na villain kwa baadhi ya waliotawaliwa na Uingereza. Hiyo haifanyi impact yake kutoweka. Vivyo hivyo, mtu anaweza kumwona Yesu kama mwalimu mkubwa wa maadili, mwingine akamwona kama chanzo cha baadhi ya matatizo, na mwingine akaamini kabisa kwamba alikuwa Mungu. Hizo ni interpretations tofauti za mtu yuleyule.
Na hapo ndipo nadhani tunakubaliana zaidi kuliko tunavyotofautiana:
Mtu akimdhihaki Yesu, msikilize kwanza.
Kama ni comedy tu, ni comedy.
Kama ni criticism ya kihistoria, ijadiliwe kihistoria.
Kama ni philosophical criticism, ijibiwe kifalsafa.
Na kama ndani ya dhihaka kuna criticism yenye ukweli, basi tusiogope kuukubali.
Lakini upande mwingine nao uwepo: uhuru wa kusema hauondoi uhuru wa wengine kusema βhoja yako ni dhaifu.β
Kwa hiyo sitaki censorship ya dhihaka. Nataka mjadala ambao hata dhihaka yenyewe inaweza kuhojiwa.
Na kuhusu mfano wako wa Yesu kusamehe waliomsulubisha, huo ni mfano mzuri. Labda tofauti yetu ni kwamba mimi nilikuwa nashauri watu waheshimu uzito wa historia wanayoijadili, wewe unasema kwanza waache watu waseme bila kuzuiwa, kisha hoja ipimwe.
Kwa hilo la pili, nakubaliana.
Uhuru wa kumdhihaki Yesu uwepo. Uhuru wa kumjibu anayemdhihaki Yesu pia uwepo. Mwisho wa siku, hoja ndiyo ipimweβnot mtu anayeisema.
Exactly,Nimekupata. Kwa argument hii, nakubaliana na wewe kwamba hakuna qualification ya lazima ya mtu kumdhihaki au kumkosoa mwingine. Mtu hahitaji kuwa na kitabu chake ili ku-criticize kitabu cha mwingine, wala hahitaji kuwa na nyumba kubwa ili kukosoa architecture ya nyumba ya tajiri.
Na hapo nakubali kwamba hoja yangu ya awali ya βkabla hujamdhihaki jiulize umefanya niniβ inaweza kueleweka vibaya, kwa sababu inaweza kuonekana kama namwekea mtu condition ya kuwa na achievement fulani kabla hajawa na haki ya kukosoa. Hiyo si standard nzuri.
Lakini kuna kitu bado ningependa kitenganishwe:
Kuwa na haki ya kusema kitu β kuwa kitu unachosema ni sahihi.
Mtu ana haki kabisa kusema Yesu alikuwa mjinga, Muhammad alikuwa mjinga, Churchill alikuwa mhalifu, au hata kwamba dini zote ni upuuzi. Hakuna achievement inayomnyangβanya mtu hiyo nafasi ya kusema.
Lakini mimi pia nina haki ya kumuuliza:
βHoja yako dhidi yake ni ipi?β
Na hapo ndipo mjadala unaanza.
Kwa hiyo sasa ningerekebisha kabisa kauli yangu ya mwanzo:
Sisemii mtu βusimdhihaki Yesu kwa sababu hujafanya makubwa.β
Nasema βukimdhihaki Yesu, usidhani dhihaka yenyewe imemaliza mjadala; tuchambue pia sababu na hoja iliyoko nyuma yake.β
Na point yako ya mwisho kuhusu comedy nimeipenda, kwa sababu inaonyesha vizuri kwamba dhihaka yenyewe inaweza kuwa criticism na hata kuwa na social value, hata kama anayefanya hiyo criticism hajawahi kufanya jambo kubwa kuliko anayemkosoa.
Kwa hiyo labda tumefika kwenye sehemu ambayo tunakubaliana:
Mtu yeyote anaweza kumdhihaki Yesu. Mtu yeyote anaweza kumtetea Yesu. Mtu yeyote anaweza kuikosoa hiyo dhihaka. Na mwisho wa siku, si ukubwa wa mtu unaoamua ukweli wa hojaβni hoja yenyewe.
Hapo nadhani mjadala unakuwa interesting zaidi kuliko kubishana nani ana βimpactβ kubwa.
Maisha ya binadamu yalianza miaka mingi sana.Sasa Yesu kaanzisha wazo gani?
Name a singular, distinct, non-derivative, original idea started by Jesus.
logical fallacy, non sequitur logical fallacy.Hoja yako kuu ni logical fallacy, non sequitur logical fallacy.
Mtu ambaye hachezi mpira, hana nia ya kucheza mpira, anaweza kuwadhihaki wacheza mpira, bila ya yeye kuweza kucheza mpira, that is the point. Anaona mpira hauna maana.
Mtu anaweza kuwadhihaki watu wanaotaka kuibadili dunia kwa dini bila ya yeye mwenyewe kuleta chochote kwako wewe, pengine akikataa kifalsafa kuleta chochote cha maana kwako, na kusimamia hoja kwamba hao wanaotaka kuibadili dunia wanaiharibu.
Na kiukweli organized religion zimeharibu mengi tu.
Na pia, mambo mengi unaweza kuyasema ni mafanikio ya mtu, wakati kiukweli mengine yanatokana na bahati na ajali za kihistoria tu, kwa hiyo unaweza kumpa credit sana Yesu, lakini ukagundua kuwa bila ya Mfalme Constantin kuukubali Ukristo na kuufanya kuwa dini ya Ufalme, Ukristo usingefanikiwa hivyo.
Sasa unawezaje kukinganisha watu wanaoishi keo zama za ibtwrnet na watu kama Yesu walioishi zama za ujinga?
Huelewi vipi kwamba Yesu labda alikuwa na bahati ya kuzaliwa zama za ujinga tu, angekuwa anaanzisha habari zake leo angeandamwa na wanamazingira na wapenda wanyama kama wa People for the Ethical Treatment of Animals, kwa kuyaruhusu majini yawaingie nguruwe walioishia kuzama ziwani?
Kwa hiyo, ukielewa historia hiyo, ukamsoma si Yesu tu, bali pia ukasoma ukosoaji aliofanyiwa Yesu katika insha ya Bertrand Russell ya "Why I am Not A Christian", unaweza kuona Yesu ana mengi ya kukejeliwa, hata na watu waliomsoma Bertrand Russell tu na kumuelewa, hata ambao hawajafanya mengi.
Tatizo umemsoma Lord Russell?
Au umeishia kwa Lord Jesus tu?
Kwanza hatupo mwaka 2026. Labda huelewi kuwa kuna kalenda nyingi duniani.Maisha ya binadamu yalianza miaka mingi sana.
Maswali
1. Kwanini tupo mwaka 2026?
2. Ni nani alitoa wazo kuwa tubadilishe mwaka na kwasababu gani?
3. Kwanini kwenye maandiko mengi tunatumia BC na AD?
4. Maana ya BC na AD ni nini?
5. Wewe hapo umetoa wazo gani ambalo limebadilisha dunia?
Mkuu, bora umeuliza. Umewashinda watu wengi wanaobishia vitu ambavyo hawajavielewi na hawataki kuuliza, wanaogopa kuonekana hawajui, wanabisha tu.logical fallacy, non sequitur logical fallacy.
Huwa unamaanisha nini mkuu Kiranga
Sasa wewe ambao upo sahihi. Jibu haya maswaliKwanza hatupo mwaka 2026. Labda huelewi kuwa kuna kalenda nyingi duniani.
Hiyo ni namna moja tu ya kuhesabu miaka. Waislamu wana namna yao ya kuhesabu miaka yao.
Yesu hajaanzisha dhaha ya kuhesabu miaka.
Na hata hao waliokija kuanza kuhesabu miaka kuanzia alipizaliwa Yesu walikuwa watu wengine, si Yesu.
Na hata hao wamekosea miaka.
.
Maswali binafsi si muhimu kwa sababu mimi si hoja, hapa kuna hoja kubwa zaidi yangu ambayo ingeweza kuwapo tu hata kama mimi nisingezaliwa.Sasa wewe ambao upo sahihi. Jibu haya maswali
1. Una miaka mingapi?
2. Umezaliwa mwaka gani?
3. Umemaliza elimu yako ya shule ya msingi mwaka gani?
Nilijua hayo maswali machache huwezi kuyajibu na lazima uje na story.Maswali binafsi si muhimu kwa sababu mimi si hoja, hapa kuna hoja kubwa zaidi yangu ambayo ingeweza kuwapo tu hata kama mimi nisingezaliwa.
Tujadili hoja, tuache kujadili mtu.
Kujadili ntu badala ya hoja kunatupeleka kwenye logical fallacy nyingine nimeitaja hapo juu ya ad hominem fallacy.
Zaidi, hata nikitaka kujibu kidhahania naweza kukuambia sisi tuna miaka ya kuhesabu kwa kufuatana na Machifu wetu huko Usukumani, kuhesabu vonginevyo ni aona ya ukoloni wa utamaduni, au mimi Muislamu nahesabu miaka ya kutoka Hijra, au mimi ni ordained Buddhist monk nimepata mafunzo kwa Rev. Pannasekara Buddhist Temple nahesabu miaka kwa kalenda ka ki Buddha. Au nimelowea China huko nahesabu miaka Kichina.
Au nimeanzisha kalenda yangu inahesabu miaka tangu ilipoanza AI kwa ChatGPT November 30 2022.
Nimeziweka kalenda kadhaa hapo juu, ukifikiri kalenda za dunia zinaishia kwenye kalenda ya Kikristo tu, huo ni ufinyu wa mawazo.
Unatumia logical fallacy ya argument from popularity.Nilijua hayo maswali machache huwezi kuyajibu na lazima uje na story.
Unajua kuna Kalenda nyingi, kwanini haujatumia kalenda zingine kujibu hayo maswali? Aliyekudanganya kuwa hatupo mwaka 2026 na bado unatumia tarehe, mwezi na mwaka 2026 mwambie ni kichaaπππ
Nilijua utakuja na kalenda yako kumbe bado unafuata mitazamo ya kalenda ya watu wengine.
Nipo nafatilia hii battle yako na kirangaNilijua hayo maswali machache huwezi kuyajibu na lazima uje na story.
Unajua kuna Kalenda nyingi, kwanini haujatumia kalenda zingine kujibu hayo maswali? Aliyekudanganya kuwa hatupo mwaka 2026 na bado unatumia tarehe, mwezi na mwaka 2026 mwambie ni kichaaπππ
Nilijua utakuja na kalenda yako kumbe bado unafuata mitazamo ya kalenda ya watu wengine.
Je Kiranga na wewe unaamini kuwa yesu ni story ya kweli kuwa alikuwepo miaka hiyo.Kama ulivyosema, there is nothing original there.
Na usimkataze mtu kukataa ukubwa wa impact ya Yesu mpaka umsikilize kwanza.
Kina Waingereza walikuwa wanamuona Sir Winston Churchill kuwa ni shujaa wao mkubwa sana, kwa sababu alitetea Ufalme wao. Lakini waliotawaliwa na waingereza wengi, hususan Wahindi, walimuona Churchill kama mkandamizaji mkubwa aliyewatesa.
Sasa, mtu anayesema usimdhihaki Churchill kwa sababu alifanya mambo makubwa duniani, katetea ufalme mkubwa sana, kuna watu wameumizwa na ufalme huo, hao wanahaki ya kuudhihaki ufalme huo kwa kusema ufalme mkubwa gani mbona umekosa haki nanumetuonea tu?
Na Yeu naye ni hivuo hivyo. Kuna watu wameumizwa na messages zake, ukiwaambia Yesu kafanya makubwa watakwambia makubwa gani mbona yametuumiza tu, bira hata asingekuwapo tusingeumizwa.
Kwa hivyo hawa wakiamua kumdhihaki Yesu, ni haki yao. Usiwakataze.
Kuwakataza hivyo ni censorship. Ni kumnyima mtu uhuru wake wa kujieleza.
Msikilize kwanza, halafu kama unaweza kumpinga kwa hoja, ndiyo umpinge.
Dunia inaenda ikiongeza elimu na the zeitgeist inaenda na kuongeza moral standard.
Watu walionekana superheroes miaka ya nyuma kwanza wanaonekana mapungufu yao, na pengine watu wanaweza hata kuhoji kama walifanya net positive at all.
Huyo Yesu mwenyewe mnamuongelea kwa stories za kuungaunga zenye natobo kibao, mpaka hapo habari nzima inakuwa na matobo yanayoifanya ihojike na kudhihakika sana kama mtu anatafuta kuijua kihistoria.
Acha huu uwe mjadala wa wazi, watu wawe huru kusema, wawe huru hata kumdhihaki Yesu, uwasikilize kwa muktadha mpana, kisha uamue kuwa huyu alidhihaki kama comedy tu hapa sitamchukulia serious, huyu hapa alidhihaki kwa falsafa lakini hoja yake ina mapungifu haya na haya, huyu hapa alimdhihaki lakini kuna ukweli mkubwa ambao hatukuufikiria.
Yani watu wangekuwa na msimamo kama wako hata huyo Yesu asingeweza kusema ukamjua.
Kwa sababu na yeye kuna wakati alionekana kama anamdhihaki Musa na mambo ya Uyahudi yaliyo rigid kwenye sheria.
Kwa hivyo, kwa kukataa Yesu asidhihakiwe, unaweza kukataa a new paradigm shift of moral consciousness of this time that is equal to what Jesus did to Judaism.
Wewe unachoona dhihaka, mwingine anaona funzo la kifalsafa. Sasa utakataaje dhihaka na kutenganisha kukataa dhihaka na mafunzo ya kifalsafa kwwnye mambo subjective hivi?
Dhihaka ni sehemu ya uhuru wa kujieleza. Jamii zote zinazothamini uhuru zinatakiwa kuthamini uhuru wa watu kufanya dhihaka, bila kujali wana uwezo gani na wamechangia nini.
Yesu mwenyewe alipofanyiwa dhihaka kubwa ya kusulubuwa huju askari wa Kiruni wakifanya kamari kugawana mavazi yaje, aliikabiki dhihaka ike kwa kusema wasamehe baba, kwa maana hawajui watendalo.
Sasa wewe kama unamthamini sana Yesu, kwa nini na wewe usiwasamehe tu hao wafanya dhihaka kama watu wasiojua watendalo?
Kama dhihaka imekaa vibaya, na wewe una uhuru wa kuikosoa hiyo dhihaka, lakini, kwenye jamii huru, huna uhuru wa kuikataza dhihaka.
Mimi kuamini si muhimu sana, maana kuamini hata uongo unaruhusiwa kuamini, ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu.Je Kiranga na wewe unaamini kuwa yesu ni story ya kweli kuwa alikuwepo miaka hiyo.
Nimekupata nilitaka jua mtazamo wako kumhusu yesu umenena vyema mkuuMimi kuamini si muhimu sana, maana kuamini hata uongo unaruhusiwa kuamini, ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu.
Na kuamini hakuhojiki, kwa sababu ni haki ya mtu. Sasa mpaka hapo suala la kuamini linakosa uzito katika mazungumzo ya kutafuta facts.
Maana yake hata kama una maswali ya kunibana naweza kuchomoa yote kwa kusema hii ni imani yangu. In fact imani ya mtu hata kuijadili (unless kaileta hapa JF mwenyewe) mimi naona ni kumuingilia huyo mtu faragha yake ya kuamini anavyotaka.
Sasa tukitoka kwenye imani, tukienda kwenye historicity, somo la kupima kama kitu fulani kilikuwapo kweli katika historia, kilitokea kweli, au ni hekaya tu? Yesu aliishi, alirekodiwa hata nje ya Biblia, mimi nina mitabu kibao ya historia hapa kwangu, nimemsoma Josephus kamuandika Yesu nje ya Biblia (ingawa kuna controversy kuhusu back editing lakini alimuandika). Nimemsoma Tacitus, Tacitus ni muandishi mashuhuri aliyeandika kuhusu ufalme wa Warumi, nimemsoma sana, kamuandika Yesu nje ya Biblia.
Kwa hiyo kwamba kulikuwa na mtu anaitwa Yesu (Yeshua, Joshua whatever the nomeclature) aliyeishi muda huo, na kufundisha dini, na kupindua meza hekaluni etc na mambo mengi makubwa yaliyoandikwa, huyo inaonekana kuwa alikuwapo.
Warumi walikuwa na rwkodi nzuri sana, mpaka hao watu waliotajwa kuwapo wakati Yesu anaishi kina Pilato, na hizo stories za nuda wao, zipo kwenye historia. Kwa hiyo si kwamba Yesu hakuwapo watu wanwtunga tu atory. There are certain facts of historicity that check well with the secular record, not even the Biblical gospels.
Lakini kuna utata mwingi kuhusu mambo aliyoyafanya, miujiza, timeline, hata wasomi wa Biblia wanaona kuwa kuna utata mkubwa kwenye consistency ya the different gospels.
Halafu kuna masuala makubwa ambayo mimi sikubali kutokana na tofauti za kifalsafa, mfano kama siamini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, obviously ukisema Yesu ni mwana wa Mungu huyo, na yeye Yesu ni Mungu, sitakubali.
Kwa hiyo hapo unaanza kuona hata swali lako lenyewe inabidi lirudiwe upya kupata jibu la maana.
Unaposema Yesu una maana gani? Una maana mwana wa Mungu Masiha au mwana wa Mariam aliyefundisha dini takriban miaka 2,000 iliyopita?
Huyo wa kwanza (mwana wa Mungu) sikubali kuwa alikuwapo, ila huyu wa pili (mwana wa Maria) sioni tatizo kukubali alikuwapo.
Let us put it this way, mimi sipo katika wale watu wanaosema kuwa Yesu hajawahi kuishi ni hadithi ya kutungwa tu, lakini pia sipo katika wale wanaosema Yesu ni mwana wa Mungu aliyewahi kuishi na kufanya miujiza.
Naona Yesu alikuwa mtu tu, mwalimu wa dini aliyewahi kuishi, ila habari zake zimewekewa uongo mwingi sana kumfanya awe Mungu ili kueneza dini.
Punguza porojo kijana.ππππ Unasema hatupo mwaka 2026 halafu hapo hapo unaamini kalenda za watu wengine.Unatumia logical fallacy ya argument from popularity.
Watu wengi kukubali kitu haina maana hicho kitu ni cha kweli zaidi, au valid zaidi. Mara nyingine mambo yanakubalika kwa bahati, kwa utamaduni tu, kwa kulazimishwa vibaya na ukoloni, na vita.
Sasa, mtu anayeangalia ubora wa hoja ukimwambia mfumo wa kalenda ya Kikristo ni mzuri zaidi kwa sababu unakubaliwa sehemu nyingi, wakati mfumo huo umeharibu tamaduni nyingi za watu, umetetea utumwa, umeenea kwa vita na ukoloni, atakuona umeshindwa kuangalia vitu kwa kina unavutiwa na vitu superficial kama wingi wa watu leo tu bila kuangalia kalenda imeenea vipi.
Na hata kwenye wingi wa watu.
Kuna wakati watu wengi walikuwa wanaamini jua linaizunguka dunia, lakini wingi wao haukufanya hoja hiyo iwe kweli.
Hoja nzima ya kumtukuza Yesu imejengwa kwenye logical fallacies kama argument from popularity na non sequitur logical fallacy.
Ndiyo maana nimekwambia nipe idea moja original aliyoianzisha Yesu, umeshindwa kutaja umekuja na kitu shallow kama mfumo wa kuhesabu miaka, ambao hata hajauanzisha Yesu.
Wameanzisha wanasiasa tu baada ya Yesu kufariki.
Tatizo usipozijua hizi logical fallacies unaweza kujiona unajenga hoja yenye logic, kumbe unajenga logical fallacy.
Yesu hajaanzisha kalenda mkuu.Punguza porojo kijana.ππππ Unasema hatupo mwaka 2026 halafu hapo hapo unaamini kalenda za watu wengine.
Walioweka kalenda wako sahihi wote haijalishi ni kalenda gani kwasababu miaka ya dunia ilianza miaka mingi sana kwahiyo ukisema hatupo mwaka 2026 hata hizo kalenda zingine hazipo sawa. Hizo kalenda zote zimeanzia kwenye matukio kwahiyo zipo sawa
Nakuuliza tena haya maswali. Umesema hatupo mwaka 2026.
1. Una umri wa miaka mingapi?
2. Umezaliwa mwaka gani?
3. Umemaliza kidato cha nne mwaka gani?
4. Kwa akili yako tupo mwaka gani?
Hayo maswali manne kwa mtu wa porojo hawezi kujibu zaidi ya kuandika maelezo marefu ya somo la History
Ndio utakuta watu wanadhihaki wanatoa maneno yasio na staha wakati wao hawajawah leta impact yyte kwenye jamii