KABLA HUJAMUOA SINGLE MOTHER JITAHIDI MJUE ALIYEZAA NAYE. KAMA AMEKUZIDI KIPATO SITISHA MAHUSIANO HARAKA. SABABU NI HIZI;
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
1. Kwa Sisi Watibeli Tunaoa wanawake ambao wako Proudly kuwa na Sisi. Yaani wakiwa kwao jina letu linavuma, wanatutaja kwa mazuri, wanatusifu, wakiwa na Rafiki zake haoni haya kukutaja.
Hiyo ni moja ya sign za mwanamke anayekupenda au ambaye anajivunia kuwa na wewe.
2. Mwanamke anaweza akawa hakupendi lakini akawa proudly na wewe kutokana na status yako. Labda unapesa, labda unacheo kikubwa, labda maarufu, labda unakipaji kikubwa.
3. Wanawake hawapendi fedheha, hawapendi aibu za rejareja. Ndio maana wadada wengine ukiwasimamisha njiani wakikuona hueleweki wanaweza hata kutapika, kujihisi unawashushia nyota, unawatia mikosi.
4. Ndio maana Kila Siku nawaambia wanaume lazima ujipambanie, ujijengee value, uwe smart, uwe na kipato, uwe na mwili mkakamavu wa mazoezi. Upendeze.
Na sio kwaajili ya wanawake bali kwaajili yako mwenyewe. Heshima, hadhi, standards, thamani.
5. Wanawake kiasili wanadharau. Hilo lipo hivyohivyo. Ndio maana Kila Siku mwanaume unatakiwa uwe mguu sawa. Uwekeze kwako zaidi, uwe mbinafsi. Kwa sababu watajali matokeo zaidi kuliko mchakato. Mshindi ndiye atazingatiwa.
6. Sisi Watibeli tunaoa wanawake wakiwa katika uanawali wao. Hatusemi wengine wawe kama sisi. Au sisi tuwe kama wao.
7. Kwa wale walioamua kuoa single MOTHER. Hakikisha Unamfahamu Mwanaume aliyezaa na mwanamke unayetaka kumuoa. Umjue Kwanza.
8. Kama amekuzidi kipato au anasifa Fulani ya maana. My friend mwanamke ambaye unamuita mkeo atakuwa proudly na Mzazi mwenzake kuliko wewe
9. Akiwa na ndugu na Rafiki zake, utasikia huyu Babaake ni Mkurugunze wa Kampuni ya Usafirishaji wa Bahraini, mara huyu anaakili kama Babaake ambaye ni Profesa pale SUA. Wakati huo wewe uliyemuoa huna lolote.
10. Utasikia Babaake ni Mkuu wa idara pale Uhamiaji au Takukuru, au Utasikia Babaake ni Dokta pale hospitali ya Rufaa.
Kwa wanawake kwao hiyo ni heshima. Bila kujali wamegombana au hawajagombana, iwe anahudumia au ahudumii.
11. Sasa wewe ni mbangaizaji, mvujajasho, mlia na mbingu, muombamungu, Muoga chumvi ya Mawe.
Unafikiri mkeo atakuheshimu kuliko mwanaume wake wa kwanza aliyemzalisha aliyebora kuliko wewe.
12. Hata kama amemuacha ukamuoa wewe hiyo haimfanyi huyo mwanamke akakuweka level moja na huyo mwanaume wake wa wali.
13. Uliwahi kuona Mwanamke amezaa na wanaume watatu tofauti lakini Kila akiongea kuhusu baba wa watoto wake atakuwa anamtaja Yule mwanaume aliyefanikiwa. Unajua ni kwa nini?
14. Kwa sababu Wanawake wanataka wanaume washindi. Na ushindi wa wanawake sio wewe kumuoa. Ushindi wa wanawake ni kumuona mwanaume mwenye mafanikio ya juu.
15. Ndio maana kijana unatakiwa uhangaike mchana na usiku kujikuza, kuongeza kipato chako, kuongeza hadhi na thamani yako.
16. Nataka nikuambie, Single mother akiitwa kwenye msiba wa Mzazi mwenzake mwenye mafanikio kukuzidi hawezi kukataa.
Kwake hiyo ni heshima kubwa
Kwenye misiba wanawake wanapata Ile heshima na kujisikia fahari watu wakisema Yule pia alizaa na Tajiri Huyu, au Waziri huyu, au Dokta huyu.
17. Lazima uelewe, mkeo atamsikiliza mwanaume aliyezaa naye aliyefanikiwa na anauwezo wa kuvunja ndoa. Na sio ajabu akawa anakushtakia na kutoa siri za hapo nyumbani.
18. Oooh! Baba nani, tushakua sasa hihi, hatuna haja ya kugombana kama watoto wadogo. Unamaisha yako na mimi ninamaisha Yangu. Lakini Sisi bado tunamtoto pamoja.
Mimi maisha Yangu kwa sasa magumu, huyu mwanaume hapa yaani ni mzigo.
Mwanaume atamwambia afupishe, mwanamke atasema niazime laki tatu hapo chapu nitakurudishia huku akijua hatarudisha. Jamaa atarusha.
19. Kijana jipange. Pambana na maisha Kwanza. Usifuate matawi ya juu usiyoyaweza. Hayo wanakula Twiga wenye shingo ndefu.
Shauri yako.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam