Kabla na baada ya ndoa

Kwanza pole kwa changamoto hiyo ambayo najua inaumiza ukiwaza mwanzo na mlipo sasa hivi. Kipindi hiki ndoa nyingi zipo taabani sana, yani mahututi. Katika watu 10 ukikutana nao wakaamua kusema ukweli basi 8 wapo kwenye shida na 2 hawajui wapi wanaelekea.
Sababu kubwa za haya yote ni mabadiliko ya maisha na shetani kwa ukubwa wake yupo kazini kupitia kaazi zetu tunazozifanya, huko tunakosa muda, kipato kinachoeleweka kukidhi mahitaj yetu ya kila siku.
Usijaribu kipindi hiki kuongelea swala la kuachana kama suluhu na usitegemee njia moja italeta suluhu, mfano ukijifanya kumpa kila kitu anaweza asione umuhimu akazidi, ukimhubiria zaid pia anaweza asikubali, ukichepuka inaweza leta shida zaid. Jaribu kumsikiliza zaid kwakuwa yeye ndio mwenye shida, kila siku muulize kwa upole anataka nini ili akae sawa? ikibidi muombe aende kwao kwa muda mfupi au safiri naye kwenda kwao, akikataa usimlazimishe kwani kuna siku ataona yeye ni tatizo kwakuwa ushamuuliza ujue wapi pa kurekebisha.
Mwisho kuwa na subra sana, binadamu kuna vipindi wanapitia huzuni kubwa sana na ni wao wenyewe wanaweza kuzibadili na sio mwingine, usiwe muongeaji sana mkiwa wote na msikilize sana na toa majibu yanayohitajika kwa wakat huo. usijaribu kumtolea mifano ya watu wengine ili kumrekebisha hiyo hali
 
Ww usha
Ushauri wako unauwa
 
Haya maneno huwezi kuyaelewa kama hujaingia kwenye ndoa kimeo... Huwa natamani kuiona expire date kwenye cheti changu
 
Sio single mother tu wanawake ndio walivyo kabla ya ndoa wanajituma ila ukishaingia mkenge ukaoa na akawa na uhakika wa namba huna rangi utaacha kuiona

Mpandishe cheo mkuu utaona milango itakavyo funguka hutaamini
Nalo neno, kuna wkt lilinijia wazo la kumpandisha cheo ila nikaona kama mambo yatakuwa mengi ila nadhani hili nalo niliangalie
 
Utatuzi ni kutafuta chanzo chake ni nini. Jitahidi kutafuta chanzo cha hayo. Au Kuna mambo ya nyuma alifikiri angesahau yalimuumiza. Haina mbaya wa kudumu
 
View attachment 3156921
Hali ya sasa ilivyo inatisha sana, Mungu tusaidie
Ni vile tu kuta haziwezi kuzungumza ila kwenye ndoa hasa hizi za kisasa kuna vioja vingi sana... Kataa ndoa huwa nawaelewa sana ila ndiyo basi tena nimeshayavagaa naishi kwa 7bu ya watoto na heshima kwa jamii

Na hata ukituona kwa macho ya nyama huwezi kuhisi chochote. Tulijifunza kugombana tukiwa wawili. Ila sasa moyo wangu umechoka
 
Pole mkuu kama habadilik na inakutesa achana nae
Watoto, na jicho la wananzengo lakini pia misingi ya kiuchumi nilivyoiseti ndiyo nilizingua zaidi maana ujasiri wa kumfurusha nautolea wapi wkt nae anajiona ni sehemu ya umiliki halali wa vile alivyonikuta navyo

Nilipozingua: wkt anakuja kwenye maisha yangu ile kindaki ndaki na akiwa wa moto, mahaba kama yote, future njema niliona nimtunuku uaminifu kwa kumpa codes zote za kiuchumi. Kwa sasa najuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…