Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Wengi tukisikia mbilikimo huwa tunawaza wale wa misitu ya Congo, lakini historia inaonyesha kusini yote ya Africa, yaani kuanzia misitu ya Congo, kuja Uganda, Kenya kidogo, Tanzania yote hadi Africa kusini kulijaa mbilikimo na Wasan (Wabushemen). Wabantu walipokuja wakachanganyana na mbilikimo na kutuzaa sisi watu wa eneo la kusini mwa Africa.
Kitabu cha historia ya Wagogo kinaonyesha kuwa kabla ya Wagogo, nchi ya Ugogo ilikaliwa na mbilikimo walioitwa Wagomvia. Kitabu kingine kuhusu asili ya Wachagga kinasema kuwa kabla ya Wachagga, miteremko ya Kilimanjaro ilikaliwa na mbilikimo walioitwa Wakonongo. Inaonekana mbilikimo hawa wawindaji walitapakaa nchi yetu hii yote.
Watanzania na watu wengi wa kusini mwa Africa si Wabantu halisi. Tu wabantu na mbilikimo.