Kabla ya kuichangia CCM, Tafakari kwa Umakini, Maana inaweza kuwa laana yako

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
CCM ndiyo chama chenye Serikali. Uovu wote unaofanyika dhidi wananchi, kama vile utekaji na mauaji ya wakosoaji wa Serikali na Rais, uporwaji wa rasilimali za Tanganyika, vyote hivyo vimeridhiwa na CCM, ndiyo maana wanaoyafanya hayo hawabughudhiwa wala kuchukuliwa hatua na Serikali ya CCM.

Mifumo, sheria na kanuni zote za kudhulumu haki za wananchi kwenye michakato ya uchaguzi, vimetengenezwa na CCM. CCM ndiyo imeandaa uchaguzi bandia wa mwezi Oktoba, uchaguzi usio na ushindani. Kama uchaguzi hauna ushindani, CCM inahitaji bilioni 100 za nini?

Kama wewe ni mtu mwema unayewapenda binadamu wenzako, na ungependa kuuishi upendo wa Mungu, kumwe usijihusishe na uchangiaji kwa CCM au viongozi wake. Badala yake tuungane katika kumlilia Mungu ili atusaidie kutuondolea hili zigo lililotuelemia, liitwalo CCM.
 
Mimi nitachagia!
 
Hawa watu c juzi hapa wamegawa baiskeli nchi nzima leo tena wanataka michango

Hapo kuna kiini macho wanataka kutuzuga kma wanachangiwa kumbe hiyo pesa wamekwapua mahali
 
Hiyo Michango ni geresha, wewe ile msafara wa watu 1000 wa kwenda tuu kuchukua form ghARAMA ya huo msafara ni zaidi ya mchango unaohitajika
 
Naishi nalo hilo la laana yako 📌
 
Chadema mnajifanya mnajua kila kitu wapumbavu nyie
 
After 67 years, I finally came to understand why some men slip away into a quiet, private life, far from the noise.
 
inamaana hakuna jema walilowahi kufanya au wanalofanya au mihemko tu.
 
Ni kweli, hiyo ni kama sadaka, ukitoa ni umejiunganisha na hao jamaa katika ulimwengu wa kiroho. Tayari laana na vilio vya watu vinaanza kukufuata ww na uzao wako.
 
Ccm wala hawahitaji mchango wowote, kinachofanyika hapo ni utakatishaji wa pesa, kuna pesa zinataka kuhamishiwa kwenye hiyo account.
By the way kwangu naona wacha wafanye tu wanavyotaka mzunguko wa pesa utaongezeka kipindi hiki maana hatuna cha kuwafanya tutabaki kulalama, hawa dawa yao ni kuangalia mifumo yao ya pesa hakikisha na wewe zinakupitia kwenye channel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…