CCM ndiyo chama chenye Serikali. Uovu wote unaofanyika dhidi wananchi, kama vile utekaji na mauaji ya wakosoaji wa Serikali na Rais, uporwaji wa rasilimali za Tanganyika, vyote hivyo vimeridhiwa na CCM, ndiyo maana wanaoyafanya hayo hawabughudhiwa wala kuchukuliwa hatua na Serikali ya CCM.
Mifumo, sheria na kanuni zote za kudhulumu haki za wananchi kwenye michakato ya uchaguzi, vimetengenezwa na CCM. CCM ndiyo imeandaa uchaguzi bandia wa mwezi Oktoba, uchaguzi usio na ushindani. Kama uchaguzi hauna ushindani, CCM inahitaji bilioni 100 za nini?
Kama wewe ni mtu mwema unayewapenda binadamu wenzako, na ungependa kuuishi upendo wa Mungu, kumwe usijihusishe na uchangiaji kwa CCM au viongozi wake. Badala yake tuungane katika kumlilia Mungu ili atusaidie kutuondolea hili zigo lililotuelemia, liitwalo CCM.