Na. M. M. Mwanakijiji
Hakuna jinsi. Kinachotokea CHADEMA ni matokeo tu..
Nashauri wafanye uamuzi kuwa atakaye peperusha bendera ya mgombea wa Urais HATOKUWA Mwenyekiti wa chama na kuwa Mwenyekiti wa chama hatokuwa mgombea Urais au Ubunge. Jukumu lake liwe kwenye chama.
Kwanini sasa?
Ni kwa sababu ya Tundu Lissu tu dhidi ya Freeman Mbowe?
Kwani huyu Mbowe ana nini alichobeba cha CCM kiasi cha kuja na mapendekezo haya?
Sababu ya maswali hayo ☝🏻☝🏻ni kuona kuwa watu tuliodhania siku zote ni wapigania mageuzi na mabadiliko ya kisiasa na mfumo wa utawala wa nchi hii kina Freeman Mbowe, Ansbert Ngurumo, wewe
Mzee Mwanakijiji na wengine kibao kumbe siyo kabisa...
It's obvious kuwa mapendekezo yako haya ni kwa ajili ya kutafuta kila possibility ya aidha Freeman Mbowe au mtu ambaye mfumo umemwandaa toka CCM kuja kugombea u - Rais CHADEMA ili mradi Tundu Lissu asipate kabisa fursa hiyo iwapo atakuwa mwenyekiti wa CHADEMA (possibility yake mpaka sasa ni zaidi ya 80%)
Wakati wa kampeni za uchaguzi atakayetangazwa kuwa mgombea wa Urais anakuwa mara moja kuwa ndiyo kiongozi mkuu wa chama hadi baada ya uchaguzi.
Huu ni utaratibu wa wapi aisee..?
Yaani mgombea tu wa u - Rais, akipata nafasi hiyo, basi mwenyekiti aliyepo kikatiba anaacha kuwa mwenyekiti badala yake aserende uenyekiti wake kwa huyu mgombea..?
Unasema "hadi baada ya uchaguzi". Halafu baada ya hapo? Una maana akiwa ameshinda ndiyo yeye anakuwa Mwenyekiti wa chama ? Vipi huyu aliyechaguliwa kikatiba? Yeye aende wapi? Na vipi akiwa ameshindwa?
Mgombea wa Urais kimadaraka anakuwa juu ya Mwenyekiti wa chama.
Huko mliko USA na Ulaya ndivyo wanavyoendesha vyama vyao?
Faida za hili ni rahisi kuziona. Kubwa ni itaondoa mvutano wa madaraka. Maaana yake ni kuwa wamuombe mtu ambaye anaweza kweli kupeperusha bendera ya ugombea ili awavushe bila mtu huyo kuutaka uenyekiti wa chama.
Yupo Tundu Lissu...
Kamwe hawezi kuwa Freeman Mbowe....
Kamwe hawezi kuwa kapi lolote toka CCM...
CHADEMA wakirudia makosa yao ya mwaka 2015, nitawadharau na kuwafuta kabisa ktk kumbukumbu zangu...
NOTE:
1. All in all, pendekezo lako hili lina ishara zote muhimu kuwa Freeman Mbowe (anayehaha sasa kuokoa uenyekiti wake) alishaandaa mtu wake aliyepewa na Bi Samia Suluhu Hassan mwenyekiti wa CCM aje CHADEMA kugombea u - Rais..
2. Hai make sense yoyote wewe
Mzee Mwanakijiji (tunayedhani unaheshimika hapa jukwaani) kuja na ushauri na pendekezo hili la ajabu kabisa..
3. We all know and understand that, mission ya haya yote ni kuhakikisha Tundu Lissu hawi mwenyekiti CHADEMA. Hili mmeshaliona kama vile linakwenda kufeli na likely kuwa limeshafeli. Na kwa kuwa uwezekano wa huyu asiyetakiwa na mfumo wa ma - CCM a.k.a "WASIOJULIKANA" kuwa kiongozi wa CHADEMA, unaelekea kufeli, umetumwa kuchokoza kwa kuleta plan C (plan A & B zote kwa mpigo ziligonga mwamba), ili kuhakikisha huyu Bwana Tundu Lissu hashindani na mama yenu a.k.a Chura Kiziwi, kwenye uchaguzi mkuu wa u - Rais mwaka huu 2025 kama utakuwepo...
Pole sana.....