Kabla ya kumjadili Kenani Kihongosi turejee kisa cha Hayati Samwel Sita na harakati zake pale UDSM

Habari wadau..!
Juzi watu walikuwa wanapiga kelele kitendo cha mkuu wa wilaya Kenani Kihongosi kutandika viboko wale wahuni walioiba madawati ya shule.

Binafsi nikawa na cheka tu maana akanikumbusha kisa cha Hayati Mwalimu JK Nyerere na mzee wetu spika wa mstaafu Hayati Samweli Sita (Mungu awalaze pema peponi).

Kifupi mimi sikuwapo kipindi hicho ila wakati nipo pale UdSM miaka ya nyuma nafanya shahada yangu ya kwanza jamaa yangu mmoja kuna siku tulikuwa tunapita pale Fuculty of Law au kwa jina jingine Kitivo cha sheria a.k.a "kitivo" wakati tunatembea alinishika bega na kunionyesha sehemu ambayo inasadikika Mwl aliamtandika mzee Hayati Samwel Sitta viboko kipindi hicho mzee Sitta alikuwa mwanafunzi wa chuo pale UDSM, na kisa kilikuwa kama hivi.

-Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka 1966, wakati yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM, wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi ilikuwa na mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa?

Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Mwalimu Julius Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili. Miezi miwili baadaye akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi hao.

Watukutu wawili – Sitta na Wilfred Mwabulambo (sasa marehemu) na wengine kadhaa – waliojitia wazimu na kutetea kile walichokiita haki zao, (haki za wakulima na wafanyakazi), walimshutumu Mwalimu Nyerere kwa maneno makali wakidai “…ni heri wakati wa ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu”.

Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao”. Miezi kumi baadaye, baada ya Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia akaamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392. Viongozi wa mgomo; Sitta na wenzake 7 walitiliwa ngumu, hawakurejeshwa chuoni.

Busara za viongozi wa chuo zilifanya Mwalimu aliliwe zaidi na kuandikiwa barua mbili maalumu na chuo zenye Kumb. Na. C3/Sa.13 ya 2/3/1967 na C3/Ss.13 ya 9/07/1967. Mwalimu alikubali kilio hicho na kuwaruhusu vijana hao wanane warudi kwa sharti kwamba wale watukutu wawili (Sitta na Mwabulambo) watandikwe viboko na “Mwalimu Nyerere” mwenyewe. Hii ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971.

Turudi kwenye mada yetu je wanaomkosoa Kanani Kihongosi wanaijua hadithi hii???Je hawa wahuni na wezi wa mali za umma hawakustahiri viboko?
Ana mamlaka hayo?
 
Ninakushangaa sana kwa kushindwa kupambanua hata jambo dogo kama hili.
Akina marehemu Sitta na mwenzake walikuwa wanafunzi,na aliyewachapa si tu alikuwa mkuu wa nchi,bali mwalimu pia.Ehee,kwa mwaka ule, Sheria zilikuwa ni Kama za saa hizi?Kwanza hata katiba rasmi ya nchi haikuwepo.Kingine kosa la wale wafanya biashara lilikuwa ni kosa la faini(pennal) Ila la akina marehemu Sitta lilikuwa ni kosa la kiutii au mtazamo.So don't relate the unrelated.
 
Wewe umehusisha vitu viwili tofauti. Wale akina Sita hawakufanya jinai bali ulionekana ni utovu wa nidhamu lakini hawa wa Kihongosi wamefanya jinai ambayo ni prosecutable. Ni wapi unaweza kumshitaki mtu anayekulalamikia kwamba hujamtendea haki? Akina Sita walikuwa wana malalaniko na waliyotendewa haikuwa haki pia kwani mwenye malalamiko husikilizwa na si kutandikwa.
Excellent
 
Sheria hiyo haikuwepo kwa maandishi. Ila viboko viliidhinishwa kisheria kwa wala rushwa siku anaingia na siku anatoka ili akamuoneshe mkewe!
Kumbe ilikuwa kwa wala rushwa tu,na sio kwa wanachuo.Mwalimu alitumia sheria ipi ss hapo??🤔🤔🤔🤔
 
Mwanachuo ndio mwanafunzi mwenyewe!

Tena alikuwa anasomeshwa na serikali!
Labda kwa ulimwengu wa ss lakini zamani mwanachuo sio mwanafunzi 100 pc walikuwa na familia zao na wajukuu ,ss ww ukamchape mtu mwenye familia na watoto ndio maana hakukuwa na sheria ya viboko kwa wanachuo.
 
Wanaopinga hawa wezi wa mali ya umma kuchapwa bakora na DC wanafanana, kwa kiasi fulani, na Blacks wa Marekani. Takwimu zinaonesha kuwa 70% - 75% ya mauaji ya Blacks yanafanywa na Blacks wenyewe, lakini mzungu akiua mweusi mmoja, Blacks wanaingia barabarani kwa kishindo na Black Lives Matter (BLM) slogan yao. Hapa kwetu, hawa hawa wanaopinga DC kuchapa bakora wezi wa mali ya umma, wakiwakamata wezi wa vitu vyao binafsi wanawavisha matairi, kuwamwagia mafuta na kuwapiga kiberiti. Ni unafiki wa aina gani huu?
 
Back
Top Bottom