Kabla ya kushinikiza Law School wafaulishe 'sub-standard advocates', njooni saiti muone wanasheria wasioiva wanavyotia hasara

Kabla ya kushinikiza Law School wafaulishe 'sub-standard advocates', njooni saiti muone wanasheria wasioiva wanavyotia hasara

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Tunapambana sana ili law school iruhusu "chakula ambacho hakijaiva" kiingie meza ya chakula. Jibu liko wazi, walaji wataharisha, wataumwa matumbo.

Nchi yetu imekuwa ikilia kuhusu mikataba ya hovyo inayosainiwa baada ya kupitishwa (vetted) na wanasheria. Nchi yetu imekuwa ikilia kuhusu kushindwa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali

Wananchi wamekuwa wakililia haki zao kupotea, na lawama zao kwa mahakama. Lakini ukichimba sana, chanzo Cha haki ya mwananchi kupotea, ni wakili wa mwananchi huyo kumuandalia nyaraka (pleadings) za hovyohovyo. Wakili kutomshauri mwananchi vizuri, wakili kumuwakilisha mwananchi hovyohovyo tu.

Wananchi wamepoteza maghorofa, mabilioni, mamilioni kwa kukutana na mawakili wa hovyo hovyo.

Ni sawa na kuruhusu daktari ambaye hajaiva kiutaalamu kuingia akufanyie operesheni.
 
Back
Top Bottom