SoC04 Kabla ya kuwaza jinsi gani ya kuiboresha Elimu zaidi nchini, tuiheshimu na tuipe nafasi Elimu tuliyonayo sasa katika nafasi mbalimbali za uongozi nchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

chrisostoms

New Member
Joined
May 10, 2024
Posts
2
Reaction score
3
Kiongozi ni mtu mwenye maono ambayo yatakayowawezesha watu wake kufikia malengo flani waliyopanga au aliyonayo mwenyewe kwa maendeleo ya watu anaowaongoza na jamiii kiujumla.

Uongozi ni kitu muhimu kwenye kila kitu(ngazi) iwe Taifa, familia, Taasisi, Biashara na hata katika maisha ya mtu binafsi inabidi awe na uongozi.

Katika nchi yetu uongozi unapatikana kwanjia mbalimbali, kama kuchaguliwa kwa kupigiwa kura mfano nafasi ya ubunge, uraisi, udiwani na nyinginezo, pia mtu anaweza kuwa kiongozi kwa kuteuliwa mfano mawaziri.

Katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna vipengele vya sheria vinavyowapa nafasi viongozi wenye vyeo mbalimbali, kuteuwa viongozi wengine katika nafasi mbalimbali katika nchi yetu kufanya kazi kwaniaba yao. Mfano sura ya pili kifungu 36(1)(2), inampa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteuwa watu katika ofisi mbalimbali kufanya kazi kwa niaba yake.

Katika uteuzi huo, kunabaadhi ya nyazifa za uongozi vinataja sifa na vigezo vya mtu anayestahili kuteuliwa kuchukua mamlaka ya uongozi usika. Lakini kwa utafiti usio rasmi nilioufanya nimebaini kuwa kigezo cha elimu hakizingatiwi sana katika uteuzi wa viongozi na kama ukizingatiwa huwa siomahususi kulingana na nafasi husika ya uongozi, mfano sifa ya elimu inawezakuwa shahada ila haitaji moja kwa moja ni shahada ya nini inayohitajika kiongozi wa hiyo nafasi kuwa nayo iliaweze kuiongoza kwa ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya nchi.

Matokeo yake tunapata viongozi wenye madaraka ya juu wasiokuwa na Elimu ya vitu wanavyosimamia ikiwemo mawaziri, kwasababu sifa ya mtu kugombea ubunge kielimu ni kujua kusoma na kuandika na mbunge huyohuyo anaweza kuteuliwa na Rais kuwa waziri hivyo kunauwezekano mkubwa kupata mawaziri wanaopewa majukumu ya kusimamia wizara zao lakini hawajayasomea na kupelekea wizara nyingi nchini kushindwa kufanya vizuri na kuleta shida kwa kushindwa kuleta maendeleo katika jamii kama wananchi wanavyo tarajia. Kikawaida bajaji haiwezi kuvuta fuso, waziri ambaye hana Elimu anawezaje kuwaongoza watu wenye Elimu katika sekta husika, siyo kama haiwezekani kabisa ila kwa asilimia kubwa atashindwa kuongoza na mbaya zaidi mawaziri pia ndio huunda baraza la mawaziri, ambalo moja ya kazi yake ni kumshauri Rais ambaye ni kiongozi mkuu wa nchi na mwenye madaraka makubwa kikatiba, kunahatali hapo katika ushauri atakaopewa Rais, kwasababu waziri hawezi kuwa na maono ya mbali kwenye wizara yake kwasababu haijui vizuri, nakama haijui vizuri ataweza vipi kubainisha changamoto na fursa zinazoitaji jicho pevu ilikuweza kuiendeleza wizara husika kwa maendeleo ya wananchi, Waziri wa aina hii ushauri atakaoutoa kwa Rais hautaletatija ya maendeleo ya nchi.

Swala lingine hatakama waziri au kiongozi mwingine anashahada au ngazi yeyote ya Elimu, inapendeza akaongoze kwenye wizara ambayo inaendana na kitu alichosomea. Hapa napo kwa uchunguzi wangu usio rasmi nimebaini viongozi wengi wenye Elimu hawaongozi ofisi walizosomea, mfano unakuta mtu ni Mganga wa Afya kielimu, anateuliwa kuwa waziri anenda kuongoza sekta ya madini, sekta ambayo hajui wachimbaji wamadini wanachangamoto gani au madini yanatoloshwa vipi, na njia gani zakisasa zinafaa kutumika ilikupunguza idadi ya vifo vya wachimbaji wadogowadogo wanapojipatia kipato, kwa kifupi uwezo wake utakuwa mdogo lakini kama akiteuliwa kuwa waziri wa Afya kama alivyosomea na mwenye uzoefu nayo atakuwa anajua changamoto zinazowakabili wagonjwa katika hospitali zetu, atajua changamoto ya waganga katika utendajiwao na changamoto nyingi katika sekta ya Afya ataweza kuzitatua na kunauwezekano akawa na maono mazuri katika wizara hiyo na kupelekea maendeleo ya haraka katika sekta hiyo na Taifa kiujumla. Hivyo kunakila sababu ya kuwapa watu uongozi kwenye vitu walivyosomea.

Pia uhamishaji wa viongozi kutoka ofisi moja kwenda nyingine tofauti na yakwanza, inawapunguzia viongozi uwezo wa kubobea katika sekta husika, kitaalam mtu akifanya kazi kwenye sekta moja anabobea katika ufanyaji kazi na uendeshajiwa wa sekta husika inakuwa ni rahisi kwake kubuni mbinu na njia zakukabiliana na changamoto zinazowakabili, pia inampa nafasi kiongozi kupanga na kutimiza malengo ya mda mfupi na ya mfa mrefu. Hapa napo kwa uchunguzi usio rasmi nilioufanya nimebaini kunachangamoto ya kuwahamisha viongozi walioteuwa kutoka eneo moja kwenda lingine, mfano mawaziri wetu nchini wamekuwa wakibadilishwa mara kwa mara kwasababu mbalimbali hivyo wanashindwa kupata uwezo wa kuongoza wizara zao.

Miongoni mwa matokeo mabovu yanayosababishwa na viongozi kutumikia ofisi walizonazo nipamoja na kushindwa kubainisha na kutatua changamoto ya eneo husika, kuchelewa kwa maendeleo, migogoro, umaskini na vipo na zaidi ni kupotea na matumizi mabaya ya fedha ya Serikali Kabla ya kuwaza jinsi gani ya kuiboresha Elimu zaidi nchini, tuiheshimu na tuipe nafasi Elimu tuliyonayo sasa katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini.

Hivyo tuitumie kwanza vizuri Elimu waliyonayo watanzania ituongoze, kuliko kuwateuwa watu kwasababu ya undugu, urafiki ama rushwa ili tuweze kuijenga Tanzania imara na nzuri tutakayojisifia nayo sisi na vizazi vijavyo kabla ya kufikilia kuiboresha zaidi Elimu inayotolewa nchini.

Picha chanzo jamiiforums

1715877826871.png
1715878202397.png
1715879695830.png
D4C758E9-86AF-4FEB-A10E-D57BF9DA4183.jpeg
8A2DB7AD-A337-4476-B3E5-29093BF10D36.jpeg
AFCF84F2-D21D-40E7-94BF-EC27512B40B1.jpeg
0095B7CA-B64B-4427-A97F-BA8CB2A85723.jpeg
BDFF2B19-6C6C-4933-AAE9-D66F729AFB52.jpeg
54CAD551-5CCC-4ACE-8990-7CD5FB2AE33B.jpeg
1685C5D1-DD8F-4DC2-99D5-CD7EEC5C6B03.jpeg
258FE380-2330-4EE5-936C-3D26E60EA174.jpeg
 
Upvote 4

View attachment 2991779View attachment 2991783View attachment 2991798View attachment 2991821View attachment 2991822View attachment 2991824View attachment 2991826View attachment 2991829View attachment 2991830View attachment 2991831View attachment 2991832
 
awaida bajaji haiwezi kuvuta fuso, waziri ambaye hana Elimu anawezaje kuwaongoza watu wenye Elimu katika sekta husika, siyo kama haiwezekani kabisa ila kwa asilimia kubwa atashindwa kuongoza
Tungefanya kama makampuni ya kifamilia yanavyofanya: mtoto anaanza kwanza kuvuna zabibu, baadaye anaungana na kitengo cha kuzichachusha kwenye mabalasi. Baadaye ameshakua sasa anaungana na kitengo cha mauzo na matangazo, anapambana na changamotooo hadi anakuwa nondo. Ndio kisha anapokea nafasi ua u vice president wa kampuni..... na akiwa bora anakuja kuchaguliwa president wa brand nzima.

Mtu kama huyo kwa uzoefu wake ataongoza hiyo biashara ya wine na vodka kikamilifu kabisa maana kuanzia uzalishaji hadi mikataba anao uzoefu.

Na sie sasa ni kwa nini vyeo visiende zaidi kwa waliocheza na hiyo idara karibi sekta zote za hiyo idara. Mfano Dr. Ndugulile alivyokuwa afya na ni kweli amewahi kufanya udakitari saaaafi.

Mi mada yako nimeikubali bro.
Hivyo kunakila sababu ya kuwapa watu uongozi kwenye vitu walivyosomea.
Sawa......

Lakini pia tuwape uongozi zaidi wale watu ambao wamesomea fani mbalimbali maana wanakuwa na uelewa wa hali ya juuu sana. Mfano mtu aliyechanganya elimu ya uinjinia na afya na madini anafaa zaidi kuliko aliyejifukia katika elimu moja tu. Ilo hata anaposimamia ujenzi wa hospitali, atahakikisha inakidhi matakwa ya kiafya na uthabiti na hatapigwa kwenye vifaa vya ujenzi.

Kiufupi tu viongozi wawe wenye akili kubwa. Dalili moja ya akili kubwa ni udadisi utakaothibitishwa na vyeti katika taaluma mbalimbali
 
Shukran bro🙏🏽
 
Back
Top Bottom