Kabla ya kuwaza kukopa fikiri kwanza haya

Michael Chairman

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
922
Reaction score
586
Watanzania wengi kwa sasa wametambua na kuona fursa nyingi ikiwemo fursa ya mikopo kama sehemu kubwa ya wao nao kujikwamua kiuchumi ni jambo jema sana kuwa na macho ya fursa kwa ulimwengu huu wa habari.

Naomba nitumie mda huu nami kukushirikisha mawazo huru juu ya mikopo fuatana nami. Kabla ya kuwaza kukopa kwanza unashauriwa kufikiri haya kwanza;

1. Epuka kuchukua mkopo kwa sababu unapatikana, chukua mkopo kwa ajili ya Biashara tu.

2. Pesa ya mkopo si yako.

3. Chukua mkopo kwa kiwango cha Biashara yako tu na si vinginevyo.

4. Usitumie pesa ya mkopo kwa matumizi ya kawaida kama kununua sofa, Tv, kutoka out, kumpa mtu kama zawadi.

5. Kama una nguvu ya fedha zako tumia zako kwanza.

6. Mgawanyo wa kiasi cha asilimia ya Biashara kwenye pesa ya mkopo ni 60% kiasi chako cha fedha na 40% ni fedha ya mkopo.

Kama na wewe una nyingine kanuni ongezea hapa ili tujikomboe watanzania.
 
well said!!
reginald mengi aliwahi kusema kama unaogopa kukopa basi huwezi kuwa tajiri.
kopa kwa sababu maalumu!!
 
Swala la riba ni la kuzingatia sana,kuna benki wanachaji riba % kadhaa kwa mwezi ukizidisha kwa mwaka mzima unakuta riba inakaribia 60%, yaani hakuna tofauti na hawa loan sharks.

Hakikisha unasoma mkataba vizuri na kujua riba yako na sio tu kufurahia kwamba hii benki fasta wanakupa pesa{ndani ya siku 2 tu} jiulize ni kwa manufaa ya nani wanafanya ivyo?
 
Swala la riba ni la kuzingatia sana,kuna benki wanachaji riba % kadhaa kwa mwezi ukizidisha kwa mwaka mzima unakuta riba inakaribia 60%, yaani hakuna tofauti na hawa loan sharks. Hakikisha unasoma mkataba vizuri na kujua riba yako na sio tu kufurahia kwamba hii benki fasta wanakupa pesa{ndani ya siku 2 tu} jiulize ni kwa manufaa ya nani wanafanya ivyo?

Huu ujumbe uwafikie axcess bank na advance bank
Hawa jamaa riba yao ni kubwa jabu

_Kuna jamaa mmoja alikopa pesa kwa dhamana vitu ndani,jamaa akapatwa na ugonjwa ambao ulimlaza ndani muda mrefu ila akawa analipa kiaina akaja akakwama kabisa imebaki kma ml moja na kidogo
Huwezi kuamini wafanyakazi wa axcess bank walienda wakakomba kila kitu wakamuacha jamaa na.kitanda alicholalia tu
Na jamaa hakuchukua round alifariki...it's so sad

Mikopo ya axcess na advance haina bima na ukifa ndugu zako lazima wawajibike
 
Ukweli mtupu kaka,na hizi Bank sikufichi muda sio mrefu zitapotea kabisaa.Maana mtu akikopa kwao mara moja harudi.Kwa hiyo kwa muda fulani uendeshaji utakuwa issue.
Halafu kama sikosei Advans Bank ni ya jamaa wa nje ya nchi,sasa hawana uchungu na raia.Wakiisha chuma haooo
Maana website yao hata email haina,hahaha kazi kweli,hii nchi kuna vibenki uchwara kibaoooo
 
Hata Azania Bank nao hawana bima. Inabidi watu wawe makini kwa hili.
 
Ukweli mtupu kaka,na hizi Bank sikufichi muda sio mrefu zitapotea kabisaa.Maana mtu akikopa kwao mara moja harudi.Kwa hiyo kwa muda fulani uendeshaji utakuwa issue.
Halafu kama sikosei Advans Bank ni ya jamaa wa nje ya nchi,sasa hawana uchungu na raia.Wakiisha chuma haooo
Maana website yao hata email haina,hahaha kazi kweli,hii nchi kuna vibenki uchwara kibaoooo
Mkuu hizi benki zinazoexploit wateja wake ni ngumu sana kupotea kwa sababu watu wengi wanaokopa huko wanakuwa desperate na iyo pesa, na wengine unakuta hawakopesheki kwenye taasisi nyingine. Vile vile ni watu wachache wanaotaka kujua riba kabla ya kukopa, wengi wanaangalia watapewa mpaka sh ngapi
 
Namfumo wa makampuni ya Sim yanavyokuwa kwa kasi katika huduma za fedha.Bank hizo lazima zitaachia tu.
Juzi nasikia Voda mpaka sasa wanahudumia huduma ya M-Pesa nchi 9 Africa.
Na wanatarajia ku launch kwa kujiunga na MTN ambapo wateja wataweza kutuma pesa sehem yoyote Africa ndani ya mwaka huu kama sikosei.
Sasa hapo ndio balaa.Yetu macho na hii BOT mbofumbofu inayotoa vibali bila kufuatilia lengo la muombaji kwa kina na utendaji wake wa kila siku.
 
Huu ujumbe uwafikie axcess bank na advance bank
Hawa jamaa riba yao ni kubwa jabu

_Kuna jamaa mmoja alikopa pesa kwa dhamana vitu ndani,jamaa akapatwa na ugonjwa ambao ulimlaza ndani muda mrefu ila akawa analipa kiaina akaja akakwama kabisa imebaki kma ml moja na kidogo
Huwezi kuamini wafanyakazi wa axcess bank walienda wakakomba kila kitu wakamuacha jamaa na.kitanda alicholalia tu
Na jamaa hakuchukua round alifariki...it's so sad

Mikopo ya axcess na advance haina bima na ukifa ndugu zako lazima wawajibike

Tatizo watz wanadhani mkopo ni fadhira yaani mtu akipatwa na shida kidogo many excuses. Hawaweki kipaumbele kulipa mkopo. Kwa nn bima ya mkopo nilipiwe na benki wkt binafsi naweza kwenda kukata bima nnayotaka km ajali' afya, moto, kifo etc.....huu ndo umasikini wa fikra
 
Ukweli mtupu kaka,na hizi Bank sikufichi muda sio mrefu zitapotea kabisaa.Maana mtu akikopa kwao mara moja harudi.Kwa hiyo kwa muda fulani uendeshaji utakuwa issue.
Halafu kama sikosei Advans Bank ni ya jamaa wa nje ya nchi,sasa hawana uchungu na raia.Wakiisha chuma haooo
Maana website yao hata email haina,hahaha kazi kweli,hii nchi kuna vibenki uchwara kibaoooo

Ni ya Mfaransa
 
Back
Top Bottom