Kabla ya Ulimwengu kuwepo, kulikuwa na nini? πŸ€”πŸŒ

Mkuu, hoja yako ina mantiki, lakini kuna tofauti kati ya kile tunachoweza kuthibitisha kisayansi na kile tunachokiamini kifalsafa au kidini. Kusema chanzo cha kwanza hakihitaji chanzo kingine ni msimamo unaowezekana, ila swali linabaki: tunawezaje kuthibitisha kwamba chanzo hicho hakina mwanzo? πŸ€”πŸŒŒ
 
Umemaliza mkuu, noted!
 
Vacuum yenyewe ni utupu, lakini kwenye falsafa ndipo maswali yanaanzia: kama mwanzo kulikuwa na utupu, basi ulimwengu ulitokeaje? Na je, utupu ni kutokuwepo kwa kila kitu, au ni hali ambayo bado ina kitu ndani yake? πŸ€”πŸ”₯
Uumbaji ni transformation of energy from one form to another...hivyo kabla ya Mungu kufanya transformation ya uumbaji kulikuwa na ENERGY TU ...ENERGY HAIKUUMBWA IPO MILELE NA MUNGU NI UFAHAMU WA HIYO ENERGY KWA UJUMLA......HATA SISI TULIKUWEPO KABLA YA KUUMBA NA VITU VYOTE VILIKUWEPO ILA SIYO KATIKA FORM HII
 
swali linabaki: tunawezaje kuthibitisha kwamba chanzo hicho hakina mwanzo? πŸ€”πŸŒŒ
Hatuwezi kuthibitisha kisayansi (katika maabara) kwamba chanzo cha kwanza hakina mwanzo.

Sayansi inafanya kazi kwa kutumia vipimo, majaribio, na uchunguzi wa kimaada (empirical evidence). Kwa sababu sayansi yenyewe ilianzia ndani ya ulimwengu huu baada ya muda na nafasi kuanza, haina chombo cha kupima au kushuhudia kilichopo nje ya mfumo huo.
 
Kuna maswali ukiuliza kibinadamu huwezi kupata majibu sababu wote mim/sisi na wew tunakinzana mawazo ila naamini kuna mwenye majibu yote haya ila sio binadamu wa kawaida
 
Wagwan broo man,

Naona swali namba tatu limebeba ujumbe mzima na kwa ufupi kabisa

So far sayansi haijathibitisha kabla ya ulimwengu kulikua na nini.

Swali lako kuu kutoka kwenye thread. Linahitaji falsafa na imani

Sayansi haitoi maana ya maisha lakini imani na falsafa zinatupa kusudi la kuwepo hapa.
 
Jambo la msingi ni kwamba hakuna mwenye jibu lenye mantiki na mashiko kuhusu hili swali mpaka sasa, labda huko mbeleni jibu litakuja kupatikana ila mpaka sasa hakuna jibu la maana kuhusu hili swali.
 
Big bang theory
 
Hili swali huwa halina jibu la kueleweka, kwsbb hata Binadamu hakuwepo wa kujua hayo 🀣🀣
 
Baada ya huu Uzi,utaleta Uzi mwingine ukilalamika maisha yako magumu,unapiga hatua za mlevi wa chang'aa (mbili mbele,nane nyuma)
Au ushapat kaz
Hapo akili ya kuchangia kwenye huu uzi huna umeanza kumshambulia mtoa uzi! mkuu hapa hamna penzi kitovu cha uzembe, hapa ni mambo ya gravitational force tu. Na hakuna kuleta mambo ya nani aliumba na kuumbwa.
 
Tatizo la falsfa na imani kila mtu ana ya kwake. Waislamu, Wakristo na Wayahudi wana zao zinazokaribia kufanana, Wahindu wana yao tofauti, Wabudha wana yao n.k
Sasa sijui ipi ni ya kweli hapo.
 
Labda tujue kwanza maana ya kutokuwa na kitu chochote ni nini. Hakuna kitu maana yake ni nini? Nahisi hapa kwenye hakuna kitu ndo kuna siri. Ukute hakuna jambo kama hilo, hakuna kitu haipo.
 
Hoja yako ina hoja ya kifalsafa inayostahili kujadiliwa, lakini kuna swali moja muhimu: kama energy haikuumbwa na imekuwepo milele, tunajuaje hilo kwa uhakika? Kihisabati na kisayansi, energy huhifadhiwa katika mifumo inayofuata sheria za uhifadhi wa nishati, lakini hilo pekee halithibitishi kwamba energy imekuwepo milele. Pia, kusema Mungu ni ufahamu wa energy kwa ujumla ni mtazamo wa kifalsafa unaohitaji hoja zaidi.


Swali langu ni hili: je, Mungu ni energy yenyewe, ufahamu unaotawala energy, au Muumba aliye nje ya energy? Maana majibu hayo matatu yanaweka msingi tofauti kabisa wa kuelewa uumbaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…