Kabla ya Ulimwengu kuwepo, kulikuwa na nini? 🤔🌍

Hoja yako inavutia, lakini kuna jambo la kutofautisha hapa: je, energy ni sawa na ufahamu? Kisayansi, nishati ni sifa ya kimwili inayopimika, lakini haijathibitishwa kwamba nishati ina ufahamu au kwamba Mungu ni nishati. Hilo linaingia zaidi kwenye falsafa na imani.

Swali langu ni hili: kama sisi ni sehemu ya ufahamu wa Mungu na tulikuwepo milele ndani ya uungu wake, ni nini kinachotufanya tusijitambue kama tulikuwepo kabla ya kuzaliwa? Hapo ndipo hoja yako inakuwa na jambo la kutafakari zaidi.
 
Mnanichanganya tu na nyuzi zenu za maswali ambayo mwenye majibu yake ni mpaka ufunge siku 40 milimani huko ili uweze kuongea nae. Hebu tuongeleeni siasa sasa eti mama kastroko mdomo umepinda upande???
 
Jambo la msingi ni kwamba hakuna mwenye jibu lenye mantiki na mashiko kuhusu hili swali mpaka sasa, labda huko mbeleni jibu litakuja kupatikana ila mpaka sasa hakuna jibu la maana kuhusu hili swali.
Hata nyie Wali nazi,mchicha mwiba hamna majibu?
 
Kabla ya Ulimwengu kuwepo kulikuwa na Ulimwengu.
 
Agree. Nadhani hakuna kitu ni concept ya mwanadamu kuelewa anachotafsiri kuwa kipo otherwise hakuna kitu ni uwepo wa kisichoeleweka kwa mwanadamu.
 
Agree. Nadhani hakuna kitu ni concept ya mwanadamu kuelewa anachotafsiri kuwa kipo otherwise hakuna kitu ni uwepo.
Nakubaliana na hoja yako kwa kiasi fulani. Huenda “hakuna kitu” ni dhana iliyojengwa na akili ya mwanadamu kuelezea kutokuwepo kwa kitu anachoweza kukitambua. Lakini swali linabaki: ikiwa hakuna kitu kabisa, hata nafasi na muda havipo, tunatumia nini kuthibitisha kutokuwepo huko? Inawezekana kabisa kwamba tunapojaribu kufikiria kutokuwepo, tayari tunakigeuza kuwa aina fulani ya uwepo katika fikra zetu. Hapo ndipo fumbo linapoanzia. 🤔
 
Reactions: Tsh
Kwanza kabisa unajua historia ya muda?
Ndiyo, lakini ningependa kusikia mtazamo wako pia. Historia ya muda inavutia kwa sababu tunajua jinsi muda unavyopimwa, lakini swali ni je, muda wenyewe ulianza lini? Je, muda ulikuwepo kabla ya ulimwengu, au muda wenyewe ni sehemu ya ulimwengu ulioanza kuwepo? Hapo ndipo mjadala unakuwa wa kina zaidi. 🤔
 
Yes. Hahaha.
 
Umeelewa nilchokwambia boss..hakuna binadamu wa kawaida kujua ukweli wa hilo.. sababu hatuna ushahidi halisi wa kujibu hiloo kwa uwezo wetu kwa sasa,ni imani tu tuliyoyakuta ulimwenguni
Nakuelewa boss. Ukweli ni kwamba kuna tofauti kati ya kile tunachoamini, kile tunachoweza kuthibitisha, na kile ambacho bado hatukijui. Huenda tumekuta imani hizi kutoka kwa waliotutangulia, lakini hilo halimaanishi moja kwa moja kwamba ni za uongo au ni za kweli. Swali langu ni hili: je, kutokuwa na ushahidi wa kuthibitisha jambo kunatosha kusema kwamba hatuwezi kulijua, au bado kuna uwezekano wa kulielewa siku zijazo?
 
Qur'an inasema: "Huwa Al-Awwalu wal Akhir" - "Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho." (57:3)


Kwa hiyo kabla ya ulimwengu - Arshi, Kalamu, Malaika, mbingu, ardhi - yote hayakuwepo, alikuwepo Allah Pekee. Yeye hakuumbwa, hakuzaa wala hakuzaliwa, na Ndiye aliyeumba muda wenyewe.


Ndiyo maana ulimwengu haukuja wenyewe, bali umetoka kwa Aliyekuwepo kabla ya kuwepo.
 
Tunaishi Duniani "Earth"
Au hujui maana ya Ulimwengu na Dunia?
Najua boss. Dunia (Earth) ni sayari tunayoishi, wakati ulimwengu (Universe) unajumuisha Dunia, sayari nyingine, nyota, galaksi, nafasi na muda. Dunia ni sehemu ndogo tu ya ulimwengu. Swali letu ni kuhusu mwanzo wa ulimwengu mzima, si mwanzo wa Dunia pekee. 🤝 The Icebreaker
 
Alikuwa mwenyezi Mungu na hapakuwa na kitu chochote kabla yake,Arsh yake ilikuwa juu ya maji.kisha akaumba mbingu na ardhi na akaandika kila kitu katika dhikr (lawhul mahfudh)

Alikuwepo mwenyezi Mungu peke yake.
Special pleading fallacy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…