Kabrasha chumba cha kunyongea

Kabrasha chumba cha kunyongea

Hii dunia ina watu wengi sana wenye roho mbaya kiasi ambacho kazi kama hii inagombaniwa na wengi mno. Nina uhakika hata wangesema watu wa kunyonga bila malipo wangepata.
Angeuliwa mtu wako mfano mke ama mtoto kwa kukusudia je unaweza kumsamehe muuaji?
Kama huwezi ujue na wenzio wanahitaji wafanyiwe haki na imetokana na maagizo ya torati ambayo ni yetu sote wakristo na waislamu.
Hata babu zetu kabla ya kuja dini walikuwa na imani zao lakini kifo kwa wauaji ilikubaliwa pia ni sheria za ubinadamu zipo moyoni alishaziandika humo Mungu mwenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
" bwana mnyongaji hukamatwa na kupelekwa kizimabani na kusomewa mashtaka ya mauaji.... Naye hukiri kosa kwa kunukuu vifungu kadha vya Jamhuri ya nchi na hatimaye kuachiwa huru..... "

Kwa nini bwana mnyongaji ashitakiwe kwa mauji peke yake? Je Rais aliye sign hati na kuidhinisha kwa nini nae asishtakiwe?

Endapo mnyongwaji kwenye process ya kunyongwa hatokufa hata baada ya kuachwa kwa muda... nini hutokea??

Cc: mahondaw
 
Adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ni mojawapo ya adhabu kongwe na ya kuogofya zaidi duniani... Na ndio adhabu ya juu zaidi.... Kunyongwa hadi ufe kabisa baada ya kuthibitishwa na mahakama tuhuma zako
Kuna taratibu ngumu na za muda mrefu hadi mtuhumiwa afikie kunyongwa kwakuwa kuhukumiwa kunyongwa ni jambo la kwanza lakini kutimizwa kwa adhabu ni jambo lingine... Unaweza ukahukumiwa kunyongwa na usinyongwe, ni mpaka mkuu wa nchi asaini hati yako ya kifo ndio unaweza kunyongwa!
Kabrasha la chumba cha kunyongea ni kubwa hivyo tuangalie dondoo zake wiki ya mwisho ya kutekeleza adhabu hasa masaa 72 ya mwisho...!!!! Maandalizi huwa mengi lakini haya ndio muhimu zaidi
. Viongozi wa dini huandaliwa kuja kuongea na wale wote wanaosubiri kitanzi..
. chumba cha kunyongea hufanyiwa ukarabati
Mnyongaji huandaliwa
. askari wasaidizi huandaliwa hawaambiwi kuna nini bali huambiwa wanaandaliwa kwa kazi maalum

Siku ya mwisho kuamkia kunyongwa
Ataanza Kiongozi wako wa dini kuongea nawe mara ya mwisho.. Kwa baadhi ya mazingira anaweza kuitwa hata rafiki yako ndani ya gereza
Utapewa chochote unachotaka hasa chakula na kinywaji... Baadhi hudai mpaka damu ya mnyama, sigara ama chakula chochote cha gharama.... Kwa sehemu kubwa hutimiziwa mahitaji yao haya...
Ni usiku wa kuamkia unyongaji, mnyongaji aliyeandaliwa huwekwa mahali pa pekeyake akipombeka usiku kucha
Kunapambazuka... Kiongozi wa chumba cha kunyongea hutoa amri ya wanyongwaji wote kuletwa chumba cha 'condemn' kazi hii hufanywa na wale askari wa kazi maalum
. chumba cha condemn mlangoni kina alama ya X nyekundu na fuvu kubwa...
Wanyongwaji wakiwa tayari na taarifa kuwa huo ndio mwisho wao wakishaingia tu hapa hufungwa vitambaa vyeusi usoni.. Na pingu kubadilishwa toka kufungwa kwa mbele mikononi na kufungwa kwa nyuma
Baada ya hapo huingizwa mlango wa pili kisha mlango wa tatu na wa mwisho ambako ndio kuna kitanzi
Baada ya kufika chumba cha kunyongea huvishwa kitanzi (kwa nchi nyingi za kiafrika) na mnyongaji hubonyeza kitufe kinachofungua milango ya sakafuni na mnyongwaji huning'inia na kitanzi kukaza shingoni na kunyonga....
Baada ya hapo mnyongaji anakuwa ameshaliza kazi yake, sasa kazi ya kwenda chini kufungua vitanzi na pingu na kuvuta miili juu ni ya askari wa kazi maalum... Kazi hii huwa ngumu na ya kutisha maana miili huwa na kila aina ya sura na miili mingine ikiwa bado inavuja damu.. ..
.Wakati wa kuivuta miili juu haivutwi kama unaopoa kitu majini bali hufungwa kamba miguuni na kuiweka mshazari na kuipandisha juu kama jeneza
Baada ya hapo huvuliwa nguo fasta na kuvalishwa shuka la sanda tena mwili ukiwa bado wa moto
Wafungwa walioandaliwa huchukua miili husika na kwenda kuizika fasta kwa makaburi yaliyokwisha chimbwa jana yake... Huko makaburini ni kufukiwa tu na si kuzikwa kwa heshima
Baada ya hapo wahusika wote hulipwa kulingana na majukumu yao na bwana mnyongaji hukamatwa na kupelekwa kizimabani na kusomewa mashtaka ya mauaji.... Naye hukiri kosa kwa kunukuu vifungu kadha vya Jamhuri ya nchi na hatimaye kuachiwa huru.....

Sehemu ijayo tutaendelea na vituko vya wanyongwaji
Asanteni

Kabrasha chumba cha kunyongea - JamiiForums

Hiki ni kitu kipya kwangu-Ahsante kwa elimu
 
Mtu yoyote anaetoka nyumbani kwake na kwenda kumtoa binadamu mwenzake uhai tayari na yeye anakua amejinyima haki yake ya msingi ya kuishi hpa Duniani______Margaret Thatcher former British prime minister
 
Angeuliwa mtu wako mfano mke ama mtoto kwa kukusudia je unaweza kumsamehe muuaji?
Kama huwezi ujue na wenzio wanahitaji wafanyiwe haki na imetokana na maagizo ya torati ambayo ni yetu sote wakristo na waislamu.
Hata babu zetu kabla ya kuja dini walikuwa na imani zao lakini kifo kwa wauaji ilikubaliwa pia ni sheria za ubinadamu zipo moyoni alishaziandika humo Mungu mwenyewe.
Mbona una wenge mazee? Kwani wanaohukumiwa kunyongwa ni wauaji tu?
 
Kwa bongo wala rushwa na wahujumu uchumi bado hawaingii kwenye adhabu hiyo hata wauza madawa ya kulevya sasa labda utujuze zaidi ya wauaji ni hatia zipi tena.
Maana tunaelimishana pia humu.
 
Mtu yoyote anaetoka nyumbani kwake na kwenda kumtoa binadamu mwenzake uhai tayari na yeye anakua amejinyima haki yake ya msingi ya kuishi hpa Duniani______Margaret Thatcher former British prime minister
Hao wanasiasa wa magharibi ni wanafiki sana. Mbona yeye alivyokuwa waziri mkuu alitoa amri kwa jeshi lake kwenda kuua raia maelfu wasio na hatia?
 
Kwa bongo wala rushwa na wahujumu uchumi bado hawaingii kwenye adhabu hiyo hata wauza madawa ya kulevya sasa labda utujuze zaidi ya wauaji ni hatia zipi tena.
Maana tunaelimishana pia humu.
Ndiyo maana nikakuambia una wenge! Mimi nilikuwa namjibu alisema kuhusu wanyongaji! Rudi usome uone tulikuwa tunajibizana nini! BTW Wewe ndiyo unavyofikiri lakini Tanzania hata uhaini unaweza kuhukumiwa kifo! Na pia siyo kila aliyehukumiwa kifo ameua kweli! Na siyo kila aliyeua ana hatia! Nchi zilizo makini kwenye mambo ya hukumu wanafungwa wasio na makosa ije kuwa hapa kwetu kwenye kila aina ua vituko!
 
" bwana mnyongaji hukamatwa na kupelekwa kizimabani na kusomewa mashtaka ya mauaji.... Naye hukiri kosa kwa kunukuu vifungu kadha vya Jamhuri ya nchi na hatimaye kuachiwa huru..... "

Kwa nini bwana mnyongaji ashitakiwe kwa mauji peke yake? Je Rais aliye sign hati na kuidhinisha kwa nini nae asishtakiwe?

Endapo mnyongwaji kwenye process ya kunyongwa hatokufa hata baada ya kuachwa kwa muda... nini hutokea??

Cc: mahondaw
Mkamatwa na kidhibiti ndio mshtakiwa... Akishaingia condemn room lazima afe kwa nyundo au sindano ya sumu
 
Adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ni mojawapo ya adhabu kongwe na ya kuogofya zaidi duniani... Na ndio adhabu ya juu zaidi.... Kunyongwa hadi ufe kabisa baada ya kuthibitishwa na mahakama tuhuma zako
Kuna taratibu ngumu na za muda mrefu hadi mtuhumiwa afikie kunyongwa kwakuwa kuhukumiwa kunyongwa ni jambo la kwanza lakini kutimizwa kwa adhabu ni jambo lingine... Unaweza ukahukumiwa kunyongwa na usinyongwe, ni mpaka mkuu wa nchi asaini hati yako ya kifo ndio unaweza kunyongwa!
Kabrasha la chumba cha kunyongea ni kubwa hivyo tuangalie dondoo zake wiki ya mwisho ya kutekeleza adhabu hasa masaa 72 ya mwisho...!!!! Maandalizi huwa mengi lakini haya ndio muhimu zaidi
. Viongozi wa dini huandaliwa kuja kuongea na wale wote wanaosubiri kitanzi..
. chumba cha kunyongea hufanyiwa ukarabati
Mnyongaji huandaliwa
. askari wasaidizi huandaliwa hawaambiwi kuna nini bali huambiwa wanaandaliwa kwa kazi maalum

Siku ya mwisho kuamkia kunyongwa
Ataanza Kiongozi wako wa dini kuongea nawe mara ya mwisho.. Kwa baadhi ya mazingira anaweza kuitwa hata rafiki yako ndani ya gereza
Utapewa chochote unachotaka hasa chakula na kinywaji... Baadhi hudai mpaka damu ya mnyama, sigara ama chakula chochote cha gharama.... Kwa sehemu kubwa hutimiziwa mahitaji yao haya...
Ni usiku wa kuamkia unyongaji, mnyongaji aliyeandaliwa huwekwa mahali pa pekeyake akipombeka usiku kucha
Kunapambazuka... Kiongozi wa chumba cha kunyongea hutoa amri ya wanyongwaji wote kuletwa chumba cha 'condemn' kazi hii hufanywa na wale askari wa kazi maalum
. chumba cha condemn mlangoni kina alama ya X nyekundu na fuvu kubwa...
Wanyongwaji wakiwa tayari na taarifa kuwa huo ndio mwisho wao wakishaingia tu hapa hufungwa vitambaa vyeusi usoni.. Na pingu kubadilishwa toka kufungwa kwa mbele mikononi na kufungwa kwa nyuma
Baada ya hapo huingizwa mlango wa pili kisha mlango wa tatu na wa mwisho ambako ndio kuna kitanzi
Baada ya kufika chumba cha kunyongea huvishwa kitanzi (kwa nchi nyingi za kiafrika) na mnyongaji hubonyeza kitufe kinachofungua milango ya sakafuni na mnyongwaji huning'inia na kitanzi kukaza shingoni na kunyonga....
Baada ya hapo mnyongaji anakuwa ameshaliza kazi yake, sasa kazi ya kwenda chini kufungua vitanzi na pingu na kuvuta miili juu ni ya askari wa kazi maalum... Kazi hii huwa ngumu na ya kutisha maana miili huwa na kila aina ya sura na miili mingine ikiwa bado inavuja damu.. ..
.Wakati wa kuivuta miili juu haivutwi kama unaopoa kitu majini bali hufungwa kamba miguuni na kuiweka mshazari na kuipandisha juu kama jeneza
Baada ya hapo huvuliwa nguo fasta na kuvalishwa shuka la sanda tena mwili ukiwa bado wa moto
Wafungwa walioandaliwa huchukua miili husika na kwenda kuizika fasta kwa makaburi yaliyokwisha chimbwa jana yake... Huko makaburini ni kufukiwa tu na si kuzikwa kwa heshima
Baada ya hapo wahusika wote hulipwa kulingana na majukumu yao na bwana mnyongaji hukamatwa na kupelekwa kizimabani na kusomewa mashtaka ya mauaji.... Naye hukiri kosa kwa kunukuu vifungu kadha vya Jamhuri ya nchi na hatimaye kuachiwa huru.....

Sehemu ijayo tutaendelea na vituko vya wanyongwaji
Asanteni

Kabrasha chumba cha kunyongea - JamiiForums
Kabrasha chumba cha kunyongea - JamiiForums
Hiiv mkuu ni kila gereza lina hiki chumba ama ni baathi ya magereza tuu?
 
Back
Top Bottom