Ndg watanzania,,mfungwa wa kunyongwa ni mfungwa ambae amehukumiwa na mahakama hukumu ya kunyongwa hadi kufa,,,baada ya hukumu mfungwa huyo uhifadhiwa gerezani( central prison)
Akiwa gerezani huhitaji ulinzi maalumu tofauti na wafungwa wengine ambapo huwa gereza lao ndani ya gereza( hawachangamani) vile vile hupewa mlo special tofauti na wafungwa wengine.
Askari wanaopangwa zamu kuwalinda huvaa tofauti na Askari wengine ambapo Askari hao hawaruhusiwi kuvaa uzi wa filimbi( leniard) pia hawaruhusiwi kuvaa viatu vya kamba mara nyingi huvaa sandals au viatu bila kamba.
Endapo Kuna uhitaji wa kwenda mahakamani msafara wao huwa wa kutisha kidogo ambapo msafara huwa na ulinzi mkali ukijichanganya unalambwa shaba.
Endapo rais atatia saini wafungwa flani kunyongwa mambo yafuatayo yatafanyika.
1.Kitanzi kitasafishwa kuhakikisha mitambo inafanya kazi.
2.Mfungwa atataarifiwa utekelezwaji wa hukumu hiyo( kunyongwa) saa 24 kabla.
3.Askari mnyongaji atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha hafanyi makosa ya kiufundi wakati wa kunyonga.
4.Mganga wa serikali atajulishwa ili afanye vipimo vya afya ya mfungwa husika.
5.Mfungwa atapewa fursa ya kuchagua chakula chochote anachotaka na atapewa.
6.Kiongozi wake wa dhehebu ataitwa ili kufanya maombi kama akihitaji.
7.Ulinzi utaimarishwa mara dufu kuzunguka eneo zima la gereza ukijichanganya shaba inakuhusu.
8.Mfungwa atafungwa kitambaa usoni kuelekea chumba cha mtambo wa kunyongea akiwa chini ulinzi Askari makini na shupavu.
9.Askari mtaalamu wa kunyonga atajongea eneo la kitanzi kwa ujasiri.
10.Mfungwa atavishwa kitanzi
11.Askari atafyatua mtambo
12.Askari atahakikisha mfungwa kanyongwa Hadi kufa ambapo mtambo hupigwa mara tatu kiustadi.
14.Baada ya kuhakikisha kafa hushushwa na mtambo Hadi kwenye andaki ambapo kamba kitanzi hutolewa shingoni na kulazwa sehemu rasmi ya kuoshea mwili.
15.Kaburi huchimbwa eneo rasmi liliandaliwa kwa ajili ya mazishi ya wafungwa.
16.Mwili hubebwa kupelekwa kaburini chini ulinzi.
17.Kuhusu unawekwaje kaburini sitasema.
18.Mkuu wa gereza hutoa amri mwili kufukiwa ,,,tukumbuke mwili huo haukabidhiwi kwa ndugu hivyo hubaki kuwa mali ya jamhuri sijui Kama sheria imebadilika sijapitia
19.Ulinzi utaimarishwa zaidi maana kunakuwa na taharuki kubwa sana kwa wafungwa wote gerezani na wafungwa wengine wa kunyongwa wanaobaki.
Hakuna siku ambayo huwa mbaya kwa wafungwa wa kunyongwa kama siku ambayo husikia chumba cha kunyongea kinafanyiwa usafi hata kama ni zoezi la kawaida tu la usafi,,,wao hudhani tiyari rais Katia saini labda.
Askari wanaolinda wafungwa hawa lazima wawe makini maana wafungwa hawa Wana roho ya kukata tamaa muda hivyo huweza kufanya lolote kwa yoyote,,ukizubaa wanakuua wanasepa.
Kwenu wtz