Kabudi, Polepole wakishiba wataikumbuka KATIBA.

Kabudi, Polepole wakishiba wataikumbuka KATIBA.

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,588
Reaction score
11,668
habari....

Prof kabudi na Polepole walikuwa wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba, ile ambayo chini ya uongozi wa jaji mstaafu joseph warioba ,iliandaa rasimu ya katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi waliyoyakusanya kwa karibu miaka mwili.

Binafsi nimeona munkari prof kabudi kuhusu haja ya kuwepo katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi, alipokaa na waandishi wa habari tarehe 17/4/2017 mjini dodoma aliwahakikishia waandishi kuwa "mchakato bado uko palepale".

Maelezo yake, yalionesha Kama mtu asiyekuwa na uwezo wa kusimamia alichokiamini kabla. Yamkini anakwepa kilichomkuta Nape Nnauye aliyejitoa sadaka kwa kusimamia alichokiamini ni wajibu wake na ni haki kwa umma.

Prof kabudi alisema wazi utekelezaji wake kuhusu suala la katiba mpya utategemea majadiliano atakayofanya na wakuu wake akiwemo waziri mkuu.

Yule alikuwa prof kabudi akifanya kazi Tume ya mabadiliko ya katiba, huyu wa sasa ni prof kabudi waziri wa sheria na Katina.

Waziri prof kabudi hawezi kuthubutu kusema ukweli kwamba Zanzibar ndiyo aliyoanza tangu mwaka 1984 kutaka mfumo wa muungano uwe wa serikali Tatu.

Prof kabudi leo hana ubavu WA kuikumbusha serikali kuwa madai ya serikali tatu yalitolewa na zanzibar na kusimamiwa na rais wake wakati huo, Alhaji Aboud Jumbe mwinyi Kama aliyofanya kwenye kumbukumbu ya miaka 50 ya muungano.

Prof kabudi ambaye leo ni waziri katika serikali ya muungano, hawezi kufafanua matumizi ya jina la Tanganyika kwenye katiba ya sasa, kama aliyofanya akiwa mjumbe wa Tume ya warioba.

Kwa Polepole wa CCM yeye alipokaribishwa "mezani kula" aliutangazi umma kwamba ataendelea kushikilia msimamo wake wa kupatikana katiba mpya yenye maoni ya wananchi.

Msimamo huo ulitoweka ghafla baada ya kuanza KULA. Tarehe 22 desemba, 2016 akiwa kituo cha televisheni cha clouds, alisema "msimamo wangu katika jambo hili utategemea muelekeo wa rais magufuli".

Hapo Polepole alionesha rangi halisi baada ya kusogezwa jikoni.

Polepole aliyekuwa anafahamu Kama mwanaharakati wa kutetea maoni ya katiba mpya si huyu ambaye sasa ni katibu mwenezi wa CCM. Sasa anatetea katiba ya 1977.

Polepole wa sasa si yule aliyebaini mambo 20 muhimu ya wananchi yaliotupwa na katiba pendekezwa 25 Novemba, 2014 ukumbi wa mlimani city.

Polepole hayupo tayari kuwa upande wa wananchi na kuona katiba ikibadilishiwa na madaraka ya mwenyekiti wake wa CCM, rais magufuli yanapunguwa.

Sasa wao wanatumikia sera ya CCM ambayo ni muungano wa serikali mbili tu.

Wanajua wakichomekea hoja ya kutetea maoni ya katiba ya wananchi inayotoka kuwepo Tume huru ya uchaguzi, watafukuzwa MEZANI. hawajali Kama uchaguzi wa 2020 lazima uwe huru na kweli na wazi.

Mr mkiki.

Nilikuwa mwana CCM wa mpito (nikiwa na miaka 5-9) na "Mpinzani endelevu" baada ya kujiridhisha CCM imeshindwa kuongoza vema nchi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani maji ya kijani na njano ni sumu kwa vichwa vya binadamu, ukiyanywa to akili inarudi kwao!
 
Back
Top Bottom