Tarehe 20 Julai, 2021, takribani roketi tatu zilitua karibu na ikulu ya rais wa Afghanistan huko Kabul wakati Rais Ashraf Ghani alipokuwa akisali sala ya Eid al-Adha.
Ingawa hakukuwa na majeruhi waliotokana na kutua kwa roketi hizo, kilichonifanya kuwa interested na tukio hili ni pale Rais Ghani alivyoendelea na sala licha ya milipuko kusikika kwa sauti kubwa huku baadhi ya waumini wakipata tunachokiita “wenge.”
Makombora hayo, yaliyorushwa mida ya saa 2 asubuhi yalisikika na wakazi wengi wa eneo linaloitwa Green Zone, eneo ambalo ndipo ilipo Ikulu na balozi kadhaa, ikiwemo wa Marekani.
Taliban ndiyo yenye kwa sasa, na jana niliona Taliban delegation imepokelewa China. Taliban inawaalika wachina waje wajenge nchi na it seems wachina wako tayari kushirikiana nao. Sasa hivi ndiyo wana control barabara kuu wanakusanya kodi hiyo serikali haina mashiko