Kaburi la Tewa Said Tewa Makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni

Kaburi la Tewa Said Tewa Makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni

Jidu..wazee wa Mohamed walipambana kupata uhuru wa Tanganyika wala sio visiwa vya Unguja na Pemba..hayo wauulize Wazanzibar
Tunajaribu kumshort circuit huy bwana Mohammed Said, yeye hoja yake ni moja tu siku zote, kuwa wazee wake, tena waislamu tu, ndio walioleta Uhuru na sio Mwalimu Nyerere.
Tatizo lake kubwa ni kushindwa kuelezea kuwa wale wazee wake wote walikufa siku moja alipoingia Nyerere au vipi?

Mtu akishajijenga kimawazo kuwa kile anachofikiri yeye ndio ukweli, kumhamisha hapo ni shida mno, maana hata mifano hai kuwa amekosea anaona unampinga tu bila sababu.
 
Jidu..wazee wa Mohamed walipambana kupata uhuru wa Tanganyika wala sio visiwa vya Unguja na Pemba..hayo wauulize Wazanzibar
Kilembwe,
Bahati mbaya kaja na matusi hivyo kwangu nimejiwekea kanuni kuwa mtu akija na lugha isiyo na heshima namkwepa kulinda heshima zetu sote yake, yangu na wasomaji.

John Okello hakuongoza mapinduzi yoyote Zanzibar.

Historia ya Zanzibar inafahamika.

Kassim Hanga ndiye aliyekuwa kiongozi wa mipango yote akisaidiwa na Oscar Kambona.

Kambi ya Kipumbwi walipokuwa wanavushwa Wamakonde kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi iko Tanga na kambi hiyo ilikuwa chini ya Regional Commissioner Jumanne Abdallah na District Commissioner Ali Mwinyi Tambwe.

Nilikuwa msaidizi wa Dr. Harith Ghassany kwa miaka 7 wakati anatafiti kitabu, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."

Huyu ndugu yetu asome hiki kitabu atapata ukweli wa mapinduzi.
Kitabu hiki kipo bure mtandaoni na aingie Google.
 
Tunajaribu kumshort circuit huy bwana Mohammed Said, yeye hoja yake ni moja tu siku zote, kuwa wazee wake, tena waislamu tu, ndio walioleta Uhuru na sio Mwalimu Nyerere.
Tatizo lake kubwa ni kushindwa kuelezea kuwa wale wazee wake wote walikufa siku moja alipoingia Nyerere au vipi?

Mtu akishajijenga kimawazo kuwa kile anachofikiri yeye ndio ukweli, kumhamisha hapo ni shida mno, maana hata mifano hai kuwa amekosea anaona unampinga tu bila sababu.
Jidu...
Mimi nimeandika kitabu cha Abdul Sykes kurasa 400+
Kipo sasa miaka 24 kimechapwa mara 4.

Kimepitiwa na mabingwa wa historia ya Afrika: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan na mapitio yao yote kuchapwa na Cambridge Journal of African History.

Unanisingizia sijasema hata siku moja kuwa ni Waislam peke yao ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Nilichosema kipo kwenye jina la kitabu : ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism. "

Jina la kitabu linaeleza kwa nini niliandika historia ya wazee wangu.

Mimi sina tatizo kama wewe huikubali historia ya wazee wangu wala sikulazimishi uiamini.

Wala sitagombana na wewe kwa fikra zako kuwa historia unayoijua wewe ndiyo kweli kuwa wazee wangu waliuliwa na Nyerere.

Wasomaji ndiyo waamuzi.
Kitabu cha Abdul Sykes kinakwenda chapa ya 5.

1671612637968.jpeg
 
Sasa hilo kaburi liko wapi? Heading tofauti na context.
Dudus,
Kaburi liko Magomeni Mwinyimkuu.
Nina staili tofauti sana ya uandishi.

Kunielewa inabidi utembee katikati ya mistari.
Uandishi ni ''art,'' yaani ni sanaa.

Unaandika mtu anapokusoma anaelimika na anaburudika pia.

Jiulize kwa nini nimeweka picha ya kaburi kisha nikaeleza hayo unayoona wewe kuwa yanapishana na kichwa cha habari.
 
Kati ya watu waongo waongo, wewe mtoa mada umetia fora!
Jidu...
Mwalimu wangu aliyenisomaesha adab katika mijadala Sheikh Haruna alikuwa akinisisitizia jambo moja nalo ni kuwa njia nyepesi ya kujivua heshima mbele ya watu ni kukosa adabu.

Nakuomba na wewe ufaidike katika somo hili la Sheikh Haruna.

Mimi si muongo sina sababu ya kuandika uongo katika historia ya wazee na jamii yangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika na katika kumpokea Julius Nyerere alipofika kwetu mwaka wa 1952.

Ni bahati mbaya sana yeye mwenyewe Mwalimu hakupata kueleza hisani iliyokuwapo baina yake na watu wa Dar es Salaam na wazee wetu walibakia kimya khasa baada ya changamoto kutokea pale uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.

Changamoto zilizotokea baada ya uhuru inataka mada ya kujitegemea kwani kuna mafunzo makubwa ndani yake kuhusu utawala.

Kwa kuhitimisha mimi ndiye huyo hapo chini ambae umejaribu kumfedhehesha kwa kumwita muongo:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002
  2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi
  4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York
  5. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  6. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  8. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
  9. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  10. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
  11. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
  12. Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam
  13. In Praise of Ancestors (1988) Africa Events (London)
  14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London)
  15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam)
  17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam)
  18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003)
  19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003)
  20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004)
  21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004)
  22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006)
  23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi
  24. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg
  25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi
  26. Awards: Several Awards
  27. Visiting Scholar: (2011)
  28. University of Iowa, Iowa City, USA
  29. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  30. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.

1671639800660.jpeg
1671639956803.jpeg

Mexence Melo wa JF akinikabidhi cheti kwa uandishi wa historia katika Jukwaa la Historia 2021
 
Back
Top Bottom