Kaburi linalochagua jinsia

Kaburi linalochagua jinsia

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
8,261
Reaction score
9,733
Ilikuwa siku ya kawaida kama ilivyo siku nyingine yoyote na watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao kama kawaida katika mji wa Greenwood, Indiana.
Sarah msichana mwenye umri wa miaka 24, ambaye alikuwa akijishughulisha na biashara haramu ya kuuza mwili wake na matumizi ya dawa za kulevya alikuwa kazini kama kawaida yake.
Utaratibu wa Sarah wa kujiuza haukuwa wa kusimama barabarani kama wafanyavyo madadapoa wengine, bali yeye alikuwa na agent anayemtaftia wateja, kisha wanapanga muda wa Saraha kutoa huduma ambapo agent wake atampeleka mpaka kwa mteja kisha atamsubiri kwenye gari mpaka utoaji huduma kwa mteja utakapokamilika.
Baada ya huduma atamrudisha Saraha kwake au atampeleka kwa mteja mwingine kutokana na order za wateja walizopata kwa siku hiyo.
Siku hiyo ya tarehe 9/10 agent alikuwa amtaarifu Saraha ya kuwa, kuna kazi ya kuwapatia huduma ya mapenzi wateja watatu wenye asili ya Kikorea waliokuwa wakiishi pamoja, yani wote watatu wamchangie kwa lugha ya wenzetu itakuwa foursome.
Hivyo Saraha alijiandaa kwa ajili ya kuingia kazini, na ilipofika saa nne usiku, agent wake alimpitia wakaelekea kwenye nyumba ambako madude yalikuwa yanaenda kuamshwa.
Saraha alimuacha agent akimsubiria kwenye gari akaelekea kwenye nyumba ambako wateja walikuwa wakimsubiria na kuzama ndani.
Kama kawaida ya kazi yake, hakuchelewa walianza manjonjo na mara ghafla Saraha alianza piga kelele akiwasukuma na kuwazuia wasimsogelee huku akipiga kelele kuwa kuna mtu anataka kumuua.
Walijaribu kumtuliza lakini alizidi piga kelele sana na akachukua simu yake na kupiga namba ya dharura ya 911, ilipopokelewa akapiga kelele huku akilia kuwa kuna mtu anataka kumuua.
Operator aliyepokea akajaribu kumtuliza ili amwelekeze yuko wapi polisi waweze kufika eneo hilo Saraha akakata simu.
Huko nje kelele zikamshtua agent naye akatoka kwenye gari akaenda kuangalia nini kimetokea ndipo alkuta Saraha akiwa kama kapagawa, wale watu wateja wanahangaika kumtuliza lakini Sarah haelewi chochote.
Mara ghafla akatoka nje na kuansa kutimua mbio, agent wake akaanza kumkimbiza ila kwakuwa alikuwa anakimbia kwa kupita barabarani akaona njia bora ni amfuate kwa kutumia gari, hivyo akarudia gari.
Sarah akakakimbia umbali wa mita kadhaa mpaka alipoona makazi ya watu akaelekea na kufuata nyumba moja akawa anagonga kwa nguvu huku akipiga kelele ya kuwa kuna mtu anataka kumuua.
Nyumba hiyo aliyokuwa anagonga afunguliwe alikuwa anaishi mwanaume ambaye umri ushamtupa mkono yani babu ajilikanaye kama Marice.
Marice alinfungulia mlango haraka na kumwingiza ndani kisha akafunga mlango haraka halafu akampeleka na kumkarisha kwenye sofa akimtuliza na kumuuliza nini tatizo binti.
Saraha akamwambia kuna mtu anajaribu kumuua, Marice akamwambia ngoja akapige simu polisi ili waje kumsaidia.
Kitendo cha kuwataja polisi kilimfanya Sarah kupandwa wazimu tena na kuanza kupiga kelele kisha akatoka ndani na kutimua mbio.
Marice alibaki kaduwaa ila alipiga simu polisi na kuwaeleza kilichotokea.
Alipokata simu akasikia mtu anagonga mlango, kumbe alikuwa agent wake Sarah akamuuliza Marice kama amebahatika kumuona mdada flani akikimbia kama kichaa eneo hilo.
Marice akahisi labda huyo ndiye anayetaka kumdhuru Sarah akamuuliza kwani wewe nani, akamwambia mimi ni rafiki yake.
Marice akamjibu alikuja hapa nikampokea ila alipoona napiga simu polisi akakimbia.
Yule agent akamwambia kwanini umepiga simu polisi utatuletea matatizo wakija kwa maana yule dada anajiuza na kisheria hairuhusuwi tutapewa adhabu ya kifungo, kisha akaondoa gari haraka polisi wasije wakamkuta eneo hilo.
Baada ya muda mfupi polisi walifija eneo hilo na Marice aliwapa maelezo ya kilichotokea nao walianza fuatilia tukio mpaka wakafika kwenye nyumba ya wale wakorea, ambapo nao walihojiwa na kutoa maelezo yao ya nini kilichojiri.
Polisi walizunguka eneo lote wakimtafuta Sarah bila mafanikio, walimtafuta usiku kucha pasipo mafanikio na Sarah hakuonekana tena.
Yani alipotelea hewani katika mazingira ya kutatanisha.

Itaendelea....
Story hii ni ya kweli ila baadhi ya majina ya wahusika nimeyabadili.
Kuna details sijaweka kwasababu sijaifanyia proof reading ila nikitudi iendeleza nitaiedit niweke taarifq vizuri.
Hiki kisa kitakuja kuibua mauaji ya kushangaza sana ambapo mpaka leo siyo polisi wala FBI ambaye wamefanikiwa kujua nani alikuwa akifanya mauaji hayo ya wanawake ambao wengi wao walikuwa na tabia zinashabihiana.

INAENDELEA
MTANISAMEHE NIMEKOSA MUDA WA KUFANYA PROOF READING NA KUFANYA EDITING

Kesho yake msako uliendelea ili kumpata Sarah, nyayo zilionyesha kuwa aliekekea upande wa nyuma wa makazi ya eneo ambalo alikuwa akiishi Malice.
Mita chache kutoka makazi hayo kulikuwa na vichaka vyenye miba na ukiingia ndani zaidi lilikuwa ni eneo lililojaa maji yani tinga tinga hivyo alama za nyayo za Sarah zilipotea.
Polisi waliomba msaada zaidi wa drones, na askari zaidi ili waweze kuzunguka na kumtafuta Sarah katika eneo lote hilo lenye tinga tinga.
Zoezi lilikuwa gumu sana ukizingatia eneo lina vichaka vyenye miba na tinga tinga, lakini polisi hawakukata tamaa walizidi mtafta Saraha.
Siku ya kwanza iliisha bila kumpata Saraha wala kuona dalili ya wapi anaweza kuwa amepita.
Yani ilikuwa kama vile kapotea tu kama Eliyah alivyo paishwa kwenda mbinguni.
Siku ya pilia waliamua waongeze mida za mraba zaidi za kumtafuta, zoezi likaendelea na katika kutafuta ndipo wakapata maiti ya mdada iliyokuwa imetupwa ndani ya hilo tinga tinga, katika kujaribu kukusanya ushahidi zaidi wakakutana na maiti nyingine eneo karibu na hapo walipokuta maiti ya kwanza.
Wakiwa wamestaajabu ya kuwa msako mmoja umeleta mwingine, maana hawakuwa wanajua hizo maiti ni nani na zimefikaji hapo wakagundua kuna maiti nyingine tena maeneo yale yale.
Lakini kwa hali ya maiti zilivyokuwa, walijua hakuna maiti ya Sarah kati ya hizo maiti maana zilionyesha zimekuwepo pale kwa muda mrefu.
Siku ikaisha kwa kupeleka hizo maiti kufanyiwa vipimo ili kubaini ni maiti za akina nani na chanzo cha vifo vyao.
Polisi hawakukataa tamaa na ndani ya siku chache mbele walipokiwa wakiendelea na msako wa kuntafuta Sarah kwenye hilo tinga tinga, walizidi kupata maiti zaidi na zaidi mpaka zikafika maiti nane.
Lakini kati ya maiti hizo Sarah hakuwa mmoja wa maiti hizo ila zote zilikuwa maiti za wanawake wenye umri kati ya miaka 20-35.
Na maiti sita ziliweza kutambuliwa na hao wote waliotambuliwa walikiwa Malaya wanaojiuza kama Sarah, walikuwa wengine wametokea miji mingine, pia wote walikuwa na historia ya kutumia madawa.
Na wote walikuwa wameuawa kwa kunyongwa kwa kamba kisha kufungwa kwenye mifuko ya nailoni na kutupwa eneo lile.
Hii iliwashutua sana polisi na wakahisi kuna muaji anayefanya mauaji endelevu akiwa ana walenga mabinti wa aina flani (serial killer).
Harakati za kumtafuta Sarah ziliendelea bila mafanikio, lakini polisi walifanikiwa kupata maiti nyingine sita eneo la mbali kidogo kutoka pale ambapo jumla zilitimia idadi ya maiti 14.
Lakini kati ya maiti hizi 6, polisi waligundua kuna uwezekano ya kuwa ni muaji tofauti na yule wa maiti zile nane.
Kwanza kati ya maiti hizo 6, kulikuwa na mtoto, na maiti moja mhanga alikuwa wa jinsia ya kiume pia kulikuwa na maiti ya binti mjamzito.
Na hizi maiti zilikuwa zinaonyesha muaji aliwaua kwa kuwapiga risasi hao watu tofauti na kundi za maiti zile nane za kwanza.
Polisi walizidi kuchanganyikiwa, kwa maana maiti za watu wengi walizookota, hawakuwahi pokea taarifa juu ya kupotea kwao.
Pili je kuna wauaji wawili tofauti au ni mtu mmoja japo staili zake za kuua zinatofautiana.
Na vipi je huyu mtu atakuwa ni nani?
Hayo maswali yaliwaumiza polisi vichwa, ikabidi wawahusishe FBI ili wawatengeneze wasifu wa muuaji au hap wauaji (killer profile).
Labda nielezee kidogo kuhusu huu wasifu. Kutokana na maelezo yanatotolewa na polisi na mazingira ya mauaji yanavyokuwa, FBI uwa wanaweza kujua huyo aliyetenda mauaji hayo atakuwa na wasifu gani na mara nyingi uwa ndivyo inakuwa.
Wanaweza wakasema mfano, huyu muaji atakuwa ni mtu anayefanya kazi bucha, atakuwa mtu mweupe mwenye miamsuri, umri wake ni kuanzia miaka 30-40.
Atakuwa mtu mpole sana anayeishi maisha ya aina mbili tofauti, akiwa na watu anaonekana mpole ana familia na ni mtu wa familia ila akiwa peke yake ni muaji hatari.
Hii FBI hutengeneza kwa kuzingatia mazingira ya huyo mtu anayefanya mauaji ameyafanya kwa kutumia siraha gani, na katika mazingira gani, wahanga wake ni watu wa aina gani.
Mfano hapo niliposema muaji atakuwa anafanya kazi bucha, hii inaweza kuwa ni pale wanapoona wahanga, wamekatwa katwa na panga au visu kwa staili inayoonyesha huyu mkataji anatumia panga au visu kwa ustadi.
Muuza bucha na mchijaji wanyama ukataji wake ni wa ustadi zaidi kuliko mtu wa kawaida.

Baada ya kutoa huo mfano basi tuendelee.
FBI, nao walikubariana na polisi ya kwamba wauaju hao watakuwa watu wawili tofauti.
Muuaji wa kwanza, walimpa wasifu wa kwamba atakuwa mtu wa miaka kati 45-60, mwenye pesa zake na anayeendesha gari la kifahari.
Pia waliongeza kwamba kuna uwezekano mkubwa anatoka mji mwingine kuja kufanya mauaji yale na mara zote huwashawishi wahanga wake wasije na simu wanaopoenda kukutana naye, kwakuwa hii ilitokana na ukweli kwamba katika maiti zilizotambuliwa walipofuatilia waligundua mara ya mwisho hao watu kuonekana, wote waliwaaga wenzao kuwa wanaenda kukutana na mteja mmoja wa maana ambaye atawalipa vizuri, ila hapendi kufahamika na pia hapendi mtu aende na simu hivyo simu zao waliziacha hawakwenda nazo.
Hii habari ya kuokotwa kwa maiti ilisambaa zaidi baada ya kurushwa sana kwenye vyombo vya habari na watu walianza kuingiwa uoga hasa madadapoa maana ilionekana walengwaji wakubwa ni madadapoa.

Itaendelea.....

Inaendelea Sehemu ya 3

Heka heka za kumtafuta Sarah, na mhusika wa mauaji yake ziliendelea pasipo kuwepo taarifa ya maana iliyopatika kuweza kusaidia polisi wala FBI.
Hof ilikuwa imetanda baina ya wakazi wa Greenwood hasa hasa wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili yao kwakuwa ilionekana ya kuwa muuaji ama wauaji walikuwa wanarenga wanawake wanaofanya biashara hiyo.
Msako uliendelea katika eneo ambalo maiti za awali ziliokotwa ila polisi wakaongeza ukubwa wa eneo la kutafuta.
Pia jamii ilijitolea kusaidia polisi katika huo msako kwa kushiriki utafutaji wa chochote kinachoweza kusaidia kupatikana kwa Sarah au ushahidi unaoweza kusaidia polisi kujua mtendaji wa mauaji yale.
Kiuhalisia, polisi walijua wazi wazi ya kwamba mauaji ya watu wale hayakuwa yamefanyika mahali pale, ila yalifanyika sehemu nyingine na pale maiti zililetwa kama sehemu ya kuzitupa.
Wakati msako ukiendelea kuna taarifa ilipatikana kuwa kuna maiti ya msichana imeonekana ikiwa imetupwa kando kando ya mto.
Polisi walifika eneo la tukio, na kukuta maiti ya msichana mwenye umri unaokadiliwa kuwa miaka 25-32, na dalili zilionyesha ameuawa kwa kukabwa, pia alikuwa sehemu ya chini hana nguo jambo lililowafanya polisi wahisi huenda alibakwa kabla ya kuawa na kuja kutupwa pale.
Lakini zaidi ya maiti hakukuwa na kitu kingine cha kuweza kuwasaidia kujua muuaji anaweza kuwa nani.
Hili liliwafanya polisi kuhisi huenda labda wakati huu wataweza kipata DNA ya muaji kama atakuwa kambaka na kuacha mbegu zake.
Maiti ilipelekwa hospitali ifanyiwe vipimo vya kimaabara ili wapate riporti ya kitabibu kuhusu chanzo cha kifo chake na kama kweli kabakwa.
Lakini jambo lililowaimiza kichwa ni swali walilokuwa wanajiuliza je mauaji hayo yana uhusiano wowote na zile maiti walizookota. Na je muuaji wa huyu binti ndiye muaji wa nayemtafuta?
Hiyo habari baada ya kusambaa juu ya kupatikana kwa maiti hiyo, watu walihisi huenda ni maiti ya Sarah lakini ripoti kutoka polisi zilikana kuwa si Sarah, hata wazazi wa Sarah walikama kuwa siyo Sarah baada ya kuonyeshwa picha ya sura ya maiti hiyo.
Jambo hilo lilizidi kuwachanganya watu je Sarah yuko wapi na amewezaje kupotea katika mazingira ya kutatanisha, na kama amekufa maiti yake mbona haionekani.
Baada ya ule mwili kufanyiwa vipimo ripoti ya kitabibu ilithibitisha kuwa kweli yule mwanamke ameuawa kwa kukabwa, ila hakubakwa na wala hakuna mbegu za kiume kwenye sehemu zake za siri.
Hii iliwafanya polisi warudi mezani kukuna vichwa maana walitegemea labda wangepata jambo la kuwasaidia kumtambua muaji wa yule dada ambaye walihisi ana uhusiano na mauaji ya wale watu wengine.
Siku ya nane toka Sarah apotee msako ukiwa unaendelea kwenye vile vichaka, kundi moja wapo la waliokuwa katika msako waliona mwili ukiwa katikati ya vichaka, walipousogelea walikuta ni mwili wa mdada, hivyo waliita polisi waliokuwa karibu wakifanya msako.
Baada ya kufika hawakuwa na shaka kuwa ule mwili ulikuwa wa Sarah kutokana na maelezo ya jinsi alivyokuwa amevaa, waliyopewa na Malice na wale wakorea ambao ni watu wa mwisho kumuona kabla ya kupotea, hivyo mwili ule ulikuwa na nguo ambazo waliambiwa Sarah alikuwa kavaa.
Katika uchunguzi wa awali kabla ya mwili kutolewa eneo la tukio, hawakuweza kujua nini kimemuua Sarah.
Pia hakukuwa na kitu chochote cha kuwasaidia ama kuonyesha ya kwamba kuna mauaji yamefanyika pale, hivyo waliamua mwili ukafanyiwe uchinguzi labda ripoti ya kitabibu itaweza saidia kutoa majibu.
Pia waliwataarifu ndugu zake waende kuutambua mwili huo japo ulikuwa umeshaharibika kwa kiasi flani.
Baada ya uchunguzi ripoti ya Daktari ilisema kuwa Sarah hakuuawa, ila kulikuwa na kiasi kikubwa cha pombe mwilini mwake kuliko kiasi kinachokubalika, pia ilidai kwamba alikuwa katumia kiasi kikubwa cha dawa za kulevya, hivyo akadai kifo chake kinaweza kuwa kimesababisha na kuumia wakati anakimbia mle vichakani alaishiwa nguvu kwa sababu ya vilevi alivyokuwa katumia kwa kiasi kikubwa.
Ndugu na watu wengi walikataa hiyo ripoti kuwa haiwezekani Sarah awe kafa tu bila kuawa na mtu.
Na je kwanini Sarah alikuwa anasema kuna mtu anataka kumuua? Mama yake alienda zaidi mbele na kusena kuwa mwanaye kama kunywa pombe na kutumia dawa kaanza zamani lakini hajawahi poteza akili aanze kukimbia bila sababu.
Kutokana na ripoti ya daktari, polisi walikubariana nayo swali na utata ukabako kwa maiti zile nyingine.

Nitarudi baadae kuhitimisha hii stori kwa kuweka picha na majina sahihi ya wahusika ili wanaosema nineitoa global wajue global kama wametumia mpaka majina niliyotumia mimi bas ndiyo wameitoa hapa na wakaiga na majina ambayo nimeyabadili makusudi.
Pia sehemu ya mwisho nitamalizia kwa kuwawekea picha ya mtu ambaye alishushiwa zigo la mauaji hayo japo watu wengi hata polisi wenyewe bado wanahisi siyo yeye aliyetekeleza mauaji hayo yote....
Na baada ya hapo nitaanza stori nyingine ya kweli yenye jina la MUAJI ALIYEAMINIWA NA MZAZI WA ALIYEUAWA

SEHEMU YA MWISHO

Ilikuwa mwaka 2015 mwezi wa saba, Claytor mwanamama aliyekuwa na umri wa miaka 38, alitoka katika tafrija usiku wa manane.
Akiwa kasimama kwenye kituo cha mafuta yeye pamoja na rafiki yake, mara gari lilikuja na kusimana karibu yake na ndani ya gari kulikuwa na mwanaume ajulikanaye kama Jason McCary.
Jason alianza kuongea na Claytor wakakubariana wakafanye mapenzi kwa malipo. Claytor alipanda gari na wakaondoka naye na ndiyo ilikuwa mara ya mwisho Claytor kuonekana mpaka mwili wake ulipokuja patikana umeterekexwa jumba bovu ukiwa umepigwa risasi tatu za kichwa.
Polisi walianza upepelezi mara moja na Jason na rafiki yake Ernest wakakamatwa na kuhojiwa pamoja na ushahidi uliopatikana, ikagundulika Jason alimtwamga risasi tatu Claytor baada ya Claytor kuvuta dawa aina ya cocaine alizokuta kwenye gari za Jason.
Jason alipata hasira wakaanza bishana akimtuhumu kwanini Claytor amevuta dawa zake alizokuwa anategemea kuvuta yeye siku hiyo maana hakuwa na dawa za ziada.
Mabishano hayo yalisabisha Jason kumtwanga risasi Claytor na kisha maiti yake kuitupa kwenye jumba bovu mpaka ilipokuja onekana.
Jason mahakama ilimkuta na hatia akahukumu kifungo cha maisha.
Lakini Jason anadai yeye siyo ambaye alimuua Claytor, bali andai ni mwanaume ajulikanaye kama Ernest Moore.
Kwa maelezo ya Jason anadai baada ya kumchukua Claytor alienda naye kwenye kituo kingine cha mafuta kisha kupaki gari sehemu ya parking, ambapo alifanya naye mapenzi.
Alipomaliza akagundua Claytor alikuwa katika siku zake hivyo alimuacha kwenye gari akaenda kujisafisha.
Alipokuwa anatoka sehemu zenye vyoo wakati anarudi kwenye gari alimuona Ernest akimpiga risasi Claytor kutokea siti za nyumba za gari lake. Anadai kuwa aliogopa akakimbia kurudi ndani na huku Ernest alitoka kwenye gari akapanda gari lingine na kuondoka eneo la tukio.
Kwa maelezo yake anadai Ernest alimuua Claytor kwakuwa siku za nyuma alimchukua kwa ajili ya kufanya mapenzi ambapo Claytor aliiba vitu nyumbani kwa Ernest, hivyo Ernest alikuwa anamtafuta ili amfunze adabu.
Baada ya kuona Ernest kaondoka anadai alirudi akaenda kutupa mwili kwenye jumba bovu kisha kusafisha gari kuondoa ushahidi maana alijua akitoa ripoti polisi hakuna atakaye muamini.
Mahakama haikukubari utetezi wake, na hukumu ya maisha ilikuwa juu yake. Pia polisi walijaribu kutaka kuonyesha kwamba yeye ndiye muaji wa wale madadapoa wengibe lakini hakushitakiwa kwa mauaji ya wengine kwasababu hapakuwa na ushahidi juu yake.
Mpaka leo haijulikani nani hasa alitenda mauaji hayo ya hao akina dada wengine, upelelezi bado unaendelea huku watu wengine wakiwa bado na hofu kuwa labda muaji katulia akisubiri watu wasahau afanye yake.

Nashukuru sana kwa wote mliofuatilua kisa hiki na hapa chini ni baadhi ya vitu ambavyo kwenye stori nilibadili makusudi hapa naweka usahihi wake.

Eneo haya matukio yalikotokea ni Chillicothe, Columbus, United States na siyo Greenwood Indiana.
Baadhi ya miili ilitambuliwa kuwa ya watu hawa
Trego, Lemons, Temeka, Lynch, Shasta Himerlock, Tifanny Sayre na Timberly Claytor.

Story inayofuata ni MUAJI ALIYEAMINIWA NA MZAZI WA ALIYEUAWA.

993bbc0d69425f8971194c77b2677a54.jpg

Jason
022bda26cfeb0d7af102c3a19a27e79e.jpg

Tifanny
afc83c1eff1a1da9a75b9feae44b944f.jpg

Claytor
 
Story ni nzuri ila jaribu kuirefusha zaidi kabla hujapumzika manake nimesoma nikiwa nimesimama sasa ilipoanza kunoga nikaona nikae...heee....mara itaendelea..
 
That's why movie industry has been coming up with something called "Series". Lets wait muendelezo
 
Story ni nzuri ila jaribu kuirefusha zaidi kabla hujapumzika manake nimesoma nikiwa nimesimama sasa ilipoanza kunoga nikaona nikae...heee....mara itaendelea..
[emoji23][emoji23][emoji23]

nYaNi wA KaLe
 
hao polisi huenda walikuwa vilaza!
walishindwa hata kuweka polisi wa kufatilia hayo maeneo ili wajue anekuja kuuwa/kutupa hiyo miili!
ngoja nisubiri hatima huenda mimi ndo kilaza...
 
Usipime upepo mzee...tupe mwendelezo na tag me
 
Mkuu kwahiyo umegoma kuendeleza hii hadithi..

Alafu tinga tinga ndio nini?
 
Back
Top Bottom