Kachanganyikiwa sababu ya utumbo wa mbuzi.

Kachanganyikiwa sababu ya utumbo wa mbuzi.

ninajiuliza utumbo wa mbuzi unaliwa,,,tangu nilipoiona hii thread lakini sipati jibu au mtoa mada alikuwa na maana nyengine???????????
Ndio utumbo wa mbuzi unaliwa...! Uko Emirates hamli nyama ya mbuzi?
 
Mama, kwani nakuzuga vipi tena,wenzetu hawana kawaida ya kuficha yaliyo mioyoni mwao,akipenda kitu anakueleza hapohapo na ukweli ni kuwa sikuwa nimemtongoza ila nilikuwa na mpango huo.

Na wakichukia ni kuachana hakuna kuombana msamaha. Lakini hebu tuambie, uko tayari kwenda kuwa mme mpishi, maana ndicho alichokupendea!? Sijui maisha yenu ya uzungu, ila mimi dah!
 
Sasa wandugu naombeni ushauri nikubali kutambulishwa au huo ndio utakuwa mwanzo wa kugeuzwa hausi boi.

Houseboy au housegirl...................................................ufafanuzi kwanza please...........................
 
Mkuu naomba upate nyingine kwa bili yangu,umenifurahisha sana maana hilo la bahati nilikuwa sijaliangalia.


Halafu ngosha kumbe wewe na wachina ni shareholder? nilikuwa sijui hilo lkn sasa nimeliona mkuu
 
Halafu ngosha kumbe wewe na wachina ni shareholder? nilikuwa sijui hilo lkn sasa nimeliona mkuu





Wachina tena...!? Hivyo vidude navyovichukia hata nikivikuta vinapigana na nyoka, mimi nitamsaidia nyoka aviume vizuri.
 
Dunia haiishi vya kushangaza,mwenzenu jana nimepata mgeni mtoto wa kijerumani,na kwa kuwa tulipanga anitembelee nikamwambia nitakupikia chakula cha kiafrika.Na kweli mtoto wa kiume nikapitia kwa mchina nikachukua utumbo wa mbuzi na ndizi matoke.Nikaandaa utumbo kwa ufundi wangu wote, nikaweka vitunguu swaumu,tangawizi,limao,pilipili mbuzi kwa mbali,kitunguu maji,nyanya ya kopo,pilipili hoho na mazagazaga kibao ya kiafrika.Mgeni wangu alipofika nikamkaribisha na alifurahia akasema tangu azaliwe hajawahi kula chakula kitamu kama hicho na ameniomba akanitambulishe kwa wazazi wake kama mchumba mwenye sifa ya upishi.Sasa wandugu naombeni ushauri nikubali kutambulishwa au huo ndio utakuwa mwanzo wa kugeuzwa hausi boi.

Kwa mjerumani hata usingekua unasifa ya kupika, kua house boy kwao ujue ni lazima, labda usiende kuishi kwao, muishi hukuhuku napo kama atakubali hiyo ndo kasheshe ingine.
 
Kwa mjerumani hata usingekua unasifa ya kupika, kua house boy kwao ujue ni lazima, labda usiende kuishi kwao, muishi hukuhuku napo kama atakubali hiyo ndo kasheshe ingine.




Ndio ninachokupendea mama,wewe huwa unajitokeza wakati sina pa kukimbilia na unanipa msaada mzuri sana kimawazo.Nitaomba basi angalau uwe unanisaidia na kimwili.
 
nyama twala mpenz lakini sijawahi kusikia wala kuona kama utumbo wake waliwa na ule uchafu wa tumboni???? na si wanuka???? au waniambia masghara tuu?
Ndio utumbo wa mbuzi unaliwa...! Uko Emirates hamli nyama ya mbuzi?
 
Back
Top Bottom