Elections 2010 Kada CCM aanzisha chama

Elections 2010 Kada CCM aanzisha chama

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,788
Reaction score
5,217
ALIYEKUWA kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paschal Kahangala, amejiengua katika chama hicho na kuanzisha Chama cha Ukombozi na Maendeleo (Chauma).

Kahangala ambaye alipata kuwania ubunge katika jimbo la Nyamagana, lakini alienguliwa katika kura za maoni za chama hicho, alisema amefikia uamuzi huo kwa kuwa amechoshwa na siasa za kibepari.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Kahangala Chauma kipo katika hatua za mwisho za usajili na kuwahamasisha Watanzania kukiunga mkono ili kiweze kuleta mabadiliko ya ukombozi nchini.

"Nimejivua gamba kwa kwa kuanzisha chama ambacho kauli mbiu ni kuboresha maisha ya Watanzania na kurudisha ujamaa na kujitegemea," alisema Kahangala.
 
Usalama wa taifa wapo kwa ajili ya mambo kama haya na si vinginevyo
 
Sikio la kufa katu halisikii dawa kabisa. Hapa bado hata mwaka mmoja baada ya uchaguzi haujatimia ndo CCM vituko kila kukicha, mara ufisadi, ubadilifu, kundana, kunyoosheana vidole, kupindisha sheria, kulalamikia maandamano ni uhaini, mara udini, ukabila nk

Baada ya dalili CCJ kuonekana wazi kuendelea kufurukuta ndani ya CCM kwa hoja ya wanaojipambanua kama wapiganaji na watetezi wa uadilifu ndani ya CCM na na serikali, sasa huyu kada naye anakuja na mpya kuanzisha mkwara miwingine wa kuanzisha chama cha upinzani ukiwa mwendelezo wa full vituko ndani ya CCM.

Sitashangaa viongozi wa juu wa Serikali na CCM mapigo ya moyo kubadilika mara kwa mara.
 
Wananchi tuwe macho zaidi na hivi vyama uyoga za hivi sasa!!!!!!!!!!!!!

ALIYEKUWA kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paschal Kahangala, amejiengua katika chama hicho na kuanzisha Chama cha Ukombozi na Maendeleo (Chauma).

Kahangala ambaye alipata kuwania ubunge katika jimbo la Nyamagana, lakini alienguliwa katika kura za maoni za chama hicho, alisema amefikia uamuzi huo kwa kuwa amechoshwa na siasa za kibepari.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Kahangala Chauma kipo katika hatua za mwisho za usajili na kuwahamasisha Watanzania kukiunga mkono ili kiweze kuleta mabadiliko ya ukombozi nchini.
"Nimejivua gamba kwa kwa kuanzisha chama ambacho kauli mbiu ni kuboresha maisha ya Watanzania na kurudisha ujamaa na kujitegemea," alisema Kahangala.

[TD="bgcolor: #ffffff"]

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][/TD]
 
ALIYEKUWA kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paschal Kahangala, amejiengua katika chama hicho na kuanzisha Chama cha Ukombozi na Maendeleo (Chauma).

Kahangala ambaye alipata kuwania ubunge katika jimbo la Nyamagana, lakini alienguliwa katika kura za maoni za chama hicho, alisema amefikia uamuzi huo kwa kuwa amechoshwa na siasa za kibepari.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Kahangala Chauma kipo katika hatua za mwisho za usajili na kuwahamasisha Watanzania kukiunga mkono ili kiweze kuleta mabadiliko ya ukombozi nchini.

"Nimejivua gamba kwa kwa kuanzisha chama ambacho kauli mbiu ni kuboresha maisha ya Watanzania na kurudisha ujamaa na kujitegemea," alisema Kahangala.

Nani anahitaji huu ujinga?
 
Ujamaa na kujitegemea? This is a load of rubbish.ujamaa si ndo umetufikisha hapa? Ajipange upya.
 
anatafuta ruzuku sio?

inawezekana kabisa hajarizika na mfumo wa vyama vilivyopo katika maana ya utawala wa ndani na hata sera walizonazo watanzania mpeni nafasi ndiyo demokrasia, tusiwe na roho ya kwanini! Kana kwamba tunaona tunastahili zaidi siesiem na kyandema
 
ni kuua chama tawala au kuugawa upinzani? God knows and may be time will tell!
 
Lipi jipya toka kwa hao magamba! hao wametumana kusudi kupunguza kasi za mashine kali za mapinduzi akina docta na Lisuu na Mbowe na wote wanaowanyanyasa magamba. Hii ni kiini macho hatudanganyiki, Wapi na wapi wee bwana ujamaa na kujitegemea leo acha utani mzee, pumuzika tu mzee kwani umechoka na huna jipya zaidi ya kuendeleza magamba tu ambayo tumeshayachoka kwani yanatukwangua tukipishana nayo. Ushauri wa bure aachane na siasa akaanze biashara ya kuuza samaki ziwa victoria hilo ndo atakaloweza. Magamba hata mkitumia njia gani sasa imeshakula kwenu! Mwisho wenu huuooooooooooooo! unakuja.
 
Labda akusanye ndugu wa ukoo wake ndio wawe wanachama,sie wengine hivi tulivyonavyo vinatutosha.
 
Kama anaanzisha chama na hitikadi zilezile za kushangilia kijivua GAMBA wakati SUMU ni ileile basi tofauti yake itakuwa ni mfanano wake tu na alikotoka!
 
Mambo ya RA AU ?MI SIPENDI HUU UTITILI wa vyama kabisa!ni kuendelea kumaliza rasilimali za watanzania.maana hapo utamsikia tendwa na timu yake wako mikoani ati wanahakiki wanachama! Ndo mambo gani?
 
Back
Top Bottom