Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wananchi wametakiwa kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu mchakato wa kumpata Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulivyofanyika kwani taarifa hizo zinalenga kupotosha umma na kuvuruga mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro Kada wa Chama cha Mapinduzi Mkoani humo, Malick Malupu amesema mchakato wa kumpata mgombea wa kiti cha Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM ulizingatia misingi ya katiba ya chama, demokrasia ya ndani na maadili ya uongozi.
Kwa upande mwingine kada huyo amewaomba wakazi wa mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanashiriki kwa ukamilifu zoezi la uchaguzi mkuu ifikapo mwezi Oktoba ili kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba.