GE2025 Kada CCM, Malick Malupu: Mchakato wa kumpata mgombea wa Urais, CCM ulikuwa wa Kidemokrasia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wananchi wametakiwa kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu mchakato wa kumpata Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulivyofanyika kwani taarifa hizo zinalenga kupotosha umma na kuvuruga mshikamano wa kitaifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro Kada wa Chama cha Mapinduzi Mkoani humo, Malick Malupu amesema mchakato wa kumpata mgombea wa kiti cha Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM ulizingatia misingi ya katiba ya chama, demokrasia ya ndani na maadili ya uongozi.

Kwa upande mwingine kada huyo amewaomba wakazi wa mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanashiriki kwa ukamilifu zoezi la uchaguzi mkuu ifikapo mwezi Oktoba ili kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba.

Your browser is not able to display this video.
 
Huyu malupu enzi za mwenda zake alichukua form ya Urais CCM ashindane na Magu,TISS walimfukuza by foot kutoka Dodoma Hadi Morogoro,.bahati yake hawakumkata
 
Huyu malupu enzi za mwenda zake alichukua form ya Urais CCM ashindane na Magu,TISS walimfukuza by foot kutoka Dodoma Hadi Morogoro,.bahati yake hawakumkata
Malupu wa Kirumba mwaloni mwanafunzi wa mzumbe
 
Kaka yake alifariki kwa kisukari alikuwa mwenyekiti wa kata ya Kirumba?
 
Thibitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…