Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Jamaa kaona ya nini tena baada ya kukaa mahabusu kwa siku kadhaa kaona siasa ngumu kaamua akiche siasa
=============
Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi wa Chama Cha ACT - Wazalendo Mkoa wa Njombe Ally Mhagama (Saga Saga), ambaye pia alikuwa mgombea wa Udiwani wa Kata ya Mkongobaki Wilayani Ludewa, ameachiwa kwa dhamana baada ya kukaa Mahabusu siku 12 akihusishwa kuratibu maandamano wakati wa uchaguzi.
Akizungumza na Jambo TV, Mhagama amesema baada ya kuachiwa huru hawezi kuendelea kujihusisha na siasa kwa sasa ili kuepuka changamoto na usumbufu kwa jamii kama zilizotokea, akidai kuwa Siasa za sasa zimekuwa za uadui jambo ambalo ni kinyume na maana ya siasa za Vyama vingi.
"Mchango wangu katika taifa kupitia siasa umefika mwisho, nataka nitulie na familia yangu na nifanye mambo mengine sitaki ugomvi na serikali" amesema Ally Mhagama