Ikiwa imetimia siku ya tano tangu kutolewa kwa taarifa ya kupotea kwa Kada wa CCM ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chonchorio, Mkazi wa Jijini Mwanza aliyepotea katika mazingira ambayo yanadaiwa kuwa tata, familia yake imeendelea kuomba Serikali kuongeza bidii ya kumtafuta.
Mtu wa karibu wa familia hiyo amesema hadi sasa hawajui mpendwa wao alipo na taarifa ambazo wanapata kutoka Jeshi la Polisi ni kuwa uchunguzi unaendelea lakini hawajui hatua zilipofikia huku akisisitiza kuwa siku moja kabla ya tukio la kupotea, Chonchorio alionekana hayupo sawa ila akajua ni uchovu wa kazi.
Mtu huyo amesema “Upande wangu mimi na wenzangu kadhaa tunaofuatilia hatujapata nafasi ya kukutana na RPC kuzungumzia hiki kinachoendelea ila tunaonana na Viongozi wengine wa Polisi kila tunapoenda kufuatilia pale Kituo cha Polisi Central."
“Polisi waliuliza kama Chonchorio alikuwa na uhasama na mtu yeyote, sisi hatujui, maana taarifa zimekuwa nyingi inawezekana ni masuala ya Kisiasa au Biashara lakini bado hatuna uhakika wa nini hasa kilichopo nyuma ya pazia.”
Pia Soma:
Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Alipoulizwa kama aliona dalili zozote za Chonchorio kutokuwa sawa au ishara yoyote iliyoonesha hayupo sawa, amesema “Siku moja kabla ya kupotea nilimuona kama hayupo sawa, tukahisi inawezekana ni masuala yake ya kazi.
“Hakutuambia chochote, ila tulimuona tu hayupo sawa, tukamwambia ‘usijali kila kitu kitakuwa sawa’, tulihisi amechoka.”
Pia Soma:
PreGE2025 - Kutoonekana kwa Patrick Boisafi (Mwenyekiti wa CCM Mkoa)na Athari zake kwa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kuhusu simu ya Chonchorio, ameeleza kuwa mara ya mwisho ilionekana ikiwa maeneo hayo ambayo alikuwepo akifanya mazoezi, baada ya hapo ikazimwa, hawajui yuko wapi, wanachohitaji ni kujua alipo.
Amesema “Tunamuomba Rais Samia atusaidie na aelekeze zaidi bidii ifanyike katika Vyombo vya Usalama ili kujua wapi alipo Chonchorio, tunachohitaji ni kumuona akiwa hai, tumeshafanya jitihada mbalimbali za pembeni ikiwemo kumtafuta Waziri Bashungwa ambaye bado hajapokea simu.”
Ameeleza Chonchorio ni Baba wa Watoto sita, ni mume, ni kaka, ni mjomba na ni kichwa cha familia, kila mtu anamtazama yeye, wanaomba arudi hata kama kuna kitu huko basi hatua zichukuliwe yeye akiwa uraiani.
Tukio la kutoweka kwa Chonchorio inadaiwa lilitokea Jumapili asubuhi Machi 23, 2025 akiwa kwenye mazoezi, eneo la Nyakato, Mwanza.
Machi 25, 2025, dada wa kada huyo, Lucy Mrimi alizungumza na Wanahabari na kusema familia iko katika sintofahamu na vitu vingi vimesimama kutokana na kupotelewa na ndugu yao katika mazingira ya kutatanisha.
Chonchorio ambaye pia ni mfanyabiashara, mkazi wa Nyakato jijini Mwanza anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha Jumapili asubuhi.
Hivi karibuni kada huyo alitangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Machi 24, 2025, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Audax Majaliwa alithibitisha kupata taarifa za kupotea kwa kada huyo na kueleza Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu kutoweka kwake.
Pia soma
~ Polisi Mwanza yatangaza kuanza uchunguzi wa tukio la kutoweka kwa Daniel Nyamhanga, Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM
~ Familia ya Daniel Nyamhanga yamuomba Rais Samia kuwasaidia kupata, wasema ushahidi upo akichukuliwa na watu wasiojulikana
~ Mwanza: Familia ya kada CCM aliyetekwa yamuangukia Rais Samia