comrade_kipepe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2019
- 3,411
- 4,435
KWAMBA WASIOJULIKANA HAWACHAGUI WA KUWADHURU? AU TUNAJARIBU KUBALANCE MAMBO DAKIKA ZA JIOOOOOOOOONI, KUELEKEA SEPTEMBER 23
——
Watu wasiojulikana wanadaiwa kumvamia na kummwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali, kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Idrissa Makishe.
Kada huyo mkazi wa Njoro wilayani Moshi amepata majeraha usoni na mikononi na amelazwa katika Hospitali ya Mawenzi.
Msemaji wa hospitali hiyo, Venna Karia, amesema Septemba 20, saa 3.00 usiku walimpokea mgonjwa huyo anayeendelea na matibabu.
"Septemba 20 tulimpokea mgonjwa anayeitwa Idrissa Makishe akiwa amejeruhiwa usoni na mikononi. Inaonekana alimwagiwa kimimimika kisichojulikana ni cha aina gani ambacho kilimsababishia majeraha hayo," amesema.
Alipotafutwa kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana.