Kada wa CCM amwagiwa tindikali

Kada wa CCM amwagiwa tindikali

KWAMBA WASIOJULIKANA HAWACHAGUI WA KUWADHURU? AU TUNAJARIBU KUBALANCE MAMBO DAKIKA ZA JIOOOOOOOOONI, KUELEKEA SEPTEMBER 23
——
Watu wasiojulikana wanadaiwa kumvamia na kummwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali, kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Idrissa Makishe.

Kada huyo mkazi wa Njoro wilayani Moshi amepata majeraha usoni na mikononi na amelazwa katika Hospitali ya Mawenzi.

Msemaji wa hospitali hiyo, Venna Karia, amesema Septemba 20, saa 3.00 usiku walimpokea mgonjwa huyo anayeendelea na matibabu.

"Septemba 20 tulimpokea mgonjwa anayeitwa Idrissa Makishe akiwa amejeruhiwa usoni na mikononi. Inaonekana alimwagiwa kimimimika kisichojulikana ni cha aina gani ambacho kilimsababishia majeraha hayo," amesema.

Alipotafutwa kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana.
Wamejimwagia kimiminika kinachosadikika kuwa Mtindi mkali ili ionekane GG. hahahaha, 2days to go.
 
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Idrissa Makishe, anayedaiwa kumwagiwa kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni tindikali, amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) kwa matibabu zaidi ya kibingwa.

Kada huyo ambaye ni mkazi wa Njoro, Manispaa ya Moshi na dereva bodaboda, alikutwa na madhila hayo usiku wa Septemba 20, 2024 baada ya mtu mmoja kumkodi akitaka ampeleke eneo la Njoro lililopo wilayani humo.

Inaelezwa kuwa baada ya kufika eneo hilo, mtu huyo aliyemkodi alimtaka asimame ampakie mwenzake ambaye alikutwa eneo la tukio akia amebeba chupa ya maji na nyundo, ndipo zikaanza purukushani hizo na baadaye alimwagiwa kimimimika hicho kilichomsababishia majeraha usoni na mikononi.

Ushahidi Kada wa CCM anayedaiwa kumwagiwa tindikali ahamishiwa KCMC
 
Kugombania buku 7 za Lumumba. Woiiiiih
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Idrissa Makishe, anayedaiwa kumwagiwa kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni tindikali, amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) kwa matibabu zaidi ya kibingwa.

Kada huyo ambaye ni mkazi wa Njoro, Manispaa ya Moshi na dereva bodaboda, alikutwa na madhila hayo usiku wa Septemba 20, 2024 baada ya mtu mmoja kumkodi akitaka ampeleke eneo la Njoro lililopo wilayani humo.

Inaelezwa kuwa baada ya kufika eneo hilo, mtu huyo aliyemkodi alimtaka asimame ampakie mwenzake ambaye alikutwa eneo la tukio akia amebeba chupa ya maji na nyundo, ndipo zikaanza purukushani hizo na baadaye alimwagiwa kimimimika hicho kilichomsababishia majeraha usoni na mikononi.

Ushahidi Kada wa CCM anayedaiwa kumwagiwa tindikali ahamishiwa KCMC
Basi vyama vyote viandamane kukemea hili jambo (ccm na chadema)
 
KWAMBA WASIOJULIKANA HAWACHAGUI WA KUWADHURU? AU TUNAJARIBU KUBALANCE MAMBO DAKIKA ZA JIOOOOOOOOONI, KUELEKEA SEPTEMBER 23
——
Watu wasiojulikana wanadaiwa kumvamia na kummwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali, kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Idrissa Makishe.

Kada huyo mkazi wa Njoro wilayani Moshi amepata majeraha usoni na mikononi na amelazwa katika Hospitali ya Mawenzi.

Msemaji wa hospitali hiyo, Venna Karia, amesema Septemba 20, saa 3.00 usiku walimpokea mgonjwa huyo anayeendelea na matibabu.

"Septemba 20 tulimpokea mgonjwa anayeitwa Idrissa Makishe akiwa amejeruhiwa usoni na mikononi. Inaonekana alimwagiwa kimimimika kisichojulikana ni cha aina gani ambacho kilimsababishia majeraha hayo," amesema.

Alipotafutwa kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana.

SI Bora yeye watoto wake na wazazi wanamuona,

Wakina Ben saanane hawajulikaniki wapi hai au laa.

Ila pole yake.

TUBUNI NA KUIAMINI INJILI YA YESU KRISTO.
Wahalifu wasakwe na waende mbele ya pilato.
 
Tindikali na risasi alizomiminiwa lisu ipi ni ukatili mkuu hao wanajitekenya wenyewe.
 
Back
Top Bottom