Kada wa CCM Kazungu atangaza kujiuzulu Siasa, akemea uchawa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CDE Bakari Kazungu, ametangaza rasmi kujiuzulu na kujiepusha na siasa za kukitetea chama hicho katika mitandao ya kijamii.

Kazungu, ambaye amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 2007 na kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi ya kata, wilaya, na mkoa, amebainisha kuwa amechukua hatua hiyo kufuatia changamoto na mateso aliyoyapitia.

Katika maelezo yake, Kazungu ameeleza kuwa amewasamehe wote waliohusika kumfanyia vitendo vilivyomsababishia maumivu, akisisitiza kuwa anaamini Mungu atayageuza mateso hayo kuwa neema katika maisha yake.

Ameeleza kuwa alijitoa kutetea CCM kwa mrengo na mfumo tofauti, tofauti na baadhi ya vijana wengine wanaotumia mbinu za kujipendekeza na "uchawa"—tabia ambazo amedai hazipaswi kuungwa mkono na viongozi wakuu wa kitaifa.

Kazungu amebainisha kuwa uamuzi wake wa kujiondoa kwenye siasa hizo unalenga kulinda afya, uzima, na uhai wake, na sasa anaelekeza nguvu zake zote kwenye taaluma yake ya uanahabari na utangazaji.

Kazungu amewashukuru viongozi wa CCM na wale wa vyama vya upinzani waliomwonyesha utu na ushirikiano wakati wa changamoto zake. Amesisitiza kuwa ingawa amejiondoa kwenye ulingo wa siasa za mitandaoni na kuwaachia fursa wanaoendeleza mrengo wa uchawa, ataendelea kubaki kuwa kada mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi


Your browser is not able to display this video.


Soma

 
Uwamuzi nzuri na Wakizalendo,CCM wote mlio Wazalendo kwa taifa lenu fuateni njia hii Bora ya kulikomboa taifa letu.
 
Kwa mpenda haki yeyote, CCM sio club sahihi. Kuwa sehemu yake is a wrong decision!
 
ok.🐒
 
Utakuwa wewe hata kama ni chawa mtukuka
ukitaka kunijibu jaribu kuwa na akili japo ya kuvukia barabara. Sijakutaja unajihisi bure ni kama jf ni ya mamako punda mzee wewe. Machawa wote wa ccm naomba mfanyiwe zaid ya huyo ili mpate akili maana akil zilirudi matacorn hadi huyo baada ya kukutana alichokutana nacho ndo akapata akili mara hiyo hiyo. Sasa nawewe jaribu kujielewa au ujaribu kupta kushoto uendelee na manna zako.
 
Kwa jicho la tatu, wana CCM wanajiondoa meli inayozama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…