Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Huyu ni Kada wa Chadema anaitwa Joseph Mwasote maarufu kama China, mkazi wa Tunduma mkoani Songwe. Anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana mwezi uliopita. Familia yake imehangaika kumtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio. Oktoba 29, 2025 mwanae aitwae Stephano akaamua kuandamana kama sehemu ya kudai haki ya baba yake. Akabeba bango lililoandikwa TUMECHOKA NA UTEKAJI, MRUDISHENI BABA YANGU.
Jioni akarudi nyumbani salama. Oktoba 30 akiwa nyumbani kabla hajatoka, watu waliovalia kiraia wakiwa na silaha wakamfuata nyumbani na kumpiga risasi, akafariki dunia. Hakua kwenye maandamano, aliuawa akiwa nyumbani.
Familia ikapeleka mwili kuhifadhi Hospital ya Tunduma, ili kujipanga na mazishi. Walipomaliza vikao vya familia wakaenda kufuata mwili hospitalini lakini hawakuupata. Hakuna taarifa za mwili huo ulichukuliwa na nani na umepelekwa wapi.
Familia hii inapitia kipindi kigumu sana. Imempoteza baba ambaye alitekwa na hajulikani alipo na imempoteza mtoto ambaye alipigwa risasi nyumbani. Mbaya zaidi maiti ya mtoto haijapatikana. Na hawajui kama baba yupo hai au nae ameuawa. Baba na mtoto wametoweka na hakuna hata mfupa wao ulioonekana. Jiweke kwenye viatu vya mama wa hii familia