Ushauri wa bure kwa kada za engineering zilizotajwa kwenye tangazo la Tamisemi.
Ombeni wadogo zangu, chonde chonde ombeni hiyo kazi, alaf huko mbele mtapigana kivingine, kuna option inaitwa Recategorization kwenye utumishi hiyo inakuwezesha kubadilishwa cheo kwenye utumishi na salary yako kubadilika.
Jambo lingine ni kwamba ukishapata Cheque number utaweza kuhama kwenda taasisi nyingine ya kiserikali kama vyuo vikuu kuwa Lecturer au engineer kama kawaida na hizo nafasi kwa sasa zipo nyingi tu za kuhamia taasisi zenye upungufu wa wataalam wa kada flani.
Mimi ni shuhuda, siwezi kusema hapa kwamba nilitoka wapi na sasa nipo wapi ila humu humu JF kuna watu tunafamiana vizuri na wao ni mashuhuda, nilianzia kazi kwenye kada ya mbali sana lakini nilipambana na saivi niko kwingine nafanya kazi ninayoipenda.
Msidanganywe na pass mark kwenye makaratasi mkavimba vichwa kwamba nyie ni wahandisi mnadharirishwa, hayo makaratasi hayajui maisha, nyie ndo mnajua hali halisi ya maisha, weka makaratasi kabatini ingia kupambana kitaeleweka tu.