Kada ya Udereva ni fani ya maana sana ofisi za Serikali

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Pamoja na kwamba wengi hufikiria dereva anadharaulika katika utumishi na kuchukuliwa Kama kibarua fulani lakini linapokuja suala la upataji wa posho madereva wako vizuri huenda kuliko watumishi wengine katika maofisi kwa sababu kila safari ya kazi ya kutoka nje ya kituo cha kazi lazima dereva ahusishwe.

Nazungumzia haswa zile ofisi ndogo za mikoa acha zile HQ za zone ambazo unakuta madereva wako watano au wanne ila hizi ofisi ndogo zilizo chini ya wizara yaani Serikali kuu unakuta gari moja na dereva mmoja na ndio hiyohiyo anayotumia boss na watumishi katika kazi hivyo dereva ana nafasi ya kutoka kila safari.

Hata ikitokea boss au mkuu wa kitengo kajiandikia dokezo peke yake kawatema wafanyakazi bado ni lazima dereva huyohuyo ndio ahusishwe na zikitokea activities za wafanyakazi bado tena anaula dereva huyohuyo.

Kingine majukumu yake mengi hayana lawama yaani means kwamba haulizwi kuhusu report za kazi na hata Kama ikitokea mmeharibu kazi yeye hausiki kazi yake ni kuwafikisha site Basi.

Hivyo ni wazi kwamba dereva ni fani nzuri tofauti na watu wanavyochukulia.
 
Imagine unakuwa dereva wa DED mwenye miguu ya kuku! Aisee mshahara utakuwa ni kwa ajili tu ya kusomeshea na kujengea.
Na wakati mwingine unakuta idara za halmashauri mfano wanaolipa hela za TASAF Wanaazima gari ofisini kwenu na wanamchukua dereva wa kwenu wanamlipa wao.nyie wafanyakazi sa hiyo mmenasa hamjapata night days Zaid ya mwezi.
 
Pamoja na kwamba wengi hufikiria dereva anadharaulika katika utumishi na kuchukuliwa Kama kibarua fulani lakini linapokuja suala la upataji wa posho madereva wako vizuri huenda kuliko watumishi wengine katika maofisi kwa sababu kila safari ya kazi ya kutoka nje ya kituo cha kazi lazima dereva ahusishwe.

Nazungumzia haswa zile ofisi ndogo za mikoa acha zile HQ za zone ambazo unakuta madereva wako watano au wanne ila hizi ofisi ndogo zilizo chini ya wizara yaani Serikali kuu unakuta gari moja na dereva mmoja na ndio hiyohiyo anayotumia boss na watumishi katika kazi hivyo dereva ana nafasi ya kutoka kila safari.

Hata ikitokea boss au mkuu wa kitengo kajiandikia dokezo peke yake kawatema wafanyakazi bado ni lazima dereva huyohuyo ndio ahusishwe na zikitokea activities za wafanyakazi bado tena anaula dereva huyohuyo.

Kingine majukumu yake mengi hayana lawama yaani means kwamba haulizwi kuhusu report za kazi na hata Kama ikitokea mmeharibu kazi yeye hausiki kazi yake ni kuwafikisha site Basi.

Hivyo ni wazi kwamba dereva ni fani nzuri tofauti na watu wanavyochukulia.
KWELI bana wewe umejibu kwa ufasaha zaidi jamani
 
Back
Top Bottom