Kadampinzani asema: MBOWE AHOJIWE!

Status
Not open for further replies.
DUH Kada..Kwa kasi hii basi kama ungekuwa nayo mwanzoni na kwa nia nzuri na nchi yetu...Then hata Ballali angeshahojiwa kabla ya kifo.
Sasa naona unataka Mbowe ahojiwe.
Kweli CCM kama ndiyo hivi basi tena.
Na hao mafisadi wengine kwenye listi ya Mwembe Yanga nao wamuhoji Mbowe ama wao ndio wahojiwe?
Wahojiwe na nyie makada wa CCM...Ama wahojiwe pia na makada wengine wa CCM weye nyadhifa kama kina Said Mwema?
Mbowe naye ahojiwe na nani?
Na unataka ahojiwe kabla ya wale wengine 10 waliobaki kwenye list of shame?
 
mzee mzima anaumbuka, yaani analipwa na mafisadi? inatisha

Na kinachoumiza zaidi ni kuwa analipwa visenti wakati wenzake wanachota mabilioni.

Usishangae hii hasira, chuki na wivu alionao kwa MBowe. Kinamuumiza sana akiona Mbowe na Chadema wakiwaumbua mabosi wake. Utaona mengi sana hapa JF. Hana kipya fisadi mkubwa kama huyu.
 
I luuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuv JF.

Watu wana data hadi inatisha. Mafisadi kina Kadampinzani na wenzake walidhani haya yote ni siri. Mimi ningewashauri tu wabaki na radio Tanzania na TVT kwa propaganda kwani hapa JF ufisadi haupiti.



huyu ndiye kinanda leo humu !
 
Ashaishiwa sasa...


Wana JF wenye uchungu na nchi yao 5... kadampinzani na mafisadi wa ccm 0
 
Yalishamshida sasa amekosa cha kuandika.

kwi kwi kwi kwi kwi.... ngoja ncheke mie!

Ngoja aendelee kujifunza inawezekana akarudia darasa la kwanza yaani na uzee wote unaabudu mafisadi. Mungu apishe mbali.
 
naona wengine mmesahau ze topic ! ni hii hapa !


Kadampinzani asema :MBOWE AHOJIWE !!

--------------------------------------------------------------------------------

Naam ni yule mwenyekiti chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Aikaeli Mbowe. Wiki iliyopita aliweza kutoa maneno makali ambayo kwa kweli ukiangalia kiundani kama unaipenda nchi yako basikamwe hutoweza kuacha hizo kauli ziende tu hivi hivi !

Mbowe ambae anakabiriwa na kesi ya kutolipa mamilioni ya shilingi aliyokopa NSSF aliyokopa kuendesha biashara yake, alisema kwamba vifo vya Marehemu Amina Chifupa na Ballali ambae alikuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania wameuliwa na CCM.

Sidhani kama kweli mtu ambae hakumaanisha anaweza kuongea mambo mazito kama haya. Hata kama tofauti za kisiasa mtu mwenye akili timamu hawezi kuongea maneno mazito kama haya halafu ategemee asihojiwe na vyombo vya dola. Kwa kweli nchi yangu ya Tanzania naipenda, na ndio maana nasema Mbowe ahojiwe ili aweze kutoa ushahidi wa kutosha na hao walioshiriki waweze kukamatwa na sheria ishike mkondo wake.

Bwana Mbowe alinukuliwa akisema, "Kuteketea kwa Ballali, tutaamini kuna mkono mchafu wa baadhi ya viongozi wa serikali, kwa sababu ni shahidi muhimu katika vita ya ufisadi. Wasifikiri kufa kwa Ballali, ndiyo mwisho wa mapambano, lakini nawaambia ndiyo kwanza vita ya ufisadi itapamba moto." hapo hapo pia aliendelea na kusema, "“Ufisadi na mchezo mchafu wa CCM, umewatesa watoto wetu, wazazi wetu na sasa basi, tutapambana hadi watakapouana wote waishe. Wamemuua Ballali, Amina Chifupa wataendelea kuuana,” . Hata hivyo Mbowe aliendea kuongea maneno hayo bilaya kutoa ushahidi wa kina ambao unaweza kuwafunga CCM na hao marehemu waliofariki.

- - - - - - - - - - - - - -MWISHO - - - - - - - - - - - - - - - -

Nini kinachotakiwa kifanyike:

(a) Kwa kuwa mbowe ana uhakika kwamba ccm imewaua hao watu, basi afikishwe kwenye vyombo vya dola na kuhojiwa ili kutoa ushahidi mzima.

(b) Kutokana na ushahidi atakaotoa, hao wafuatiliaji waweze kulinganisha na hali halisi ya matukio yaliyotokea ili kupata ukweli !

Naamini Mbowe atakuwa anajua zaidi ya hayo aliyosema, hivyo ahojiwe ili kupatikana ukweli !
 
Ngoja aendelee kujifunza inawezekana akarudia darasa la kwanza yaani na uzee wote unaabudu mafisadi. Mungu apishe mbali.

kwi kwi kwi..

Si unaona mwenyewe ameanza kutoa mifano ya darasa la kwanza.
Anatia huruma kama Kikwete na mafisadi wenzake huko ccm.

Utaona sasa anaanza kujaza hii thread kwa viroja na vimisemo vya ajabu maana hoja zimemwishia.

Tuhesabu kuanzia 10, ukifika 3 utaona viroja vimeanza.
 
kama mnafikiri kada ataondoka humu leo, basi mmenoa ! kama mpo tayari kaeni kabisa kwenye vistuli maana mwenzenu nishafunga mkanda kwa ajili ya safari ! na asikimbie tu mtu leo humu !

mtajigonga kwenye ukuta, mtajigonga tena hadi mjue ninachoongelea humu leo !
 
sasa kada nakuonea huruma sana naona usome vizuri signature ya mkuu MMKJJ

Subiri uone atakavyoanza kubandika picha za ajabu ajabu hapa na kutoa vimisemo vya ajabu kama kawaida yake kila mara akiishiwa hoja.
 
Subiri uone atakavyoanza kubandika picha za ajabu ajabu hapa na kutoa vimisemo vya ajabu kama kawaida yake kila mara akiishiwa hoja.

soma maneno yako hayo highlighted na hii picha chini ! hahaaaaa, i know, right !

 

Nani ategemee wewe kuondoka hapa? As longer as unazidi kujiabisha na kuonesha vile ulivyo na chuki dhidi ya MBowe, mimi ninaenjoy hii explosion unayoonyesha hapa.

Ulianza kwa kujisifia ... ohhh someni posts zangu za mwanzo, wapi..
haikuchukua hata saa moja kabla hujaonesha ufisadi wako...

Fisadi mkubwa, hata Mkapa amesema kama wewe kwa watanzania.
 

Nilijua maana kuna jamaa alisema unalipwa kwa post sasa nafikiri leo utapata overtime
 
soma maneno yako hayo highlighted na hii picha chini ! hahaaaaa, i know, right !


Nilichosema tayari kimetokea...

hoja zimeisha.. vimeanza viroja.....

Kuna mtu yuko obsessed na Mbowe kupita kiasi. Kuna mtu aliwahi kusema hapa JF kuwa Kada amejaza picha za mbowe kwenye chumba chake na kila sehemu.

Ukweli ni kuwa Kada anamuabudu Mbowe.
Haipiti siku kabla hajamsema au kumtaja jina lake.
 
Ukweli ni kwamba wanachama wa CHADEMA wana haki ya kujua kiongozi wao wa taifa aliposema CCM inaua watu alikuwa na kithibitisho au lah na wana haki ya kujua viongozi wa chama chao wana mpango gani juu ya hilo.

Wananchi wengine pia wana haki ya kujua ukweli wa maneno ya Mbowe kwa sababu kwa kauli aliyotoa kuna watu wengi hivi sasa wanaishi kwenye hofu.

Iwapo Mbowe hatatoa ufafanuzi na vithibiti vya kauli yake basi itathibitisha jinsi asivyokuwa makini na uongozi wa taifa.

Hakuna haja ya kungoja kuhojiwa na vyombo vya dola kwa sababu vyombo vya dola havitafanya hivyo bila kuwa na malalamiko toka CCM, ila yeye mwenyewe anapaswa kuona umuhimu wa kuthibitisha au angalau kufafanua usemi wake ili asiwe anaongea kama kijana wa kijiweni.
 
Nilijua maana kuna jamaa alisema unalipwa kwa post sasa nafikiri leo utapata overtime

Kwa sababu malipo yake ni kidogo ukilinganisha na kina Saliva Rweyemamu. Kada anajaribu kupost nyingi angalau afikie robo ya malipo ya kina Balile.
 

sasa picha ya mbowe ndio picha ya ajabu ajabu au ?? acha kujivika utume bepari mkubwa wewe ! watu tunaenjoy kuona dogos kama nyie mnadandia treni kwa mbele, sasa hili la leo unalo kijana ! na utajuta kwa nini umelidandia kwa mbele !
 
siku mbowe atakapokuja na kufafanua kauli yake hiyo aliyosema,(kitu ambacho kitacause sparkle) nitawatafuta hawa vidogoz wanaopiga kelele humu ndani wakati wazee wanachambua mamboz !
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…