Ukweli ni kwamba wanachama wa CHADEMA wana haki ya kujua kiongozi wao wa taifa aliposema CCM inaua watu alikuwa na kithibitisho au lah na wana haki ya kujua viongozi wa chama chao wana mpango gani juu ya hilo.
Wananchi wengine pia wana haki ya kujua ukweli wa maneno ya Mbowe kwa sababu kwa kauli aliyotoa kuna watu wengi hivi sasa wanaishi kwenye hofu.
Mafisadi ndio mna hofu na maneno ya Mbowe na wananchi wanafurahi kuwa angalau kuna mtu anawatetea.
Iwapo Mbowe hatatoa ufafanuzi na vithibiti vya kauli yake basi itathibitisha jinsi asivyokuwa makini na uongozi wa taifa.
Hii kauli ndiyo imethibitisha kuwa Mbowe anafaa kuwa kiongozi wa kitaifa kwa vile amewapata mafisadi kama nyie mkichanganiyikiwa.
Hakuna haja ya kungoja kuhojiwa na vyombo vya dola kwa sababu vyombo vya dola havitafanya hivyo bila kuwa na malalamiko toka CCM, ila yeye mwenyewe anapaswa kuona umuhimu wa kuthibitisha au angalau kufafanua usemi wake ili asiwe anaongea kama kijana wa kijiweni.
Kama mna ubavu, mfungulieni Mbowe mashitaka.