Kadampinzani asema: MBOWE AHOJIWE!

Kadampinzani asema: MBOWE AHOJIWE!

Status
Not open for further replies.
i think there is a point that is trying to come out here. Wengine huku tumekata tamaa na hawa mafioso, lakini kama kweli watu wanajua hao wanaocoperate katika kutoa ushahidi, nafikiri hilo ni jambo jema
 
Serikali nayo haina cha kujibu ama cha kuhojiwa.....?

Kauli za serikali kuhusiana na EPA VS Ballali:

1)haitajiki..Tukimuhitaji tutampata.
2)Tunajua aliko.
3)Hatujui aliko
4)Tunamtafuta.
5)Ni mgonjwa.
6)Ana afya..Ni mzima.
7)Ni mgonjwa..amelazwa
Ni huru.
9)Si shahidi
10)Si mtuhumiwa.

NB:Mustafa Mkullo.."Nilienda Washington nikamtafuta sikumpata"
Mh J.Kikwete.."Kifo cha Ballali ni mapenzi ya Mungu"

Ni wakati wa serikali kutoa tamko lao wakati huu ili sisi wananchi tujue moja.

Ni muhimu sana kwa serikali kufanya hivyo kwasababu sasa Ballali ameshakufa na kuna minon'gono kuwa ni serikali yenyewe imeamua kumwua Ballali ili asitajwe tena kwenye kesi ya EPA wala ushahidi wake usitumike.

Na ili pia tukubali kuwa kifo chake ni mapenzi ya Mungu kama vile Mh rais anavyotaka tuamini..

Then maswali ya wananchi kuhusiana na kuhusika ama kutohuisika kwa Ballali yajibiwe ili tuweze kujua mustakabali wa shauri hili tata la EPA.

Tunajua pia kuwa Mh Rais alisema kuwa kamati haiwezi kutaja siri nyingine ili kuepusha uchunguzi usiharibike..Lakini ni wazi kuwa kutaja mashahidi ama watuhumiwa hakuharibu ushahidi bali kutaja waliyosema ndio kunaweza kuwa matatizo.

Serikali haijawahi kusema kama Ballali ni shahidi ama mtuhumiwa na sikumbuki kama wameshawahi kuwataja watuhumiwa ama mashahidi!

Kuwataja watuhumiwa ama mashahidi ni haki ya Mtanzania na serikali inawezekana iliwahoji kina Ballali na wenzake kwa kigezo kile walichokitumia kuwa wananchi wapeleke taarifa.

Serikali pia inaweza kudai kuwa kamati ilikuwa ni ya uchunguzi tu na mshahidi na watuhumiwa watatajwa mara baada ya kesi kufunguliwa rasmi mahakamani! Kwangu madai hayo yatashinikiza fikra kuwa serikali imefanya usanii kwa watanzania!

Ni wazi serikali inaweza kusema kuwa Ballali kama raia wengine naye alipeleka taarifa zake kwa kamati hiyo ya rais.

Na kama imefanya hivyo..Then tunaomba ripoti ili tuweze kujua kuwa nani alikuwa kama shahidi na nani kama mtuhumiwa,pia ni kesi gani watakayoifungua dhidi ya hao watuhumiwa ambao bado haijaamua kuwatangaza ama kuwahoji licha ya kwamba Dk Slaa alikwisha fanya hivyo pale mwembe Yanga.
 
Serikali nayo haina cha kujibu ama cha kuhojiwa.....?

Kauli za serikali kuhusiana na EPA VS Ballali:

1)haitajiki..Tukimuhitaji tutampata.
2)Tunajua aliko.
3)Hatujui aliko
4)Tunamtafuta.
5)Ni mgonjwa.
6)Ana afya..Ni mzima.
7)Ni mgonjwa..amelazwa
Ni huru.
9)Si shahidi
10)Si mtuhumiwa.

NB:Mustafa Mkullo.."Nilienda Washington nikamtafuta sikumpata"
Mh J.Kikwete.."Kifo cha Ballali ni mapenzi ya Mungu"

Ni wakati wa serikali kutoa tamko lao wakati huu ili sisi wananchi tujue moja.

Ni muhimu sana kwa serikali kufanya hivyo kwasababu sasa Ballali ameshakufa na kuna minon'gono kuwa ni serikali yenyewe imeamua kumwua Ballali ili asitajwe tena kwenye kesi ya EPA wala ushahidi wake usitumike.

Na ili pia tukubali kuwa kifo chake ni mapenzi ya Mungu kama vile Mh rais anavyotaka tuamini..

Then maswali ya wananchi kuhusiana na kuhusika ama kutohuisika kwa Ballali yajibiwe ili tuweze kujua mustakabali wa shauri hili tata la EPA.

Tunajua pia kuwa Mh Rais alisema kuwa kamati haiwezi kutaja siri nyingine ili kuepusha uchunguzi usiharibike..Lakini ni wazi kuwa kutaja mashahidi ama watuhumiwa hakuharibu ushahidi bali kutaja waliyosema ndio kunaweza kuwa matatizo.

Serikali haijawahi kusema kama Ballali ni shahidi ama mtuhumiwa na sikumbuki kama wameshawahi kuwataja watuhumiwa ama mashahidi!

Kuwataja watuhumiwa ama mashahidi ni haki ya Mtanzania na serikali inawezekana iliwahoji kina Ballali na wenzake kwa kigezo kile walichokitumia kuwa wananchi wapeleke taarifa.

Serikali pia inaweza kudai kuwa kamati ilikuwa ni ya uchunguzi tu na mshahidi na watuhumiwa watatajwa mara baada ya kesi kufunguliwa rasmi mahakamani! Kwangu madai hayo yatashinikiza fikra kuwa serikali imefanya usanii kwa watanzania!

Ni wazi serikali inaweza kusema kuwa Ballali kama raia wengine naye alipeleka taarifa zake kwa kamati hiyo ya rais.

Na kama imefanya hivyo..Then tunaomba ripoti ili tuweze kujua kuwa nani alikuwa kama shahidi na nani kama mtuhumiwa,pia ni kesi gani watakayoifungua dhidi ya hao watuhumiwa ambao bado haijaamua kuwatangaza licha ya kwamba Dk Slaa alikwisha fanya hivyo pale mwembe Yanga.

Kabla ya kumuhoji Mbowe..Mh Rais aseme ni kwa kivipi amegundua kuwa kifo cha Ballali ni mapenzi ya Mungu!
Kwasababu kifo cha mapenzi ya Mungu kinajulikana...Atueleza yeye ni vigezo vipi hivyo alivyovitumia kusema ni kifo hiki cha Ballali ni kifo chenye mapenzi ya Mungu kama alikuwa hajui kilichomuua!
 
Strong argument mkuu!
 
Halafu bado hawajasema kuhusu wale maofisa saba waliowatuma kum "comb" huko kwenye majiji ya Washington na Boston!
Walishasema walichokifanya wanausalama hao dhidi ya Ballali?
 
Kabla ya kumuhoji Mbowe..Mh Rais aseme ni kwa kivipi amegundua kuwa kifo cha Ballali ni mapenzi ya Mungu!...

Serikali imetuambia, kupitia Waziri Membe, ``Ballali`s death was natural...If you want to prove that this was the case, then have a look at his death certificate. His doctors know what caused his death``

Yeye Membe yeye kaiona death certificate?

Sasa sijui walimtumia fax ya death certificate au vipi. Na kama walimtumia ina maana na yeye alitaka uthibitisho! Alikuwa anashuku nini? LOL

Man, Serikali ya Muungwana ina maajabu sijapata ona!
 
Kama serikali walitumiwa death certificate then hiyo ni siri.
Hakuna anayejua..Ni assumptions tu!
Na nitashangazwa sana kama kuna mtu anaweza kuzitetea kauli flani flani tu za serikali na kuziacha nyingine!
Kwenye post nilizotuma hapo nyuma nimeandika kauli karibu zote zilizowahi kutolewa na serikali...Sasa kama mkuu unaiamini zaidi kauli hii ya Membe ya natural death..Naomba pia uniambie ni kauli zipi kati ya nyingine zilizopita zilizowahi kutolewa na serikali dhidi ya Ballali ambazo pia unaziamini.

NB:Kuna yeyote hapa JF amabaye keshaiona death certificate?
 
Kama serikali walitumiwa death certificate then hiyo ni siri.
Hakuna anayejua..Ni assumptions tu!
Na nitashangazwa sana kama kuna mtu anaweza kuzitetea kauli flani flani tu za serikali na kuziacha nyingine!
Kwenye post nilizotuma hapo nyuma nimeandika kauli zote zilizowahi kutolewa na serikali...Sasa kama mkuu unaiamini zaidi kauli hii ya Membe ya natural death..Naomba pia uniambie ni kauli zipi kati ya nyingine zilizopita zilizowahi kutolewa na serikali dhidi ya Ballali ambazo pia unaziamini.

Membe hawezi kuona death certificate. Alikuwa anabwabwaja tu. Nilikuwa namdhihaki kwamba yeye anaesema proof ya kifo iko kwenye death certicate, kaiona?
 
Sasa nani wa kuhojiwa hapo?
Mbowe mwenye kauli ipi na serikali yenye kauli zipi?
Kipi kihojiwe na kipi kiachwe?
Kusema eti wamuhoji Mbowe wala hawatathubutu kwasababu labda Mbowe naye anaujua ukweli ambao na wao wanaujua!
Kwa hiyo hapo wanaviziana na mataimingi tu..Ila nafikiri upande wenye makali wameushika kina Kada na CCM wao.
HILO HALINA SIRI KWA SASA.
 
hapa patamu kweli kweli!
ccm imepewa fursa nzuri ya kumshtaki mbowe kuwa anawachafulia jina, lakini haiwezi kufanya hivyo kwa sababu inajua kuwa imefanya hivyo na wana wasi wasi kuwa labda mbowe anaweza kuwa anaoushahidi wa waliyoyatenda.!

kama ccm wasafi kwenye hili wangemshitaki mbowe....lakini masikini hawawezi
 
Kada,So far hujasema kwanini Mbowe ahojiwe wakati kuna watu kama akina mramba ambao ndio kiini cha Tatizo.Wewe siku zote unakuja na spidi za kuusapoti ufisadi tu,utaishia kuwa mpiga debe hapa JF tu.

Wewe na SHy hamna tofauti kwani kazi yenu kubwa hapa ni kuharibu hili jamvi.Sijawahi kujua kama kuna watanzania wenye akili zilizo-freeze namna hii
 
Sasa nani wa kuhojiwa hapo?
Mbowe mwenye kauli ipi na serikali yenye kauli zipi?
Kipi kihojiwe na kipi kiachwe?
Kusema eti wamuhoji Mbowe wala hawatathubutu kwasababu labda Mbowe naye anaujua ukweli ambao na wao wanaujua!
Kwa hiyo hapo wanaviziana na mataimingi tu..Ila nafikiri upande wenye makali wameushika kina Kada na CCM wao.
HILO HALINA SIRI KWA SASA.

Mkuu wangu,

Trust me buddy,hawa jamaa hawana guts za kumshitaki Mbowe.Hawa wanajua kutishia tu,tuseme ni mbwa wasio na meno
 
Mkuu wangu,

Trust me buddy,hawa jamaa hawana guts za kumshitaki Mbowe.Hawa wanajua kutishia tu,tuseme ni mbwa wasio na meno

kwa hiyo hii ishu inaendeleaje ?? atahojiwa huyo mbowe au
 
wote hapa jf tunaamini kuwa kuna mkono kwenye vifo hivi, na hizo ndo reflections za mbowe, kuhojiwa sawa labda itasaidia kupata information zingine,

tusisahau historia

dr ouko , akina tom mboya huko kenya walikufa kimzahazaha hivi hivi,
akina askofu luwun kule uganda walikufa kwa jali aliyoitengeneza idd amin, hivyo serikali kuwa na mkono kwenye vifo vya viongozi siyo jambo geni duniani
 
Wana JF, heshima mbele!

Wakati mnajadili Mbowe ahojiwe au la, vizuri kujiuliza maswali ya msingi kutokana na mtiririko wa matukio na sio kuwashambulia watu binafsi (personalities).

Ni kweli Mbowe ametoa matamshi mazito. Yeye kama kiongozi wa chama, ana wajibu wa kujieleza. Tamko lake ni la chama (CHADEMA) au lake binafsi? Pengine, anaweza akawa anajua mengi ambayo sisi hatujui. Lakini, pia kutokana na mtiririko wa matukio na usiri, na maguvu yanatumika kuficha hizo siri, hali iliyopo mpaka sasa hivi, ni mawazo ya mtu yeyote ambaye anawaza vyema ambaye atakuwa atatilia shaka juu ya kifo hiki. Kwa hiyo Mhe.Mbowe kusema kwamba serikali ina mkono wake, yeye ni mmoja tu ya wananchi wengi wenye mtazamo kama wake.

Tunapojadili tamko la Mbowe, tusisahau kuibana serikali. Mhe.Membe amesema serikali haihusiki hata kidogo.Hili ni tamko kutoka serikalini. Yeye kama waziri ambaye amediriki kuweka rehani nafasi yake (kwa kujiuzulu) ikiwa itagundulika vinginevyo. Waziri Membe anaoneka kuwa na siri na uhakika juu ya kifo hiki. Kwa nini naye asiulizwe? Pengine ni kweli serikali haisuhiki, au pengine inahusika ila kutokana na yeye kuwa waziri hawezi kusema vinginevyo hadharani. Inakuwaje suala la Mhe.Membe kuwa na uhakika kwamba serikali haihusiki, wakati mlolongo mzima wa matukio haupati majibu.

Kama serikali haihusiki, Dr.Ballali (RIP) amefariki kwa sababu gani ? Na kama serikali haihusiki kwa nini kuna kuwa na usiri uliogubika mlolongo wa mambo haya ?
Kama serikali haihusiki, kwa nini ulinzi wa hali ya juu umewekwa kwa ndugu wa marehemu? Ni siri gani serikali inayoificha ikiwa kweli haihusiki?

Je, kuna uwezekano Dr.Ballali bado yupo ndio maana serikali haihusiki na "kifo" chake?

Ni mtazamo tu ...........
 
Naomba ufafanuzi.
 
Naomba ufafanuzi.

UFAFANUZI HUU HAPA CHINI MHESHIMIWA, KAMA HAWAHUSIKI NA KIFO KWA NINI WANAMLINDA MAMA YAKE NA KUZUIA WANAOKWENDA KUHANI MSIBA? WANAOGOPA NINI

amaye Ballali alindwa

na Kulwa Karedia

HALI ya ulinzi mkali imeimarishwa nyumbani kwa mama mzazi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) marehemu Daudi Ballali.

Habari za kuaminika zilizopatikana jana nyumbani kwa mama huyo Boko, Dar es Salaam, zinasema kuwa ulinzi huo umewekwa na serikali kupitia BoT tangu kutangazwa kwa kifo cha Ballali wiki iliyopita.

“Tumesikia ulinzi huu umewakwa na serikali kwa kushirikiana na BoT kwamba hakuna mtu yeyote kuingia hapa, tunashangaa sana kuona hata sisi ambao tumekuwa naye hapa tumebaki kuwa watazamaji tu,” alisema Seif Omar, mkazi wa Boko.

Alisema kitendo kilichofanywa na serikali si cha kiungwana, kutokana na ukweli kwamba msiba huwa hauchagui maskini au tajiri wa kwenda kuzika mwenzake au jirani yake.

Tanzania Daima jana ilipofika nyumbani kwa mama huyo anayeishi nyumba namba BNJ/BOKO/1081, ilishuhudia hali ya ulinzi mkali, kitendo kilichosababisha hata mwandishi wa habari hizi kuzuiwa kuingia ndani.

Baada ya kuwasili nyumbani, mmoja wa walinzi wa Kampuni ya Regimental Security aliyekuwa getini, alikataa katakata kufungua geti hilo kwa madai kuwa amepewa maelekezo kutoka ngazi za juu serikalini na BoT.

“Nikusaidie nini, unaitwa nani na una shida gani ndugu…tafadhali nionyeshe kibali chako cha kuingia humu ndani kutoka BoT, na kama huna, nakuomba uondoke eneo hili,” alisema mlinzi aliyekataa kutaja jina lake.

Alisema yeye amepewa maelekezo hayo na maofisa wa juu wa BoT, ambao hakuwa tayari kuwataja majina na kusisitiza kuwa anatekeleza majukumu yake ya kazi.

“Nashindwa jinsi ya kuwasaidia…jamani nawaomba sana muondoke hapa,” alisema mlinzi huyo na kuendelea kufunga geti hilo, kitendo kilichoashilia kuna shinikizo kutoka juu.

Juhudi za gazeti hili kumuona mama mzazi wa Ballali ziligonga mwamba kutokana na hali ya ulinzi iliyopo.

Wakati huo huo, baadhi ya wananchi waliohojiwa na Tanzania Daima kuhusiana na kauli ya serikali juu ya kifo cha Ballali wamesema serikali inapaswa kueleza ukweli baada ya kuuficha.

“Tumeshangazwa na kauli ya serikali, tunaelewa wazi kwamba Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, atakuwa ameelewa ukweli, sasa kwa nini atufiche?” alihoji Dickson Juma.

Alisema kama kifo hicho kisingekuwa cha siri, kwanini serikali ilipata kigugumizi kusema ukweli kuanzia ugonjwa wake hadi anafariki, jambo ambalo linazua maswali mengi.

“Sisi tunasema umefika wakati sasa wa kuelezwa ukweli na kama sivyo, basi iundwe tume haraka kabla ya mambo haya hajapoa, maana tunajua yakipoa, ndiyo yamekwisha,” alisema Juma.

Naye Mwanakombo Hussein alisema kitendo cha serikali kushindwa kushiriki katika mazishi ya Ballali kinaonyesha wazi kwamba kuna matabaka ndani ya viongozi wa serikali.

Aliwataka wananchi wote kuungana na kuishinikiza serikali ili kuhakikisha inaunda tume huru kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina na majibu yatolewe haraka.

Marehemu Ballali alifariki dunia Mei 16 jijini Washington, Marekani, alikokuwa akipata matibabu tangu mwaka jana, baada ya kufukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kuhusishwa na ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ambako zaidi ya sh bilioni 133 zinadaiwa kupotea.

juu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom